Kama nilivyo kuahidi Bro HM Hafif nitachambua kidogo Kutoka katiba ya JM Tanzania kuhusu sifa za kiongozi wa juu yaani Rais na haki za kupiga kura. Tukiangalia Uchaguzi wa Rais Sheria ya 15 ya mwaka 1984, Ibara ya 19 inasema
'
38
.-(1) Rais atachaguliwa na wananchi kwa mujibu wa
masharti ya Katiba hii na kwa mujibu wa sheria itakayoweka
masharti kuhusu uchaguzi wa Rais ambayo itatungwa na Bunge kwa kufuata masharti ya katiba hii''
Na Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania Sheria ya 4 ya mwaka 1992,Sheria ya 13 ya mwaka 1994,Sheria ya 34 ya mwaka 1994 na sheria ya 3 ibara ya 7 ya mwaka 2000 zinabainisha kuwa
39
.-(1) Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa
Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-
(a) ni raia wa kuzaliwa wa Jamhuri ya Muungano kwa
mujibu wa Sheria ya Uraia.
(b) ametimiza umri wa miaka arobaini;
(c) ni mwanachama, na mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(d) anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge au Mjumbe
wa Baraza la Wawakilishi,
(e) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi Mkuu hajawahi kutiwa hatiani katika
Mahakama yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa
kodi yoyote ya Serikali.
Sasa utaona hizo ni sifa za Mtu kuweza kuchaguliwa kugombea uongozi wa juu ndani ya Tanzania.
Kwa haraka haraka tuiangalie tene katiba ya JM wa TZ inasemaje kuhusu haki ya kupiga kura sheria ya 15 ya mwaka 1984 ibara ya 6 na sheria ya 3 ya mwaka 2000 ibara ya 4
5
.-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi
unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa
kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti
mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini
Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
(2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti
yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana
na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
(a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
(b) kuwa na ugonjwa wa akili;
(c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
(d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa
kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama
mpiga kura,
mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote
inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.
Sasa utaona wazi mtu mwenye uraia wa nchi mbili haruhusiwi kabisa kupata ruhsa ya kupata haki ya Kupiga kura. Na kama ilivyo kama huna haki ya kupiga kura basi automatic huna haki hata ya kugombea uongozi katika Tanzania.
Hafif hao ni kwa ufupi tu kuhusu haki ya mtu kugombea uongozi wa juu kuhusu Tanzania. Naeza kuzidi bainisha zaidi lakini naona watu wengi wana jazba kubwa na kutotaka wengi wafaidike na darsa hili.
Lakini kama nilivyobainisha awali nitapembua vile vile sheria za kimataifa zinasemaje kuhusu ili nikijaaliwa Insh'Allah baadayn.
kama kuna suala Naruhusu Bismillah..
Nasriyah Saleh Al Nahdi
Doha. Qatar