GE2025 Hivi CCM, hekaheka zote hizi za nini kwenye Self election?

GE2025 Hivi CCM, hekaheka zote hizi za nini kwenye Self election?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Anonymous Caller

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2016
Posts
1,434
Reaction score
1,930
Hii nchi ina vituko sijawahi kuona.
CCM inasumbua watu sana huku matawini.

As I speak, Nimeshangaa Nimekutana na wanafunzi wameagizwa wafuate vitambulisho vyao vya kura majumbani, wawapelekee walimu.

Nikawauliza nyie mmefikisha miaka 18? wakanyamaza. Nikawauliza tena mlijiandikisha na mkapewa vitambulisho? wakajibu ndio. Nikashangaa sana. Nikaenda zangu.

Yaani CCM Pamoja na kubaki peke yao bado wanawaza kufanya ballot rigging, kweeeli!

Mgombea kama Mpina ambaye ipo obvious hawezi kushinda, hata kama uchaguzi nao huwa unadunda...
Eti nae kaenguliwa kwenye presidential race.

Yaani CCM wahonge baiskeli, pikipiki.

Wapige watu, wafunge madhehebu, wahonge wahariri, Wasanii wote wao, media kubwa zote wao, bado wanawaza ballot rigging tena.

Sasa hivi wamegawana mikoa, Samia huku, Nchimbi kule, hii yote kutafuta nini?

Huko chini Watendaji wa mitaa, kata na vijiji ni mwendo wa mchakamchaka wa kupokea maagizo na amri toka juu kuhusu hii Self election ijayo.

Tafakari.
 
Justification ya upigaji kama kawa! Kuna bilion 86 kutoka kwa wanamtandao na zingine 500 ujue kutoka hazina ya kengez!

Wataretire vipi sasa kwani?
 
Akili yao imeshamezwa na tamaa na ufisadi hawajali kuhusu raia wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom