Hivi Diamond anazungumza na sisi au na Harmonize?’

Hivi Diamond anazungumza na sisi au na Harmonize?’

Nyani haoni kundule mbona yy hakukumbuka na alivyofanyiwa na marehemu Ruge Mutahab
Kama ulikua hujui nakujuza chanzo cha Diamond kugombana na Ruge ni kwasababu ya Harmonize..Ruge alitaka kumtumia Harmonize kwa maslahi kidogo Mond akagoma ndo bifu lilianzia hapo
 
Kama ulikua hujui nakujuza chanzo cha Diamond kugombana na Ruge ni kwasababu ya Harmonize..Ruge alitaka kumtumia Harmonize kwa maslahi kidogo Mond akagoma ndo bifu lilianzia hapo
naomba source ya hiyo habari yako mkuu?
 
Yule bwana wa kariakooo vp mbona mna taka kumshusha wanadamu hamna jema..




[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ali sikika kiba100 aki nong'ona back stage
 
Mbona yy alileta jeuri kwa ruge mtu ambaye ana mchango mkubwa katika mafanikio yke
 
Wasafi wanajichanganya sana, walisema Harmonize ameondoka kwa kuaga na uongozi umempa baraka zote huko aendako lkn sasa hivi wanaongea vitu kama vile Konde ameekimbia.
Konde amezingua , amewaacha washkaj na makaratasi akatokomea kusikojulikana , wanachoumiza
kichwa sa hv ni kuwa waende kisheria au niaje, jamaa kakubali gharama Ila kutoa mpunga ndo miyeyusho, na sa hv kila analofanya ni nje ya WCB... Kiufupi katokomea kinyemela indirect
 
Honestly bado siamini kama huyu Dogo ata prosper zaidi ya sasa.. Ni kama ameshafika ukomo wake wa umaarufu.

Diamond halikadhalika.. Na sasa tusubiri wwngine wang'ae.
 
Honestly bado siamini kama huyu Dogo ata prosper zaidi ya sasa.. Ni kama ameshafika ukomo wake wa umaarufu.

Diamond halikadhalika.. Na sasa tusubiri wwngine wang'ae.
Diamond amefikia ukomo wa umaarufu? We jamaa unaota si bure Hadi sasa hiv diamond ni balozi wa makampuni 9 na amekuwa nominees kwenye tuzo nyingi kubwa za mwaka Huu ikiwemo ile ya marekani inaitwa people choice award, ngoma zake zote alizotoa mwaka Huu time hit Sana,kumbuka pia mwezi huu ameweka record ya kujaza ukumbi mkubwa wa ujerumani unaitwa columbius lakini mwaka Huu amepata show 50 za ndani na nje ya nchi,mwezi uliopita tu kafanya show ya Uganda kwa kiingilio kikubwa Cha laki moja kama kiingilio Cha chini na vip ni mil 1 lakini kajaza na wengine wameishia nje kwa kukosa nafasi kwenye huo ukumbi mkubwa wa Uganda mzee baba unata kuniambia hiv ndio kufa ki mziki?we jamaa unamasiala
 
Inawezekana kinachozungumzwa na wengi kuwa Mkurugenzi wa lebo ya WCB, Diamond Platnumz hajapendezwa na kuondoka Harmonize kuondoka kwenye lebo hiyo kuna ukweli.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na minong’ono kuwa wawili hao hawapo karibu na hawana mawasiliano kabisa hasa baada ya Harmonize ambaye Diamond alimkuza kisanii kuomba kujitoa kwenye lebo hiyo, akionekana kama hana shukurani baada ya mambo yote aliyofanyiwa ikiwamo kukuzwa kisanii lakini ameamua kutemana nao.
Kauli hiyo imeonekana ina mashiko kutokana na kile kilichosemwa na Diamond mara baada ya kukabidhiwa ubalozi wa kampuni ya Bomet inayozalisha sabuni ya unga ya Niceone, kuwataka vijana wakumbuke walikotoka.
“Kijana kumbuka sehemu uliyotoka na kumbuka na kuwaheshimu watu waliokuwezesha, mimi nisingeweza kufika hapa bila mameneja wangu na Watanzania ambao ni mashabiki wangu, nitaendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwapenda,”
“Naamini kila kijana ameandikiwa fungu lake kwenye maisha na hakuna mtu anaweza kukushusha au kukuzibia riziki yako cha muhimu ni kufanya kazi na kumuomba sana Mungu,” alisema.

Licha ya kutomtaja mtu, kauli hiyo ilizua minong’ono kuwa inawezekana anamfikishia ujumbe huo Harmonize.
Ikihusishwa na mchuano kati yao unaoendelea mtandaoni ambapo Septemba 22, 2019 zilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha Diamond akiwa Uwanja wa Taifa wakati wa uzinduzi wa tamasha la utamaduni la Afrika Mashariki (Jamafest), akionekana kazungukwa na vijana wengi wakimshangilia na kumwimbia.
Kesho yake Harmonize naye akaweka video inayomuonyesha akiwa kwenye uwanja huo siku ya mechi ya Taifa Stars na Burundi, ambapo naye alizungukwa na kundi la vijana kama ilivyokuwa kwa bosi wake wa zamani.
Mbali na hayo Diamond aliwakumbusha vijana kuwa ili kufikia mafanikio kama yake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii.
“Unaweza kuniangalia ukanichukulia poa, nitolee mfano jana kuanzia asubuhi nilikuwa narekodi video hadi asubuhi ya leo, nimejiegesha saa chache nagongewa mlango niende kwenye miadi ubalozini, nimetoka huko safari ya kuja hapa Kilimanjaro Hoteli ikaanza unaweza kuona ni jinsi gani natumia muda mwingi kufanya kazi,”
“Kwangu muda huu wa ujana ndiyo wa kufanya haya ninayoyafanya, hivyo kijana yeyote anayependa muziki na anatamani kuwa na mafanikio kama mimi akubali kulala uzeeni, kupumzika uzeeni,” alisema Diamond.
Alisema mafanikio hayaangalii kazi, hivyo vijana popote pale walipo bila kujali wanafanya kazi gani, wasikubali kuchoka kabla hawajafanikiwa.



Mwananchi
Ama kweli £"%$^ ya kale hayanuki maana huyu kijana amesahau aliyomfanyia Bob Junior? Watasha wana kamsemo 'What goes around, comes around'
 
Back
Top Bottom