Hivi, CCM tunamtapeli na kumlaghai nani kuhusu kuichukia rushwa uchaguzini?

Hivi, CCM tunamtapeli na kumlaghai nani kuhusu kuichukia rushwa uchaguzini?

Umeisoma wapi hii mkuu, au ni utafiti mpya ulioufanya na kugundua sababu hii ndio iliyosababisha aondolewe madarakani?

Kama wewe ni mwalimu unawalisha ndimu vijana nao wanakuwa na elimu potofu kama uliyonayo wewe.

Haya ndio matatizo yanayoiandama Tanzania kwa kasi sasa, maanake serikali yenyewe ndio kimekuwa kiwanda cha kusema uongo.

Sasa hata wananchi wenyewe tunawaunga mkono kwa kusema uongo.
Asante wewe msema kweli....
 
Hata wewe kama una sifa za kibunge yaani unajua kusoma na kuandika unaruhusiwa kugombea Uspika bwashee siyo lazima uwe mbunge!

Naibu Spika ndio lazima awe mbunge.
Nimekuelewa.

This will be new to me, labda uniambie kwa experience yako umeshawahi kushuhudia hili before kwenye bunge letu?

If No. Am waiting anxiously.
 
Nimekuelewa.

This will be new to me, labda uniambie kwa experience yako umeshawahi kushuhudia hili before kwenye bunge letu?

If No. Am waiting anxiously.
Ndio..... Mzee Marando amewahi kugombea Uspika

2015 Chadema iligombea uspika kupitia mwanachama wake ambaye hakuwa mbunge alitokea Arumeru jina nimesahau!
 
Ndio..... Mzee Marando amewahi kugombea Uspika

2015 Chadema iligombea uspika kupitia mwanachama wake ambaye hakuwa mbunge alitokea Arumeru jina nimesahau!
Kugombea lakini hakushinda, hata hao wa upinzani wengi huwa naona hawana nafasi kubwa ya kushinda but wengi huwa wabunge, nataka yule ambaye anatoka kwenye kada nyingine tofauti kabisa na siasa halafu achaguliwe kuwa Spika wa bunge.

Naamini itakuwa expirience fulani amazing ya kufungua akili.
 
Kugombea lakini hakushinda, hata hao wa upinzani wengi huwa naona hawana nafasi kubwa ya kushinda but wengi huwa wabunge, nataka yule ambaye anatoka kwenye kada nyingine tofauti kabisa na siasa halafu achaguliwe kuwa Spika wa bunge.

Naamini itakuwa expirience fulani amazing ya kufungua akili.
Huyo utamuona mwezi November, 2020!
 
Kisiasa, unapoisha uchaguzi mmoja maandalizi ya uchaguzi mwingine huanza. Maandalizi ya uchaguzi wa mwaka huu 2020 (kuihusu CCM pekee) yalianza tangu mwaka 2015. Makada walijipanga kutetea majimbo na kata na wengine wakitamani kuzipoka kata na majimbo kutoka kwa wasasa. Maandalizi ya kiuchaguzi hayakufanyika kwa wapinzani tu. Wao waliminywa vya kutosha na kutisha na kulazimishwa kufanya mambo yao ya kisiasa kimyakimya na sirini kama kuuza gongo, bangi au ngada.

Makada wa CCM, kabla ya maigizo yaliyoanzishwa jana ya kutoa namba ya simu ya kuripoti vitendo vya rushwa, walishatoa rushwa na kujijenga ipasavyo. Tazama ayafanyayo Naibu Spika Dr. Tulia kule Mbeya. Amekuwa akijibanza kwenye taasisi yake ya Tulia Trust kugawa rushwa na kusaka ushawishi ili aweze kugombea na kushinda jimbo la Mbeya Mjini linaloshikiliwa na CHADEMA. Mtazame Silvestry Koka wa Kibaha Mjini. Ameshagawa baiskeli na pikipiki kwa makada wa CCM tayari kutaka kuutetea ubunge wake. Majimbo yote hali ipo hivyo, wataripotiwa wangapi? Watafanywaje?

Rushwa, as always, imeota mizizi na kutamalaki ndani ya CCM. Rushwa ndiyo inayowapa ushindi makada ndani ya CCM na hata kwenye uchaguzi mkuu. Rushwa ni njia pekee ya kuibuka kidedea huku ukichekelea ndani ya CCM. Mafao ya Ubunge mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge ndiyo hutumika kugawa mahela kwa makada na wananchi na kuwawezesha watu kutetea viti vyao. Ni vichekesho, utapeli na ulaghai kusema kuwa CCM inachukia rushwa. Sisi wanaCCM tunajua ukweli huo. Hakuna haja ya kudanganyana.

Kazi ya kupambana na kuzuia rushwa ni ya TAKUKURU. Lakini, wakati kama huu wa uchaguzi, CCM ndiyo huwakingia vifua makada wake wanaotiwa mbaroni kwa rushwa na kuwaharibia kazi TAKUKURU. Inashangaza kutapeli na kulaghai wananchi kuwa chama chetu cha CCM kinachukia na kupambana na rushwa. Ni ajabu inayofaa kuingia kwenye kitabu cha maajabu ya kidunia.Wananchi wamekosa nini hadi wadanganywe na kulaghaiwa kiasi hiki? Kinaendelea nini kwenye kukamatwa kwa Rage kule Tabora?

Uchaguzi ndani ya CCM bila rushwa hauwezekani!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Nzega, Tabora)
Wanafanya maigizo mwanzo mwisho,unyama waliowafanyia wapinzani kwa miaka mitano iliyopita hata shetani anawaogopa.
Wanatisha,awamu zingine walikuwa wanafanya kwa kificho na ustadi.Sasa hivi wamekuwa hatari, mchana kweupe MTU anakatwa mapanga,wengine wanatekwa,baadhi wamejeruhiwa vibaya,wengine wameunga mkono juhudi,wengine wamepotea au kuuawa na hakuna hatua zozote kuwasaka wahusika.Majuzi tumeona wahuni wanasafirishwa kufanya fujo,kushangila na kulaghai wasioelewa mbinu zao.
Watanzania tusipozinduka,huko tuendapo kutakuwa na makubwa zaidi.Kipindi cha kwanza kwa awmu tatu zilizopita walikuwa wanawafurahisha wananchi na kutoa huduma ili kipindi cha pili kisiwe kigumu sana,ila CCM mpya yangu waingie ni visasi full volume kwa wote.Hakuna aliyenusurika kuanzia wakulima,wafanyabiashara,wavuvi,wafanyakazi,machinga,wastaafu,wahitimu nk.kila moja ameonja chungu.Kweli tumelimia nawe.Huyu anategemea kura halali kushinda?Mbona anajiamini hivi na asilimia za ushindi washapanga.Watapata hizi kura kwenye madaraja,Barbara za lami,sgr,Stigler's,Flyovers au kwa wananchi?
 
Asante wewe msema kweli....
Hivi ile 'skando' yake inaitwaje vile, "WtaerGate"? Mbona hata hukuitaja mkuu, maanake hiyo ingeonyesha ufahamu mkubwa ulio nayo juu ya jambo hilo la Nixon na kujiuzuru kwake.!
 
Nawaangalia weeee wale tausi waliogawiwa kwa wazee wetu kwa jicho la tatu [emoji41]
 
Back
Top Bottom