Hivi haiwezekani kuwa na makampuni ya umeme kwenye nchi yetu?

Hivi haiwezekani kuwa na makampuni ya umeme kwenye nchi yetu?

LA7

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
655
Reaction score
2,369
Habari za humu wana jukwaa natumaini hamjambo.

Nimekuja na mada hii baada ya kulala giza kila wakati, pia kushindwa kufanya kazi zangu za kiuchumi.

Yaani serikali yenyewe iwe inachimbia tu nguzo halafu kuwepo na makampuni ya kupitisha waya za umeme, naamini nguzo moja kuna uwezekano wa kupitisha hata line tatu za umeme.

Yaani iwe kama barabara tu inajenga serikali lakini kila mtu anaweka usafiri wake.

Nimemaliza, ni hivo tu yaani.
 
Hata watu binafsi wanaweza kujitengezea umeme wao tena kwa gharama nafuu wakaachana na longo longo la Main grid.

Ukiwa na makaa ya mawe, au maji,au upepo au oil chafu, au maranda ya mbao au mpunga au taka za plastic au mabaki ya shambani au biogas, tosha kwa umeme saizi ya kiwanda, garage, mgodi wako, nk.
 
Hata watu binafsi wanaweza kujitengezea umeme wao tena kwa gharama nafuu wakaachana na longo longo la Main grid.
Hiyo inaruhusiwa kwa mtu binafsi, ila ni gharama walala hoi wengi hawawezi.

Tatizo ni kwamba ukitengeneza umeme wako ukamuuzia hata jirani tu ni kosa kisheria.
Unafungwa.

Yani ni bora tuendelee kupambana na umeme wa mgao wa shirika lililofeli la Tanesco ili sirikali ipate mapato kuliko kuruhusu mashirika binafsi kuzalisha na kuuza umeme.

ili wananchi wapate unafuu.
Ni ujinga na fikra za kijamaa ndio zinatawala.
 
.

Yaani serikali yenyewe iwe inachimbia tu nguzo halafu kuwepo na makampuni ya kupitisha waya za umeme naamini nguzo moja kuna uwezekano wa kupitisha hata line tatu za umeme.

Yaani iwe kama barabara tu inajenga serikali lakini kila mtu anaweka usafiri wake.
Nimemaliza ni hivo tu yaani

Kwanini uwaze kutumia Nguzo za Serikali/ (Tanesco) ?
Kama unaweza ,tafuta chanzo chako Cha umeme, baada ya upembuzi ya kinifu utapata kibali Cha kuzalisha , na kujenga miundo mbinu ya kusambaza.

Na sio Kila umeme unasafiri kwa manguzo .

Njombe (Rupembe) Kuna company inasambaza kwa cable za chini ya ardhi, pia IPO Kilolo (kidabaga) Mfindi IPO company mesambazia vijiji vya Isipii ,Ibwanzi , kilosa, mlevera , na Bado imeunga kwenye grid ya taifa.

Imevuka imeenda hadi Irogombe kipanga .

Wamefunga mita zakwako na wanauza kwa mfumo wa Luku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanini wasiruhusiwe kuwa na nguzo zao? Au kupitisha waya chini?
Kuwa na nguzo zao itakuwa ni uchafu,minguzo itakuwa mingi sana ,labda hiyo option ya kupitisha chini kwenye tunnel kama wanavyofanya kwenye fibre optic cable ,then mtu akitaka kuunganishwa kuwe na ulazima wa kutumia amar cable kwenda kwa mteja.
 
hapa umepiga kamba, mzalishaji mdogo huweziunga 'gridi ya taifa'
Jaribu kupitia hapo kabla hujanibatiza jina la (muongo)
Screenshot_20221208-144920.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari za humu wana jukwaa natumaini hamjambo.

Nimekuja na mada hii baada ya kulala giza kila wakati, pia kushindwa kufanya kazi zangu za kiuchumi.

Yaani serikali yenyewe iwe inachimbia tu nguzo halafu kuwepo na makampuni ya kupitisha waya za umeme, naamini nguzo moja kuna uwezekano wa kupitisha hata line tatu za umeme.

Yaani iwe kama barabara tu inajenga serikali lakini kila mtu anaweka usafiri wake.

Nimemaliza, ni hivo tu yaani.
Makampuni ya uzalishaji yapo,, ya usambazaji labda in small scale huko vijijini,,,, hatuwezi kuwa na makampuni makubwa ya kusambaza nyaya zake, ni ufala😄
 
Habari za humu wana jukwaa natumaini hamjambo.

Nimekuja na mada hii baada ya kulala giza kila wakati, pia kushindwa kufanya kazi zangu za kiuchumi.

Yaani serikali yenyewe iwe inachimbia tu nguzo halafu kuwepo na makampuni ya kupitisha waya za umeme, naamini nguzo moja kuna uwezekano wa kupitisha hata line tatu za umeme.

Yaani iwe kama barabara tu inajenga serikali lakini kila mtu anaweka usafiri wake.

Nimemaliza, ni hivo tu yaani.
Sera ya chama.chetu hairuhusu nishati hii kufanywa kiholela..TANESCO yatosha.

Umeme.si unawaka mnataka nn tena...

Chagua CCM pekee kwa maendeleo ya taifa lako.
 
Back
Top Bottom