Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 11,884
- 21,175
Juzi kati nilisoma habari moja kuwa mama mmoja wa kambo huko ughaibuni alimfungia kijana wake wa miaka kumi na moja ndani kwa muda wa miaka 20. Kijana alikutwa akiwa na afya dhoofu kabisa. Mama amekamatwa na kushtakiwa.
Miaka ya 1800 mwishoni huko Ufaransa kulikuwa na msichana aliyeitwa Blanche Monnier. Alipokuwa na miaka 25 alitaka kuolewa. Mama na kaka yake hawakuafiki juu ya mtu aliyetaka kumuoa. Wakamfungia ndani kwa muda wa miaka 50. Polisi ndiyo walikuja kumuokoa. Kaka na mama yake wakashtakiwa, raia wenye hasira nusura wawaue.
Wakati Blanche anaokolewa na polisi alikuwa na afya mbaya huku akili ikiwa imemharibika.
Visa vya watu katili kufungia wengine ndani ni vingi sana. Pia kwenye jamii nyingi kuna kawaida ya kufungia ndani wagonjwa wa akili. Kwa ajili ya usalama wao wenyewe na wa wengine.
Huku kwetu ikitokea amegundulika mtu aliyekuwa amefungiwa ndani huwa tunasema aliwekwa msukule. Kwamba aliyemfungia alikuwa anamtumia kishirikina. Je inawezekana awa tunaita misukule ni watu waliofungiwa ndani na watu wakatili tu au sababu ya kuwa wagonjwa wa akili? Na wanapopatikana wakiwa wagonjwa wa akili tunazidi kujiaminisha kuwa wamechukuliwa akili. Habari ya kuamini misukule ni sababu ya ujinga wetu?