Hivi hakuna jema linalofanywa na Serikali

Hivi hakuna jema linalofanywa na Serikali

Matiko manga

Member
Joined
Jun 18, 2024
Posts
9
Reaction score
15
Hebu tuwe wakweli ndugu zangu watanzania, ni kweli hakuna jema linalofanywa na Serikali yetu? Mbona asilimia kubwa humu tunapenda kulaumu sana.

Sijasema viongozi wetu ni malaika hapana, lakini ni kweli hakuna wanachofanya? Ni kweli wanauza nchi?

Kuongoza nchi sio kama kuongoza familia. Kwenye familia ya mke na watoto wawili tu baba unaweza usieleweke ndio uje ueleweke na raia milioni zaidi ya 60.

Tuendelee kukosoa lakini pale pakupongeza pia tupongeze.niwatakieni jumatano njema.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU UBARIKI UMOJA WETU
 
Hebu tuwe wakweli ndugu zangiu watanzania.ni kweli hakuna JEMA linalofanywa na SERIKALI yetu?mbona asilimia kubwa humu tunapenda kulaumu sana.sijasema viongozi wetu ni malaika hapana,lakini ni kweli hakuna wanachofanya?ni kweli wanauza nchi?kuongoza nchi sio kama kuongoza familia.kwenye familia ya mke na watoto wawili TU baba unaweza usieleweke ndo uje ueleweke na raia milioni zaidi ya 60.tuendelee kukosoa lakini pale pakupongeza pia tupongeze.niwatakieni jumatano njema.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU UBARIKI UMOJA WETU
Kwa kawaida kufanya mema ni wajibu wa serikali wala si lazima kuipongeza ndio kazi yake, lakini yale mabaya si jukumu lake ndio maana tunayasema.

So, kuipongeza serikali kwa kufanya mazuri huo ni uamuzi binafsi maana inatekeleza majukumu yake ila kuikosoa na kuisema inapokosea hiyo ni lazima maana inakuwa imetenda nje ya majukumu yake.

Ni sawa na baba kwenye familia, ukileta chakula kila siku unaweza usipongezwe maana unatimiza jukumu lako, sasa pitisha siku moja watu wanalala njaa ndipo utaelewa.
 
Hebu tuwe wakweli ndugu zangiu Watanzania ni kweli hakuna JEMA linalofanywa na SERIKALI yetu?

Tuendelee kukosoa lakini pale pakupongeza pia tupongeze.niwatakieni jumatano njema.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU UBARIKI UMOJA WETU
Mkuu Matiko manga , naunga mkono hoja, Watanzania ni watu walalamishi sana, ni wepesi wa kulaumu, na wepesi wa kusahau mema.

Pamoja na mazuri yote waliotendewa huko nyuma, leo kumetokea tatizo kidogo, eti wamesahau yote ya nyuma, wanamgomea!.

Kwenye mapungufu tukosoe lakini na kwenye mazuri, tupongeze!. Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.

P
 
Mnasema kama vile ni fadhila wakati ni jukumu na wajibu wa serikali kufanya hivyo. Kuisifu na kutoisifu ni uamuzi. Kusifiwa kwa kutekeleza majukumu yako si lazima ila usipoyatekeleza kukusema ni lazima.
 
Ungeanza wewe kuyasema hayo mema.
Tutawapongeza siku mema yakizidi mabaya.
 
Tutawapongeza siku wakileta mikataba yote bungeni yanayoshukiwa na 10 percent

1. Mikataba ya ununuzi wa ndege
2. SGR
3. JNHP
4. Viwanja vya ndege
5. Barabara
6. Bandari
7.
 
Sijasema viongozi wetu ni malaika hapana, lakini ni kweli hakuna wanachofanya?
Kuongoza nchi sio kama kuongoza familia.
Umejijibu mwenyewe kwenye posti yako!
Si malaika hivyo wanafanya makosa mengi!
Sasa mbona wanaongoza nchi kama familia zao?
 
Ukimpongeza mtoto kwa kupata 30% kati 100% utakuwa unamuharibu.
Wajibu wa serikali ni kuhudumia wananchi wake.
Wajibu wa wananchi ni kulipa kodi halali.
Inahitajika Neema ya Mungu kumpongeza mtu anayekuumiza tena kwa makusudi.
 
Kwa kawaida kufanya mema ni wajibu wa serikali wala si lazima kuipongeza ndio kazi yake, lakini yale mabaya si jukumu lake ndio maana tunayasema.

So, kuipongeza serikali kwa kufanya mazuri huo ni uamuzi binafsi maana inatekeleza majukumu yake ila kuikosoa na kuisema inapokosea hiyo ni lazima maana inakuwa imetenda nje ya majukumu yake.

Ni sawa na baba kwenye familia, ukileta chakula kila siku unaweza usipongezwe maana unatimiza jukumu lako, sasa pitisha siku moja watu wanalala njaa ndipo utaelewa.
Mleta uzi,umesoma hii komenti?Haya sasa kabugie kichuri.
 
Mkuu Matiko manga , naunga mkono hoja, Watanzania ni watu walalamishi sana, ni wepesi wa kulaumu, na wepesi wa kusahau mema.

Pamoja na mazuri yote waliotendewa huko nyuma, leo kumetokea tatizo kidogo, eti wamesahau yote ya nyuma, wanamgomea!.

Kwenye mapungufu tukosoe lakini na kwenye mazuri, tupongeze!. Tujifunze kuwa na Shukrani kwa Madogo ili Tupatiwe Makubwa!. Japo Tulitaka Kikubwa, Tumepewa Kiduchu!, Tukipokee Tushukuru, au Tususe Kudai Kikubwa?.

P
Kwani kupongezwa ni lazima.
Pongezi hazilazimishwi.
 
Kwani machawa wamezidi kufa?
Kwa mambo yalivyo hovyo, akina Lucas ndio wanaweza kukesha wakisifia.
Je wewe unaishi inje ya a chi ndg?
 
Kujenga jela na mahakama ili watu wapuuzi kama wewe mkapumzike, alisikika mnoko mmoja akisema
 
Back
Top Bottom