Hivi CHADEMA walitaka wajisifie kuwa na jengo zuri au Siasa na Demokrasia nzuri za kuikomboa Tanzania?

Na wapuuzi tuh ndio wataendelea kuishabikia chadema.siasa za chuki ni mbaya kwa taifa.magu alivokua akiwaadabisha tuliwaonea huruma xnaa,ila saiv naona jamaa alikua sahihi mbowe c mtu mzur kabisa na masuala ya ukanda na ubaguzi wa kijinga
 
Hii Chadema ya Mbowe kama haiwatishi mbona mlimuweka Mbowe ndani miezi sita, na mkawaibia kura wagombea wao kwenye uchafuzi mkuu uliopita?

Sheria za Nchi ndio zilimkuta na Hatia kiasi cha kuwa Jela kwa Muda wote huo!

Hakuonewa ilikuwa ni Haki yake ile
 
Nawasubiri na Moto wangu Wanaujua.
Hizi bangi zako unazovuta asubuhi kabla ya kuweka kitu chochote tumboni, ndiyo mara zote zimekuwa zikikuhamasisha kutukana watu hovyo.

Halafu Mods wakifanya ya kwao, unakuja kwa upooole na kale ka ID kako ka Minosaiklini! Jitahidi kuwajibu watu kwa hoja dogo. Acha kujivunia huo mdomo wako mchafu.
 
Sheria za Nchi ndio zilimkuta na Hatia kiasi cha kuwa Jela kwa Muda wote huo!

Hakuonewa ilikuwa ni Haki yake ile
Kwanini mkamtoa wenyewe kama mlimkuta na hatia? Tena baada ya kumtoa mkampeleka ikulu moja kwa moja, hivyo ndivyo sheria za nchi zinavyotaka!.
 
Jamani msitoke kwenye mstari.

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…