Hivi Gesi asilia inayozalishwa nchini Tanzania inatusaidia Nini?

Joshua Mbezi

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2024
Posts
1,994
Reaction score
4,446
Nchini kwetu tuna vitaru vingi vinavyozalisha gesi asilia kutoka mikoa ya kusini (lindi ,mtwara) na hiyo gesi inafaa kwa matumizi mbalimbali (domestic & economically)

Je kwanini serikali haichukulii ongezeko la bei ya mafuta kama jambo la dharula na ikatafutwa njia ya haraka ya kudhibiti ongezeko la gharama za maisha kupitia gesi

Kwa mfano
Kuwataka watoa huduma za usafiri na usafirishaji kufunga mifumo ya gesi kwenye magari

Kujengwa kwa dharula vituo Cha kujazia gesi kwa mikoa kama ya dar es salaam, dodoma, mwanza Kagera, Kigoma na mtwara

Kufanya hivi kunaweza kuthibiti ongezeko la gharama za maisha

Au
Ndo kufa kufaana mwenye nacho anajiongezea masikini wafe na watoto wao?
 
Muulize JK aliyewasainisha Wabunge sheria ya hiyo gesi usiku wa manane. Mheshimiwa Tundu Lissu, Rais ajaye wa Tanganyika huru, pamoja na baadhi ya wazalendo wenzake walipiga kelele za kutosha tu kuipinga hiyo sheria tata iliyoruhusu Mabeberu kujimilikisha gesi yetu; wakaishia tu kupuuzwa na wabunge wengi wa ccm.
 
Mkuu unauelewa Gani kuhusu gesi asilia?

Kwa Dar es salaam vituo vya gesi asilia ni vyakujitosheleza kwasasa hata msongamano sikuhizi haupo katika vituo, jukumu lililobaki ni watu kubadili mfumo wa Gali (Maamuzi ya mtu binafsi)

Kuhusu Dodoma na mikoa mingine njia Bora ni kupelekwa bomba la gesi Hadi sehemu husika jambo ambalo SI la wiki Moja (hauwezi kuwa mpango wa dharura), njia nyingine ni kupelekwa gesi kwa magari jambo linalo hitaji uagize magari maalumu pamoja na kutengeneza vituo maalumu kwaajili ya regasification (hii haiwezi kuwa mpango wa dharura pia)

Gesi tuliyonayo inatunufaisha vipi?
Kwasasa Tanzania gesi yote inayozalishwa inatumika nchini 100% kwenye uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwanda, kwenye vyombo vya usafiri pamoja na matumizi ya majumbani kwa mikoa ya DSM, Lindi MTWARA

Gesi asilia haiwezi kuwa mpango wa dharura mikoani kwasasa. Isipokuwa inaweza kuwa mpango wa muda mrefu hapo baadae

Nitarudi.
 
Kuvutia watalii mkuu tushone sare za polisi arusha
 
Hapo nakukataa Mkuu
Nchi haiwez kuendeshwa kwa utashi wa mtu mmoja sasa hivi angalia bei za mafuta zilivyopaa namna pekee ya kunusuru hali ni kupitia matumizi ya gesi au umeme
Kwenye suala la kutumia umeme kwenye sector ya usafiri na usafirishaji hasa wa bidhaa na masafa marefu tunaweza kufeli
Lkn tungekuwa na viongozi wenye maono ya namna ya kudhibiti mfumuko wa bei tungeangali kwenye gesi kwa sasa

Na kitu kingine mbona hapo nyuma kulikuwa na Mpango wa kwamba kila anayehtaji kujenga kituo Cha mafuta lazma awe Tyr kujenga na sehemu ya kuhifadhi gesi je huo Mpango uliishia wapi?

Wakat kila siku tunaona vituo vya mafuta vikijengwa lkn sehemu ya kujazia gesi Amna maana yake Nini wahuni washatoa Rushwa na kanuni hyo haifuatwi tena

Wao wanachoangalia ni maslahi yao binafsi tu sio maslahi ya umma
 
CHAWA Mindset
Mkuu unauelewa Gani kuhusu gesi asilia?

Kwa Dar es salaam vituo vya gesi asilia ni vyakujitosheleza kwasasa hata msongamano sikuhizi haupo katika vituo, jukumu lililobaki ni watu kubadili mfumo wa Gali (Maamuzi ya mtu binafsi)

Kuhusu Dodoma na mikoa mingine njia Bora ni kupelekwa bomba la gesi Hadi sehemu husika jambo ambalo SI la wiki Moja (hauwezi kuwa mpango wa dharura), njia nyingine ni kupelekwa gesi kwa magari jambo linalo hitaji uagize magari maalumu pamoja na kutengeneza vituo maalumu kwaajili ya regasification (hii haiwezi kuwa mpango wa dharura pia)

Gesi tuliyonayo inatunufaisha vipi?
Kwasasa Tanzania gesi yote inayozalishwa inatumika nchini 100% kwenye uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwanda, kwenye vyombo vya usafiri pamoja na matumizi ya majumbani kwa mikoa ya DSM, Lindi MTWARA

Gesi asilia haiwezi kuwa mpango wa dharura mikoani kwasasa. Isipokuwa inaweza kuwa mpango wa muda mrefu hapo baadae

Nitarudi.
 
Mkuu unauelewa Gani kuhusu gesi asilia?

Kwa Dar es salaam vituo vya gesi asilia ni vyakujitosheleza kwasasa hata msongamano sikuhizi haupo katika vituo, jukumu lililobaki ni watu kubadili mfumo wa Gali (Maamuzi ya mtu binafsi)

Kuhusu Dodoma na mikoa mingine njia Bora ni kupelekwa bomba la gesi Hadi sehemu husika jambo ambalo SI la wiki Moja (hauwezi kuwa mpango wa dharura), njia nyingine ni kupelekwa gesi kwa magari jambo linalo hitaji uagize magari maalumu pamoja na kutengeneza vituo maalumu kwaajili ya regasification (hii haiwezi kuwa mpango wa dharura pia)

Gesi tuliyonayo inatunufaisha vipi?
Kwasasa Tanzania gesi yote inayozalishwa inatumika nchini 100% kwenye uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwanda, kwenye vyombo vya usafiri pamoja na matumizi ya majumbani kwa mikoa ya DSM, Lindi MTWARA

Gesi asilia haiwezi kuwa mpango wa dharura mikoani kwasasa. Isipokuwa inaweza kuwa mpango wa muda mrefu hapo baadae

Nitarudi.
kwenye matumizi ya majumbani mbona kama kimya mudamrefu sana , au hakuna uungwaji wa watu wapya?
na gharama zipoje kwa walioungwa?
 
Nchini kwetu tuna vitaru vingi vinavyozalisha gesi asilia kutoka mikoa ya kusini (lindi ,mtwara) na hiyo gesi inafaa kwa matumizi mbalimbali (domestic & economically)

Je kwanini serikali haichukulii ongezeko la bei ya mafuta kama jambo la dharula na ikatafutwa njia ya haraka ya kudhibiti ongezeko la gharama za maisha kupitia gesi

Kwa mfano
Kuwataka watoa huduma za usafiri na usafirishaji kufunga mifumo ya gesi kwenye magari

Kujengwa kwa dharula vituo Cha kujazia gesi kwa mikoa kama ya dar es salaam, dodoma, mwanza Kagera, Kigoma na mtwara

Kufanya hivi kunaweza kuthibiti ongezeko la gharama za maisha

Au
Ndo kufa kufaana mwenye nacho anajiongezea masikini wafe na watoto wao?

Siasa za nje ni ngumu sana.
Kabla ya kujiuliza hili, hebu tafakar kuwa

- Uganda ina Grude oil, ila hawajafikiria kujenga refinery ya kugeuza hiyo Grude kuwa Petrol au Diesel, na wakaamua kujenga Bomba had Bandar ya Tanga (kwa gharama kubwa) ili kuuza hiyo Grude nje. Alaf wao waendelea kununua Diesel na Petrol.😭😭😭😭😭

- Nigeria ina Grude oil, Dangote akajitosa kutengeneza Refinery (kwa gharama kubwa). Ili aweze kununua grude kwa serikal , kugeuza kuwa mafuta na kuyauza nchin kwake.
Alaf baada ya kukamilisha kiwanda. Serikal ya nchi yake ikakataa kununua mafuta kutoka kwake 😎😎😎 ikaendelea kuagiza mafuta nje.😂😂😂😂.

Mfereji wa Harmuz inasemwa unapitisha 20% ya mafuta yote ya dunian. Mgogoro wa mwez tu Umepandisha mafuta TZ kwa zaid ya 1k.😭😭😭😭

Imagine kama mafuta yakiadimika kwa 80% .

Afrika haiwez kuwa huru.
Kuna Siasa kubwa sana Nchi zilizoendelea wanatuchezea Afrika.
 
Mkuu unauelewa Gani kuhusu gesi asilia?

Kwa Dar es salaam vituo vya gesi asilia ni vyakujitosheleza kwasasa hata msongamano sikuhizi haupo katika vituo, jukumu lililobaki ni watu kubadili mfumo wa Gali (Maamuzi ya mtu binafsi)

Kuhusu Dodoma na mikoa mingine njia Bora ni kupelekwa bomba la gesi Hadi sehemu husika jambo ambalo SI la wiki Moja (hauwezi kuwa mpango wa dharura), njia nyingine ni kupelekwa gesi kwa magari jambo linalo hitaji uagize magari maalumu pamoja na kutengeneza vituo maalumu kwaajili ya regasification (hii haiwezi kuwa mpango wa dharura pia)

Gesi tuliyonayo inatunufaisha vipi?
Kwasasa Tanzania gesi yote inayozalishwa inatumika nchini 100% kwenye uzalishaji wa umeme, matumizi ya viwanda, kwenye vyombo vya usafiri pamoja na matumizi ya majumbani kwa mikoa ya DSM, Lindi MTWARA

Gesi asilia haiwezi kuwa mpango wa dharura mikoani kwasasa. Isipokuwa inaweza kuwa mpango wa muda mrefu hapo baadae

Nitarudi.
Wala usirudi umeongea uharo mtupu, wee mwenyewe umeona umeongea madini. Chikichia tu mazima.
 
Sasa huu si upum
Siasa za nje ni ngumu sana.
Kabla ya kujiuliza hili, hebu tafakar kuwa

- Uganda ina Grude oil, ila hawajafikiria kujenga refinery ya kugeuza hiyo Grude kuwa Petrol au Diesel, na wakaamua kujenga Bomba had Bandar ya Tanga (kwa gharama kubwa) ili kuuza hiyo Grude nje. Alaf wao waendelea kununua Diesel na Petrol.😭😭😭😭😭

- Nigeria ina Grude oil, Dangote akajitosa kutengeneza Refinery (kwa gharama kubwa). Ili aweze kununua grude kwa serikal , kugeuza kuwa mafuta na kuyauza nchin kwake.
Alaf baada ya kukamilisha kiwanda. Serikal ya nchi yake ikakataa kununua mafuta kutoka kwake 😎😎😎 ikaendelea kuagiza mafuta nje.😂😂😂😂.

Mfereji wa Harmuz inasemwa unapitisha 20% ya mafuta yote ya dunian. Mgogoro wa mwez tu Umepandisha mafuta TZ kwa zaid ya 1k.😭😭😭😭

Imagine kama mafuta yakiadimika kwa 80% .

Afrika haiwez kuwa huru.
Kuna Siasa kubwa sana Nchi zilizoendelea wanatuchezea Afrika.
Sasa huu si upumbavu kabisa muda mwingne napata hamasa ya kuwaunga mkono watu wanaosema kuzaliwa Africa ni laana
 
Tatizo lililopo ni kupenda rushwa na ubinafsi Tu...Hizi mambo za mafuta na gesi zina pesa nyingi mnooo sasa Kwa viongozi wetu hawa lazima itakuwa wanakula parefu halafu kama nchi tunapigwa vibaya Sana...Mfano ishu ya mafuta tungekuwa na maono kitambo basi sasa tungekuwa na refinery plants nyingi Tu...
 
Nchini kwetu tuna vitaru vingi vinavyozalisha gesi asilia kutoka mikoa ya kusini (lindi ,mtwara) na hiyo gesi inafaa kwa matumizi mbalimbali (domestic & economically)

Je kwanini serikali haichukulii ongezeko la bei ya mafuta kama jambo la dharula na ikatafutwa njia ya haraka ya kudhibiti ongezeko la gharama za maisha kupitia gesi

Kwa mfano
Kuwataka watoa huduma za usafiri na usafirishaji kufunga mifumo ya gesi kwenye magari

Kujengwa kwa dharula vituo Cha kujazia gesi kwa mikoa kama ya dar es salaam, dodoma, mwanza Kagera, Kigoma na mtwara

Kufanya hivi kunaweza kuthibiti ongezeko la gharama za maisha

Au
Ndo kufa kufaana mwenye nacho anajiongezea masikini wafe na watoto wao?
Screenshot_20260401-130445~2.png
 
Wala usirudi umeongea uharo mtupu, wee mwenyewe umeona umeongea madini. Chikichia tu mazima.
Nimeongea fact kama unapinga njoo na hoja uniambie mpango wa dharura wa kutumia gesi asilia kwenye kipindi hili unautekelezaje
 
CHAWA Mindset
Nimeongea fact kama mtaalamu tu Sina Cha kufanya kwenye siaza za bongo na Africa, njoo hapa na mindset Yako Bora ya kimaendeleo uniambie mpango wa dharura wa kutumia gesi asilia badala ya mafuta kwa kipindi hiki unautekelezaje

Hiyo miradi si chini ya miaka 2 kuitekeleza, nipinge kwa fact
 
Sijakataa unachokisema , ninachokataa ni kusema gesi asilia iwe mbadala wa kwa Wakati huu, Wanachi wa DSM, Lindi na MTWARA ndio wannaweza kuwa na excess hiyo kwasasa labda kwa baadae hilo unalolisema linaweza kutekelezeka

Ni Zaid ya Miaka 2 kutekeleza hilo.
 
Mkuu Sina uelewa kuhusu masuala ya serikali na mipango na gharama kwa hapa nchini lakini najua kuna baadhi ya viwanda vimeunganishwa na baadhi ya Nyumba zilizopo karibu na viwanda hivyo zimeunganishwa

Kuhusu gharama kwa uzoefu duniani
Gesi asilia Huwa inasafirishwa kwa Pressure kubwa sana karibu 100bar hivyo Ili kufikia matumizi ya Nyumbani inatikiwa pressure hiyo ipunguzwe Hadi kufikia < 1bar, hilo linahitaji vifaa vya gharama zaidi pamoja na mabomba ya kuhimili pressure hiyo ( kwa viwandani gharama wanazimu ukizingati ni Nishati ya bei rahisi kulinganisha na umeme wa tanesco) ( Moja ya sababu ambayo gesi ya MTWARA haiwekwe kwenye mitungi ya kupikia)

Kwa maeneo ambayo miundombinu ya gesi imefika gharama haziwezi kuwa kubwa sana kutokana na miundombinu kuwepo na umbali wa kuvuta bomba ni rahisi zaidi
 
Back
Top Bottom