1. Maridhiano ya kweli au maigizo ya kisiasa?
- Tumekuwa tukisikia kauli za “maridhiano” kati ya CCM na CHADEMA, lakini ukitazama Kwa makini vitendo vinavyoendelea, ni vigumu kuona dhamira safi ya hizo kauli za maridhiano.
- Serikali hii hii inayosema inaleta amani na maridhiano, ndiyo hiyo hiyo inayomkamata na kumfungulia kiongozi wa CHADEMA kesi nzito ya uhaini.
- Mahakama – ambazo wananchi wengi wanahisi zipo chini ya ushawishi wa chama tawala – zimewapiga marufuku CHADEMA kufanya siasa hadi kesi ya mgawanyo wa mali imalizike. Je, hili ndilo “daraja la maridhiano” au ni mtego wa kisiasa?
2. Kiini macho cha maridhiano:
- Watanzania milioni 60 tunaambiwa kuna “muafaka,” lakini chini ya kapeti, CHADEMA wanachezeshwa michezo ya kitoto na kuhujumiwa kisiasa.
- Maneno ya “tusameheane” yanaimbwa hadharani, lakini nyuma ya pazia kuna vitisho, kesi za kubambikiziwa na kufungwa kwa milango ya siasa.
- Swali la wazi: Kama maridhiano ni ya kweli, kwa nini viongozi wa upinzani wanateseka mahakamani na kuzuiwa kufanya shughuli za kisiasa?
3. Kauli ya Polepole: “Wahuni wa mtandao wamefanya state capture”
- Polepole mwenyewe amekiri hadharani kwamba kuna mtandao umeiteka dola – “state capture.”
- Ikiwa dola imechukuliwa na “wahuni wa mtandao,” je, Mama Samia anajua ukubwa wa tatizo?
- Wassira, ambaye sasa anaongoza wimbo wa “maridhiano,” anapuuza ukweli huu na hata hataki kumwambia mwenyekiti wake wa chama – acha maigizo, kwanza vunja mnyororo wa kesi za kubambikiziwa CHADEMA, halafu ndio mambo mengine yafuate.
4. Dhamira ya kweli inahitajika, si maigizo ya kisiasa
- CCM na serikali yake lazima zionyeshe dhamira ya kweli kwa kuachana na maigizo ya “maridhiano” huku wakitesa upande wa pili.
- Mama Samia ana nafasi ya kuandika historia nzuri – au kubaki kumbukumbu ya kiongozi aliyefunika maovu kwa maneno matamu.
- Ujumbe muhimu: Maridhiano si maneno mazuri kwenye mikutano; ni vitendo vya haki na usawa mbele ya sheria.
5. Kwa nini kuwasumbua watu kupiga kura kama matokeo tayari yanajulikana?
- Kila kona ya nchi, watu wanalia kwa mabadiliko, lakini bado wanabebeshwa mzigo wa siasa zisizo na matumaini.
- Kama chama tawala tayari “kina watu wake,” kwa nini kuendelea kuwalazimisha wananchi wapige kura kana kwamba sauti yao itahesabika?
- Uchaguzi ni mzigo wa heshima ya taifa – si maigizo ya kuhalalisha maamuzi ya wachache.
6. Nchi ni yetu sote, si ya wanamtandao pekee
- Kauli ya Polepole kuwa “wanamtandao wametekeleza state capture” inamaanisha wazi kuwa dola imekuwa mali ya wachache.
- Kwa haya mambo ya “polepole,” ni wazi sasa rasilimali za taifa zimepigwa mnada kwa wanamtandao.
- Tukifikia hatua ya vurugu, nani atalaumiwa?
- Mzee wa Taifa Gas?
- Mstaafu Kikwete?
- Au Mzee Wassira na maridhiano yake feki?
7. Mama Samia, chukua hatua kwa manufaa ya taifa na yako binafsi
- Mama Samia, historia inakuangalia. Kila ukichelewa, maigizo haya yanachoma imani ya wananchi.
- Maridhiano ya kweli hayahitaji kesi za kisiasa, vitisho au michezo ya mahakama – yanahitaji dhamira safi.
- Watanzania milioni 60 wanataka mabadiliko na ukweli, si maigizo.
CCM, serikali na viongozi wake – muache maigizo. Muwe na ujasiri wa kufanya maridhiano ya kweli au semeni wazi kuwa hamtaki. Hii nchi ni ya wote, na kila tone la unafiki linatugharimu zaidi.