Kwanza ningependa kusema hii mada haina maana yeyote kwa sababu utaifa wa Kadinali Pengo unajulikana kuwa ni Mtanzania, nadhani mwandishi wa hii mada aliamua kuleta porojo ambazo hazina maana yeyote kwenye uulizaji wa swali lake.
Lakini kinachoshangaza ni jinsi ya baadhi ya watu wanaoheshimika humu ndani kukurupuka na kuanza kutoa shutuma kwa waislamu na uislamu kana kwamba wana uhakika mwandishi wa porojo hizi anawakilisha uislamu au waislamu, Hivi mna uhakika gani aliendika hii mada ni Muislamu? Ina maana kila mtu anayehoji kitu chochote kuhusiana na Kadinali Pengo basi ni Muislamu?