Hivi CCM inaweza kuchukua mtu aliyekuwa wa mwisho kwenye kura za maoni apeperushe bendera?

Hivi CCM inaweza kuchukua mtu aliyekuwa wa mwisho kwenye kura za maoni apeperushe bendera?

budagala

Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
75
Reaction score
137
Kwa utaratibu uliowekwa na CCM kwa wagombea kutofanya Kampeni kwenye kura za maoni,ni wazi sasa wote waliopata kura moja au sifuri ndio ambao hawajatoa rushwa au kukutana na wajumbe.

Swali ni je CCM ambayo huchukua mshindi wa kwanza hadi wa nne,inaweza kuvunja utaratibu mwaka huu na kuchukua hadi washindi wa mwishoni kabisa waliopata kura moja au sifuri?
 
Mhhh! Inategemea na lengo la CCM. Kama lengo ni kupata watu bora kuendesha serikali, hiyo ni halali kabisa! lakini wanaweza kuwa na lengo na kuongeza namba ya wabunge tu: kumbuka kule Bungeni kila mtu ana umuhimu wake. Wengine ni washangiliaji tu, inatosha!
 
Wapo ambao hawajatoa kabisa na walionekana siku ya kuchukua fork na kupigiwa kura tu..mimi nina classmate wangu aligombea kigamboni na kapata kura tano hajatoa hata mia zaid ya hela ya form tu
 
Wapo ambao hawajatoa kabisa na walionekana siku ya kuchukua fork na kupigiwa kura tu..mimi nina classmate wangu aligombea kigamboni na kapata kura tano hajatoa hata mia zaid ya hela ya form tu
Jamaa yako katisha kamfunika mpaka Mpoki.
Au ndio mzee wa tokomeza zero
 
Wakifanya hivo ndo vizuri ili majimbo mengi yaende upinzani, maamuzi ya wajumbe yaheshimiwe
 
Wakifanya hivo ndo vizuri ili majimbo mengi yaende upinzani, maamuzi ya wajumbe yaheshimiwe
Ingekua ni ccm ile ya miaka iliyopita mwaka huu majimbo mengi sana yangepita na upinzani maana mfumo wa safari hii ni waovyo kupata kutokea ila ndo hivo tena magu hatak utan linapokuja suala la ccm kupita
 
Ndio mfano mwaka 2015 Dodoma makao makuu nafasi za 3 bora Amina salum Ali alishinda kwa kura nyingi za ugombea urais wa mungano lkn hakupewa yy kapewa mwengine
 
UTARATIBU WA CCM MBAYA SANA WATU WAMEPIGA KAMPENI ZA NYUMBA KWA NYUMBA MI NIPO SINGIDA VIJIJINI WALIOSHINDA ASILIMIA KUBWA WALIGAWA HELA USIKU KWA USIKU TENA RUSHWA HAPEWI MJUMBE ANAPEWA ASIYE MJUMBE NDIO AGAWE WALIOSHINDA KIHALALI WACHACHE SANA
 
Ndio mfano mwaka 2015 Dodoma makao makuu nafasi za 3 bora Amina salum Ali alishinda kwa kura nyingi za ugombea urais wa mungano lkn hakupewa yy kapewa mwengine
Huyu namfahamu Sana kwanza ameoa, asingeweza kukaa na j hata miezi 6.
 
Back
Top Bottom