Hivi haka kaugonjwa ni kangu peke yangu au tuko wengi?

Aiseee yani umeandika kitu ninachopitia, nilisoma zaidi kupitia NIMH. Mimi nikifunga mlango huwa sina amani kabisa na ni lazima nitarudia kuhakiki na kama ulivyosema mimi huwa nahakiki kwa mara 7 au 10 na hizo namba nina bond nazo.

Ni kweli kabisa mimi huwa nanawa mikono mara nyingi zaidi na hata watu ninaoishi nao hunishangaa kwa hilo. 'Fear of germs and contamination' hivi ndiyo jinsi NIMH wameandika na ndiyo ukweli ninaoishi.

Kingine huwa napenda kufanya mambo yangu kwa mpangilio kitu ambacho huwa kinachelewesha mipango yangu kwenda haraka, hii ndiyo ipo siku nyingi sana ila kuhakiki vitu mara nyingi pamoja na kunawa sana mikono siyo vya muda mrefu.

Najaribu kupitia makala mbalimbali kuona najinasuaje katika hili ila kuu ni kuanza kuacha kufanya hivi vitu huenda ikajengeka tabia mpya ya kutokuwa na hofu na kuishi maisha ya kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…