Hivi haka kaugonjwa ni kangu peke yangu au tuko wengi?

Namba 3 pia ukichanganya na tabia nyingine ulizoorodhesha inaonesha una Obsessive–compulsive disorder (OCD).
Hii hali huwa inamfanya mtu kurudia jambo au mambo fulani kwa mara kadhaa na mara nyingi kwa namba maalum labda 3 au 5 au hata 19.
Namba ambazo anakuwa na bond nazo bila sababu au kwa sababu maaalum.

Hali hii inapomtokea mtu humfanya ajihisi kufanya jambo fulani kwa kurudia rudia ili kuprevent kitu fulani kisitokee na asipokifanya hicho kitu hukosa amani na kupata hofu kwamba jambo baya litatokea na mwisho wa siku lazima afanye hiyo ritual.
Mfano kuzima taa na kuwasha mara tatu kabla ya kulala.
Kufunga na kufungua mlango mara tatu au mara namba yoyote zile kutokana na maamuzi ya mtu na mtazamo juu ya namba hiyo.
kupanga vitu kwenye mstari kabla ya kufanya kitu fulani
Kugeuza kichwa mara kadhaa, kuvuta na kubana pumzi mara kadhaa etc.

Na hali hiyo siyo kwenye physical world tu bali hata kwenye akili hii inaitwa mental ritual.
Mfano anaweza akafikiria kitu ambacho anaona ni kibaya ili kujisikia amani atarudia maneno fulani mara kadhaa au namba fulani mara kadhaa ili ajisikie amani tena na asipofanya anakosa amani na kuhisi jambo fulani baya litamtokea yeye au yoyote yule mfano kufa au nyumba kuwaka moto etc.

So obsessions au intrusive thoughts means ni yale mawazo ambayo huyataki yanayokuwa kichwani kwako lakini uko obsessive nayo.
mfano: kesho nitakufa au fulani atakufa
nyumba yangu sio salama
sijazima jiko hivyo gesi inaweza kulipuka na kuchoma nyumba moto.
typically jambo lolote baya ambalo unaogopa litatokea hivyo inasababisha hofu kukosa amani na uoga au anxiety.

Na hiyo anxiety inapelekea kwenda kwenye compulsions yaani mambo ambayo unaamini ukiyafanya basi utapunguza au kuondoa hiyo anxiety na hizo obsessions au intrusive thoughts.
Wameita compulsive sababu inakuwa inakulazimu yaani ni lazima ufanye ili uondoe hofu na uoga ili upate amani.

Njia ya kwanza kujitibu ni kuacha hizo rituals yaani usisurrender kwa hizo compulsions.
Au hiyo kitu ikikua basi utakosa amani kabisa na itaangamiza maisha yako yote sababu utakuwa unapoteza muda mwingi sana.
mfano kuna wengine wanatumia masaa mawili au zaidi kila siku kukunja na kukunjua nguo kabati zima sasa imagine kuna nini cha maana utafanya hapo?

Na usiombee iwe pure OCD sababu hii inapelekea uwe kichaa bila kupenda.
Mara nyingi kuna watu wanajiona wanaover think hii ni OCD lakini ipo ndani ya kichwa chako na utapoteza masaa kufikiria kitu kimoja bila sababu.
I know the pain and the struggle hii kitu siyo ya kuchekea wala kuombea.

Chanzo chake hakijulikani lakini inasemekana mara nyingi inasababisha na kurithi au mazingira mfano unyanyasaji.
Nilivyokuwa mdogo nilikuwa napenda kurudiarudia vitu mara tatu tatu bila kujua kwanini lakini baada ya kukua nikagundua ni nini mostly lazima nitakuwa nimerithi.

Mental disorders.
 
nikiwa na hela natembea taratibu na huwa naongea kiswahili fasaha siweki uhunii.

nikiwa sina hela mfukoni nakuwaga na waswas mda wote.

napenda nikiita mtoto getho afike uleule mda niliompangia akichelewa naweza hata nisichakate.

napenda mademu wanaoongea kama wanabembeleza

bila kuchanganya kvant na konyagi sijisikii kama nimekunywa
 
Hilo tatizo la 7 hakika tumefanana, na hii imepelekea niwe nawachakata na kuwabadirisha kila week.
 
Ahsante sana mkuu kwa somo zuri
 
Namba 6 ..[emoji1787][emoji1787]
Nakuwa najistukia hatari mpaka nahisi wananicheka sijui imekaaje hii [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Na kale katabia, nikiangalia movie nikaipenda sana nita I puse kila wakati ni kama natamani isiishe [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] huwa nafanya hivi zaidi nikiwa mwenyewe nikama nahitaji buckup mtu wa kutazama nae [emoji1787]
 
Hii kitu nilikuwa nayo, ilinitesa sana, sema sikujua inaitwaje,
 
puker [emoji23][emoji23][emoji23]Ndo uyo mimi sasa mkuu nimesoma uku nacheka yaani

No1 hyo me nmeanza kuiacha sasahivi

2-Mara nyingi nikiwa sehemu ya umeme shida uwa sipendi ifike 80% nahisi kama itazima[emoji23]

3-hiyo Sijui ntaacha lini kwani muda mwingine uwa nakuwa nmefika mbali kabisa alafu narudi tena kuhakikisha na naweza nikaenda safari yangu uku wasiwasi ukiwepo kuwa sijafunga mlango

5-[emoji23][emoji23][emoji23]hii toka utotoni me ni mbishi sana kuvaa nguo mpya labda mambo mawili yafanyike niifue kwanza au niivae mida ya usiku ili watu wasinione nayo

6-miwani napenda sana ila kimbembe kuivaa yaani naweza ivaa ila akitokea tu mtu navua chap chap

7-Ilo ndo linatesa sana sana yaani kila manzi ntakaekuwa nae najua ananipenda ila ntamchokonoa maswali kibao mpaka najikuta napoteza imani nae kuwa hanipendi labda[emoji20]

Nb:uwa muda mwingine natunza sana vitu vya zamani ambavyo sina matumizi navyo kabisa mfano nina vitabu vya shulen sekondari ambavyo naombwa sana na ndugu watumie nawapa Lakin nawasisitizia kabisa wakimaliza wanirudishie alafu Sasa utafikiri nina matumizi navyo ila basi tu[emoji16][emoji16]nguo, na vikorokoro vingine sina hata kazi navyo ila kuvitupa ni big NO....
 

Aiseee
 
Early stage of obsessive compulsive disorder (OCD) so angalia uone namna ya Kutibiwa
 

Najiona hapa kabsaa, 😔
 
Huwa sikumbukagi kuzima data sina hayo mazoea kabisa yani
Nimejiepusha na tabia kama kumaliza chakula kwanza ndiyo nile nyama au kulock gari na kujaribu tena kufungua
Huwa nawachora watu kwenye hivyo vipengele na kuwaona wana kaushamba fulani hivi
Siwezi kuvaa miwani kwa namna yoyote naona inanitekenya pua lakini najiona kama kituko mbele ya watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…