Elections 2010 Hivi CHADEMA haina wataalamu, au viongozi wake ndiyo wasioambilika?

Nikisema nawe ni mhuni nitakuwa nimekosea? Soma mara mbili bandiko lako na utajua kwa nini nimediriki kukuita mhuni.
 
Unahitaji kuiedit kazi yako uliyoi paste hapa manake haileti hamu ya kuisomaa, weka paragraphs ivutie mkuu!
 
Dabomani umetumia nguvu kubwa sana kujaribu kuonyesha ahadi za Slaa hazitekelezeki. Hata hivyo, ni kama kumpigia mbuzi gitaa, midundo yako haichezeki. Haichezeki kwa kuwa imekosa ushahidi wa kisayansi. Bahati mbaya kwako ulidhani unahutubia mkutano wa hadhara ambao watu watakusikiliza na kukuacha uende zako. Hapa no mzee. Kwa kifupi ahadi zote za Chadema zinatekelezeka. Mpe kura yako tarehe 31 Oktoba halafu uje umpime kwazo 2015.
 

Sikonge,

Wana ccm wengi wana makengeza ... wanaona tu upande mmoja
 
Dabomani,
Mkuu wangu kusema kweli sijakuelewa kabisa ktk mada hii unazungumzia vitu vikubwa kwa kutumia mifano midogo sana isiyolingana. Unazungmzia Alibaba.com kama soko kubwa sijui nani alokwambia hivyo ndivyo Utawala bora unavyowaandaa wananchi wake.

Pili, swala la Usafiri wa reli leo hii hatuna kabisa, hivyo kuufikiria tu umuhimu wake unatosha kwa mwenye elimu na msomi kama wewe kukubali haja ya kuwa na usafiri acha hizo ahadi za masaa kuwa kigezo kikubwa cha Upinzani wako. Yaani hapa swala kubwa kwako ni masaa mangapi mtu ataweza kutoka Dar kwenda Mwanza badala ya kuzungumzia Usafiri wa reli ambao kichwa kimoja kinaweza vuta mabehewa 60 hadi 100 yenye mali inayoweza kubebwa na malori 200 kwa usafiri wa siku nne kufika hadi Mwanza..

Sasa hapa napata mshangao mkubwa sana kwa msomi kama wewe kuzungumzia zaidi ahadi ya masaa badala ya kufikiria kwanza uwezekano wa kuwa na usafiri wenyewe na upi unaotufaa kulingana na mahitaji yetu bila kusahau uwezo wetu..

Tatu, umezungumzia swala la Saruji na kusema kwamba Clinker inaagizwa China sijui ndio wanauza bei rahisi, wewe umefanya utafiti na kujua kwamba Tanzania hatu produce Clinker? Je ikiwa Hiyo jasi ndio tunaagiza na sii Clinker kuna uwezekano wa saruji kuuzwa bei ya Tsh. 5000 maanake sijui kama kweli msomi wewe umefanya utafiti wa kutosha. Ebu rudia tena kutafiti kisha rudi na majibu yenye kuleta maana.

Mkuu ni bora zaidi mtu uzungumzie mapungufu ya sera za Chadema kwa kuorodhesha yale yanayowezekana kufanyika na sii habari ya gharama kwani hiyo hiyo cement kutoka nchi jirani inauzwa bei nafuu sana kuliko hiyo inayotengezwa nchini na kwa mfano wako sijui hao wenzetu waliweza vipi kukabiri gharama za Clinker. tena hujaweka gharama zaidi ya walanguzi ambao wanaitoa cement nchi za majirani na kuingiza nchini.

Ifike wakati watu tufikirie zaidi Maendeleo ya nchi kwa hisia za Ushindi na sii kutumia lugha ya KiCCM kwamba HAIWEZEKANI hali kitu kinawezekana kabisa.
 
Katika watu wenye utumwa wa kiakili ni huyu jamaa alieandika this baseless and pointless topic,

yeye kama kapewa hela na kuwekwa pale upanga ili aanze kuandika utumbo tunampa pole. Ukombozi ni lazima na kwa sasa tunayo elimu nzuri ya urai

yote anayosema drkt wa ukweli yanawezekana provided hao waliomtuma kuandika hayo wasiibe kura.

Kwanini tuandikie mate wino upo, tumpe nafasi drkt uone kazi itakavyofanyika, kwanini tuwe na baraza la mawaziri 46???? Eti kisa unalipa fadhili!!!!!! Wakati watanzania milion 42 wanateseka, tunataka drk slaa akabadili katiba ya kinyonyaji, tunataka drkt slaa akatoe elimu bure na afya bure, tunataka drkt slaa akasikie kilio cha watantanzania kwa kurudisha uwajibikaji-sio hao waliokutuma kuandika mtu anaandikwa fisadi weeeeeee rais anajifanya kiziwi na bubu, tunataka rais muwajibikaji hatutaki rais anaewachekea mafisadi, tunataka rais anapanga mipango ya kuwafanya watanzania kuwa na makazi bora, inawezekana kwa serikali inayowajiba acha umbumbumbu, na kujiita wewe mtaalam. Jamani inawezekana tunataka rais anaeangalia mfumuko wa bei sio anaechangia mfumuko wa bei, tunataka rais who can demonstrate walk the talk, tuliambiwa eti ninawafahamu mapapa nitawafikisha mbele ya dola leo hii mtu huyohuyo anawapigia debe mafisadi sijui ramba, chnye, richmond jamani kama kweli unataka kupima wapi kuna wataalamu tulinganishe chadema na ccm? Hata mtu wa mtaani tuuu hawezi kumpeleka mtu mahakamani kwa ufisadi then akaja kumpigia debe, are we real serious????? Wanafungwa watu walioiba kuku hawa wanaombewa kura hivi hii si dharau kweli??? Tuseme kweli?? Labda wafanye vinginevyo lakini hapa hawachomoki kwa drkt slaa -aliepata udkt mwaka 1982 achana na drk za sura, naweza kesha hapa lakini madudu ni mengi tumeyaona -mwalimu nyerere alisema ccm sio baba yetu ni wakati muafaka umefika, katika kitu ambacho drkt slaa amefanikiwa kwa sasa ni elimu ya uraia na kujiamni, you cant fool all people all the time, sawa fanyeni mfanyalo sasa lakini kumbukeni you cant fool all people all the time, we need slaa and people like slaa we know them-mwakyembe good example, magufuli good example but for sure they cant do more ndani ya uchafu tunaouona, if we get a team of peole like tundu lisu, zito, mbowe, mwakyembe, mpandozoe, marando,young fighters like halima mdee, waitara, godbless lema, mwanza man, john mnyika, but also put lipumba as economic advisor-while slaa is presidar, nakwambia patawaka moto -foleni hatutaiona dar, mshahara kima cha chini 350000/=, nyumba nzuri zitajengwa na mifuko ya jamii, afya na shule bure, mikataba ya kinyonyaji mwisho, katiba mpya, na mwisho demokrasia ya kweli na maisha bora.
 
Jamani mambo ya kusema hatuwezi ndo kuendelea kuwa jalala la vifaa vibovu kila mwaka. Tunataka viongozi wabunifu siyo viongozi wenye tamaa, hata kutatua matatizo ya mahitaji ya kila siku hawawezi. Kiongozi anatakiwa kuonyesha njia wapi twende na wapi tusiende kwa wakati muafaka.

Train kwenda mwanza kwa masaa 3 inawezekana, kama haiwezekani tulishajaribu hata hiyo yenye kutumia siku moja? Hebu mtu aseme hapa kuna nini cha kujivunia Tanzania tunachotegemea baada ya muda fulani tutakuwa tumengeneza au tutakuwa tunauza nje?

Ni aibu kuwa wateja kila wakati bila kujiuliza kwa nini hatuuzi? Tuache ubishi, Dr Slaa anaweza kurudisha uzalendo ktk nchi yetu
 

Miongoni mwa wagombea uraisi ambao wamekuwa wakitoa ahadi ambazo kwa mtizamo wangu zina walakini mkubwa, ni Dr. Slaa wa CHADEMA. Miongoni mwa ahadi hizo ni ile ya kuweka treni ya masaa matatu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam, na ile ya kushusha bei ya saruji hadi shilingi 5,000.00 kwa mfuko wa saruji wa kilo 50.
Inawezekana CHADEMA haikuwa na nia ya kutudanganya, lakini wanawezaje wakajitetea kuwa wamekuja na ahadi nzito kiasi hicho bila kufanya utafiti? Tangu kampeni hizi zimeanza chama hiki kimefanya makosa mengi mno ya kiufundi na ya wazi, kiasi kwamba mtu unabaki ukiwa umepigwa na bumbuwazi. Ni vipi chama kichanga kiasi hicho kiwe na matumaini ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi? Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba viongozi na wagombea wake wawe wanatoa ahadi baada ya kuzifanyia kazi; vinginevo watagundua kuwa Watanzania wanaowadhania ni wajinga, kumbe ni wajanja kuliko wao.
[/QUOTE]


Wewe ni mjinga kwelikweli ama unataka kuwadanganya watu kwa makusudi. Lazima uwe mnufaika wa uongozi dhaifu na m-bovu ulioko madarakani ama mwenyewe pia ni m-bovu japo wadhani kuwa ni mtaalamu.
Kwanza suala la umbali kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam kuwa km 1,200 ni uongo. Kwani ndege kubwa hutumia saa moja na hakuna ndege yenye kasi ya kilomita hizo kwa saa. Huo umbali unaousema wewe ni huu wa njia za treni za mwaka 47. Wala treni ya kasi kiasi hicho usidhani itatumia njia chakavu zilizopo, wala mfumo m-bovu wa umeme uliopo sasa. Ni lazima ziwepo njia mpya tena za mkato na umeme wa uhakika. Hivyo umbali kutoka Dar hadi Mwanza unaweza kupunguzwa kiasi kikubwa. Pili, umeendeleza upotoshaji wako kutaka watu waamini kuwa treni hiyo ni mradi wa miaka mitano. Si kweli, usimuwekee Dr. wa kweli maneno mdomoni mwake – anayo ya kwake makini na ya kutosha. Ukitaka kuwa muongo mzuri (kama unavyojidhania kuwa) basi uwe pia na kumbukumbu. Alichosema Dr (wa ukweli aliyesomea si kupewa kama ruzuku) ni kuwa umefika wakati tuwe na mipango ya maana ya taifa ya muda mrefu (visheni/maono). Hivyo wakati binadamu wenzetu wanafikiria kutua kwenye sayari za mbali basi nasi angalau kwa miaka 15 ijayo tuwe na treni ya kasi hiyo. Ikiwa sasa zipo treni zenye kasi ulizoelezea (km 250 hadi 400 kwa saa) ni dhahiri katika kipindi cha miaka hiyo 15 mambo yatakuwa bora zaidi. Usipoteze muda wako kudanganya kuwa ni ahadi ya miaka mitano, si kweli. Mwaka huu Watanzania tulikwisha kuweka wazi na kukuonya kuwa “hatudanganyiki”!
Pili ni kuhusu sementi. Mpaka sasa ni kiasi kidogo sana cha klinka ambacho kinaagizwa kutoka nje ya nchi. Haifiki hata asilimia tano. Sehemu kubwa inatoka hapahapa nchini na huzalishwa na malighafi zinazopatikana karibu kabisa na viwanda husika. Klinka si malighafi bali ni zao la kati (intermediate product) katika uzalishaji wa sementi. Kiwanda cha Twiga Cement na Tanga ndivyo vina mipango hiyo ya kuagiza klinka lakini ni nyakati za mahitaji makubwa tu. Hivyo ni kiasi kidogo mno. Pia ufahamu kuwa hivi sasa kuna viwanda kadhaa (kule Tanga [Arthi River Mining], Mtwara, Dar es Salaam) ambavyo viko kwenye hatua mbalimbali za ujenzi kwa ajili ya kuzalisha saruji. Kiwanda cha Wazo kina mpango wa kufanya upanuzi wa kiwanda na ukarabati unaendelea sasa kwenye moja ya chungu (500 t/day kiln) cha kuzalishia klinka. Hivyo ni uposhaji mkubwa kuchukua bei ya klinka ya China na kuiweka kuwa ndicho kipimo cha sementi ya Tanzania.
Labda wasomaji wajue tu kuwa hiyo klinka huzalishwa kutokana na madini ya chokaa ambayo kwa lugha za wenzetu huitwa limestone, udongo mwekundu (red soil), mchanga wa mtoni (river sand), (wakati mwingine madini ya chuma), gypsum na vikorombwezo vingine vyenye lengo la kupunguza kiasi cha klinka kwenye sementi. Kwa upande wa Tanga na Mbeya ili kupunguza klinka wao hutumia pozzolana, aina ya klinka ambayo ilitengenezwa zamani na volcano, ambapo wanaweza kutumia hadi asilimia 35. Kwa mfano sementi za Tanga tunazotumia moja (Ordinary Portland Cement) ina klinka 80%, madini ya chokaa 15% na gypsum 5%, nyingine Pozzolana Portland Cement ina klinka 60%, pozzolana 35% na gypsum 5%. Madini yote haya hupatikana kwa wingi mno hapahapa Tanzania. Pozolana inayotumika Tanga sementi hutoka Holili na gypsum hutoka Makanya (Kilimanjaro). Ile pozolana ya Mbeya wanachota karibu kabisa na kiwanda. Twiga sementi wao hupata gypsum yao kutoka Makanya, Lindi (gredi ya juu kabisa) na Itigi.
Ni dhahiri kukiwa na mipango mizuri (kama ya CHADEMA) utashi na nia thabiti (wala si nia zaidi) inawezekana kabisa kuuza mfuko mmoja wa saruji kwa shilingi elfu tano. Kwani wakati Kikwete anaingia madarakani mfuko wa sementi ulikuwa shilingi ngapi? Kwa tarifa yako ilikuwa bei hiyohiyo anayosema Dr. wa kweli. Kuuza kwa shilingi elfu tano ni sawa tu na kuondoa uharibifu wa miaka mitano uliofanywa na serikali mbofu (mkangafu) na dhaifu iliyopo madarakani. Unajua sementi ya Kenya ingeuzwa kiasi gani kama si kodi za kulazimisha inayotozwa? Hivi unajua nyumba bora ina thamani kiasi gani katika kupunguza (adui) maradhi na kustawisha maisha ya Watanzania? Hata kama ikibidi kutoa ruzuku ni sawa. Ruksa!
Tueleze wewe mtaalamu, zile ruzuku wanazopewa makampuni makubwa ya (matajiri) madini kwa njia ya msamaha wa kodi, serikali yako tukufu inazitoa wapi? Kwa nini hasa unapinga hatua makini za kuwakomboa Watanzania? Mwenzetu una nyumba na hutaki na sisi tujenge? Unapodhamiria kujenga taifa kama letu si lazima kila kitu kiwe na mantiki ya kiuchumi. Taifa kwanza!
Sasa lazima tufanye uamuzi. Kuwezeshwa kujenga au kuyawezesha makampuni ya matajiri kupora madini yetu? Kuendeleza reli chakavu au kuanza kufikiria na kutekeleza njia za treni za kasi? Tuchague, maana kupanga ni kuchagua, kila mmoja wetu aweze kutibiwa bila malipo anapougua ama tulipie na serikali ichagie huduma duni za matibabu?. Tarehe 31 Oktoba tuseme kwa sauti ya kusikika kama tunataka watoto wa taifa hili wasome kwa kadri ya akili zao au kwa kadri wa uwezo wa kifedha wa mifuko ya wazazi wao? Hayo ndiyo ya kuamua wala si uwongo uliouweka mtoa kiroja.

Dawa ya Mjinga ni kuumia
 

Miongoni mwa wagombea uraisi ambao wamekuwa wakitoa ahadi ambazo kwa mtizamo wangu zina walakini mkubwa, ni Dr. Slaa wa CHADEMA. Miongoni mwa ahadi hizo ni ile ya kuweka treni ya masaa matatu kutoka Mwanza hadi Dar es Salaam, na ile ya kushusha bei ya saruji hadi shilingi 5,000.00 kwa mfuko wa saruji wa kilo 50.
Inawezekana CHADEMA haikuwa na nia ya kutudanganya, lakini wanawezaje wakajitetea kuwa wamekuja na ahadi nzito kiasi hicho bila kufanya utafiti? Tangu kampeni hizi zimeanza chama hiki kimefanya makosa mengi mno ya kiufundi na ya wazi, kiasi kwamba mtu unabaki ukiwa umepigwa na bumbuwazi. Ni vipi chama kichanga kiasi hicho kiwe na matumaini ya kupewa ridhaa ya kuongoza nchi? Ushauri wangu kwa CHADEMA ni kwamba viongozi na wagombea wake wawe wanatoa ahadi baada ya kuzifanyia kazi; vinginevo watagundua kuwa Watanzania wanaowadhania ni wajinga, kumbe ni wajanja kuliko wao.
[/QUOTE]
 

Utashangaa wanaoamini uongo wa Dr Slaa wanasema "HATUDANGANYIKI." Tatizo hapa ni kwamba anayepiga mahesabu ya kiuchumi ya Chadema ni MGOMBEA MWENZA

Tukija kwenye ahadi ya kuuza mfuko wa saruji kwa shilingi 5,000/- tu, hapa napo inabidi tujiulize: Hivi CHADEMA haina wataalamu wa uchumi, au mgombea wao ndiye asiyeambilika?

Hapo sina jibu, ila kama waliweza kuandika historia kwa kumsimamisha mgombea mwenza wa darasa la saba, it is possible kwamba hawana wachumi wakweli.
 
Dawa ya Mjinga,

Labda huyu jamaa asome pia hapa apate kuona kwamba tumekatisha hata production ya Clinker huko Mbeya kutokana na soko na kikubwa zaidi Uongozi mbaya wahao wasomi wetu..Bofya
 
aiseeeeeee ulikuwa na muda kiasi hiki kuandika pumba hizi bora ungeenda kulima anyaway utakuwa umepewa something ili ujipoze mpe hi makamba:blah:
 
Unaweza kuwa ni miongoni mwa walimbukeni wengi huko chadema kwa kutetea upupu huu pasipo udhibitisho rasmi. Umbali toka Dsm mpaka Mza kwa treni ni km 1260 hivi. Tena kumbuka vizuri ni kwa treni! Kwa barabara umbali huo unaweza kupungua kwa asilimia kadhaa, na kwa usafiri wa anga unapungua kwa asilimia kubwa.

Ukipima umbali huo moja kwa moja toka kwenye ramani, utapata kilometa 850.20 hivi. Na sijawahi kuona reli iliyoonyoka toka pointi A hadi B kama ambavyo wewe unavyotaka kutuambia hapa!

Reli ya kati imepita katika mikoa zaidi ya minne(Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Shinyanga, na Mwanza), sasa wewe na slaa wako mnataka kutuambia kuwa mtajenga reli mpya bila kupita katika mikoa hiyo? Mtaipitisha angani nini? Je wananchi wa mikoa iliyobaki wasahau huduma hiyo muhimu kwao kwa usafiri?

Treni ya sasa yenye kutumia diseli inakwenda kilomita 65 kwa saa, na ina vituo vingi, ndio maana inachukua karibu masaa 39 kufika Mwanza ilhali ndege yenye kutumia injini za jet inachukuwa sio zaidi ya saa moja. Usafiri kwa barabara sasa upunguza umbali, kwani asilimia 90 ya barabara hiyo ipo katika kiwango cha lami, hivyo kuruhusu magari madogo kusafiri zaidi ya kilomita 100 kwa saa, mabasi kilomita 80 kwa saa (ingawa madereva wengi wa mabasi hayo uendesha km 100-120 kwa saa) na malori ya mizigo km 80 kwa saa.
 
Nimeshindwa kusoma. Ni ndefu sana na Maelezo ni mengi na tangu mwanzo haionekani wataka kusema nini hasa kiasi kwamba imeninyima ladha ya kuisoma.
 
Nimeshindwa kusoma. Ni ndefu sana na Maelezo ni mengi na tangu mwanzo haionekani wataka kusema nini hasa kiasi kwamba imeninyima ladha ya kuisoma.
Mkuu MF
Kama umeshindwa kuisoma yote, nini sababu ya msingi ya kukoti jamvi lote hilo? Si ungeandika tu kwamba umeshindwa kusoma? Kajamvi haka kanakutia uvivu wa kusoma? Vipi umeshamaliza kusoma sera na ilani ya Chadema?
 
Mkuu MF
Kama umeshindwa kuisoma yote, nini sababu ya msingi ya kukoti jamvi lote hilo? Si ungeandika tu kwamba umeshindwa kusoma? Kajamvi haka kanakutia uvivu wa kusoma? Vipi umeshamaliza kusoma sera na ilani ya Chadema?

Mkuu Kibunango, kwa hili niko na Mchukia Fisadi...hii posting inatia kizunguzungu kuisoma. Imenichukuwa muda kupata point iliyokusudiwa. Kusoma Ilani nadhani ni tofauti na kusoma postings za JF, ilani unaweza kuisoma kipengele kimoja kwa siku.
 
Mwenye uvumilivu wa kuusoma mpaka mwisho huo upupu na kukubaliana nao, ampigie kura Kikwete. Sisi tulio na kiu ya maendeleo tutampigia kura Dr. Slaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…