Hivi haiwezekani dunia nzima tukaungana tukaivamia North Korea kupitia UN na kumtoa Kim Jong Un madarakani?

Hivi haiwezekani dunia nzima tukaungana tukaivamia North Korea kupitia UN na kumtoa Kim Jong Un madarakani?

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Kwa hizi akili za Kim Jong Un na namna ambavyo anahangaika kutafuta vita na the Western world ni dhahir kuwa nchi imemshinda na tusipokaa vizuri mjinga huyu atatupeleka kwenye WWIII

Kwanza Kim ndo anaongoza kwa kuwa na hostages wengi zaidi in the world kwani anaongoza watu Milioni 26 ambao hawana uhuru wa kufanya chochote.

Kim ni Psycho. Hivi kwanini UN Security Council isikae chini ikavote kumtoa huyu maniac madarakani?

Ikafanyika coup flani hivi ya kibabe ikiongozwa na Western countries ili North Korea iwe huru?

Au ipitishwe UN resolution tu kuamua kwamba dunia nzima tunaunda jeshi la kumtoa Kim madarakani?

Kama ni nyuklia hata US anazo. Nini kinasababisha tusiweze kumdhibiti huyu kiumbe?

Hizi ni baadhi ya headlines zinaoonesha jinsi Kim anavyotafuta vita ya tatu ya dunia kwa nguvu.

Kim jong.png

Nk1.png

NK.png

Mumvamie mtu ambaye anaongoza taifa lake kwa utashi wake? Are you mad! Lile ni taifa huru mwacheni afanye anachotaka kumvamia ndio kutafta majanga sababu yule kurusha nuclear hajiulizi mara mbili
 
Lugha yetu ya kiswahili inatumika vibaya sana.

Unaona sawa kabisa kuvamia Nchi ya mwenzenu kisa Wana Nchi wake hawana uhuru wewe hapa kwako una uhuru Gani wa kumtambia raia wa Korea Kasi? Utofauti uliopo kati Yako na korea Kasi ni % chache maana wakosoaji wa serikali wote mna uawa kama mbwa tu.

Hata mkiungana china hawezi kumpiga kiduku Russia na Iran Hawa wote ni kitu kimoja.

Tukija Kwa Africa hamna Kila kitu labda uchawa.
 
Sijawahi ona Uzi wa kijinga na kipumbavu kama huu.

Mental health ni tatizo kubwa sana. Ufinyu wa kufikilia na kupambanua mambo ni janga la kitaifa.

Hizo nchi ulizotaja TZ Yako haiwafikii hata kidogo kiteknolojia, kiuchumi na hata kisiasa.

Wewe demokrasia uchwara na uchawa ndio Dili kwako.

Hata huelewi bila Urusi, Uchin na washirika wao, Dunia ingekuaje Leo.
 
Kuzaliwa North Korea ni aheri kuzaliwa ndani ya jela kwa nchi za Magharibi.

Wananchi wa North Korea wamezuiwa kusherehekea hata Christmas eti ni sherehe ya kimagharibu, badala yake wanatakiwa kusherehekea siku aliyozaliwa bibi yake Kim. Jong Un.

North Korea ukipatikana na biblia, au mkakusanyika kusali, adhabu ni jela miaka 15.

Kama umezaliwa Korea kaskazini ni marufuku kutoka nje ya nchi.

North Korea ukipatikana umevaa jeans au nguo yoyote inayotafsiriwa ni ya kimagharibi, adhabu ni jela.

Ukinunua TV lazima uipeleke polisi ikaandikishwe na ikawe tuned kwa station ya North Korea.

North Korea, hakuna anayeruhusiwakutumia internet.

Hayo ni machache, yanayoshangaza.
 
Baraza la usalama la umoja wa mataifa halina mamlaka yoyote ikiwa nchi moja yenye veto itakataa. Kwenye baraza la usalama la umoja wa mataifa Russia, China, Marekani, Uingereza na Ufaransa ndio wanaoweza kupitisha azimio la kuivamia nchi yoyote ile lakini ni hadi azimio hilo likubaliwe na wote, ikitokea nchi moja imekataa azimio hilo linakuwa batili.

North Korea imepakana na Russia na China kujaribu kuisogelea tu Russia na China haziwezi kukubali maana adui yao atakuwa amewakaribia kwahiyo ni hatari hata kwa west wenyewe kwa sababu Russia na China haziwezi kuruhusu hilo.
 
Kuzaliwa North Korea ni aheri kuzaliwa ndani ya jela kwa nchi za Magharibi.

Wananchi wa North Korea wamezuiwa kusherehekea hata Christmas eti ni sherehe ya kimagharibu, badala yake wanatakiwa kusherehekea siku aliyozaliwa bibi yake Kim. Jong Un.

North Korea ukipatikana na biblia, au mkakusanyika kusali, adhabu ni jela miaka 15.

Kama umezaliwa Korea kaskazini ni marufuku kutoka nje ya nchi.

North Korea ukipatikana umevaa jeans au nguo yoyote inayotafsiriwa ni ya kimagharibi, adhabu ni jela.

Ukinunua TV lazima uipeleke polisi ikaandikishwe na ikawe tuned kwa station ya North Korea.

North Korea, hakuna anayeruhusiwakutumia internet.

Hayo ni machache, yanayoshangaza.
Kuzaliwa North Korea ni aheri kuzaliwa ndani ya jela kwa nchi za Magharibi.

Wananchi wa North Korea wamezuiwa kusherehekea hata Christmas eti ni sherehe ya kimagharibu, badala yake wanatakiwa kusherehekea siku aliyozaliwa bibi yake Kim. Jong Un.

North Korea ukipatikana na biblia, au mkakusanyika kusali, adhabu ni jela miaka 15.

Kama umezaliwa Korea kaskazini ni marufuku kutoka nje ya nchi.

North Korea ukipatikana umevaa jeans au nguo yoyote inayotafsiriwa ni ya kimagharibi, adhabu ni jela.

Ukinunua TV lazima uipeleke polisi ikaandikishwe na ikawe tuned kwa station ya North Korea.

North Korea, hakuna anayeruhusiwakutumia internet.

Hayo ni machache, yanayoshangaza.
Andika propaganda nyengine hizi tushazizoea
 
Back
Top Bottom