Forgotten
JF-Expert Member
- Jul 20, 2018
- 3,518
- 10,839
Aiseee yani umeandika kitu ninachopitia, nilisoma zaidi kupitia NIMH. Mimi nikifunga mlango huwa sina amani kabisa na ni lazima nitarudia kuhakiki na kama ulivyosema mimi huwa nahakiki kwa mara 7 au 10 na hizo namba nina bond nazo.Namba 3 pia ukichanganya na tabia nyingine ulizoorodhesha inaonesha una Obsessive–compulsive disorder (OCD).
Hii hali huwa inamfanya mtu kurudia jambo au mambo fulani kwa mara kadhaa na mara nyingi kwa namba maalum labda 3 au 5 au hata 19.
Namba ambazo anakuwa na bond nazo bila sababu au kwa sababu maaalum.
Hali hii inapomtokea mtu humfanya ajihisi kufanya jambo fulani kwa kurudia rudia ili kuprevent kitu fulani kisitokee na asipokifanya hicho kitu hukosa amani na kupata hofu kwamba jambo baya litatokea na mwisho wa siku lazima afanye hiyo ritual.
Mfano kuzima taa na kuwasha mara tatu kabla ya kulala.
Kufunga na kufungua mlango mara tatu au mara namba yoyote zile kutokana na maamuzi ya mtu na mtazamo juu ya namba hiyo.
kupanga vitu kwenye mstari kabla ya kufanya kitu fulani
Kugeuza kichwa mara kadhaa, kuvuta na kubana pumzi mara kadhaa etc.
Na hali hiyo siyo kwenye physical world tu bali hata kwenye akili hii inaitwa mental ritual.
Mfano anaweza akafikiria kitu ambacho anaona ni kibaya ili kujisikia amani atarudia maneno fulani mara kadhaa au namba fulani mara kadhaa ili ajisikie amani tena na asipofanya anakosa amani na kuhisi jambo fulani baya litamtokea yeye au yoyote yule mfano kufa au nyumba kuwaka moto etc.
So obsessions au intrusive thoughts means ni yale mawazo ambayo huyataki yanayokuwa kichwani kwako lakini uko obsessive nayo.
mfano: kesho nitakufa au fulani atakufa
nyumba yangu sio salama
sijazima jiko hivyo gesi inaweza kulipuka na kuchoma nyumba moto.
typically jambo lolote baya ambalo unaogopa litatokea hivyo inasababisha hofu kukosa amani na uoga au anxiety.
Na hiyo anxiety inapelekea kwenda kwenye compulsions yaani mambo ambayo unaamini ukiyafanya basi utapunguza au kuondoa hiyo anxiety na hizo obsessions au intrusive thoughts.
Wameita compulsive sababu inakuwa inakulazimu yaani ni lazima ufanye ili uondoe hofu na uoga ili upate amani.
Njia ya kwanza kujitibu ni kuacha hizo rituals yaani usisurrender kwa hizo compulsions.
Au hiyo kitu ikikua basi utakosa amani kabisa na itaangamiza maisha yako yote sababu utakuwa unapoteza muda mwingi sana.
mfano kuna wengine wanatumia masaa mawili au zaidi kila siku kukunja na kukunjua nguo kabati zima sasa imagine kuna nini cha maana utafanya hapo?
Na usiombee iwe pure OCD sababu hii inapelekea uwe kichaa bila kupenda.
Mara nyingi kuna watu wanajiona wanaover think hii ni OCD lakini ipo ndani ya kichwa chako na utapoteza masaa kufikiria kitu kimoja bila sababu.
I know the pain and the struggle hii kitu siyo ya kuchekea wala kuombea.
Chanzo chake hakijulikani lakini inasemekana mara nyingi inasababisha na kurithi au mazingira mfano unyanyasaji.
Nilivyokuwa mdogo nilikuwa napenda kurudiarudia vitu mara tatu tatu bila kujua kwanini lakini baada ya kukua nikagundua ni nini mostly lazima nitakuwa nimerithi.
Mental disorders.
Ni kweli kabisa mimi huwa nanawa mikono mara nyingi zaidi na hata watu ninaoishi nao hunishangaa kwa hilo. 'Fear of germs and contamination' hivi ndiyo jinsi NIMH wameandika na ndiyo ukweli ninaoishi.
Kingine huwa napenda kufanya mambo yangu kwa mpangilio kitu ambacho huwa kinachelewesha mipango yangu kwenda haraka, hii ndiyo ipo siku nyingi sana ila kuhakiki vitu mara nyingi pamoja na kunawa sana mikono siyo vya muda mrefu.
Najaribu kupitia makala mbalimbali kuona najinasuaje katika hili ila kuu ni kuanza kuacha kufanya hivi vitu huenda ikajengeka tabia mpya ya kutokuwa na hofu na kuishi maisha ya kawaida.