hapo hamna kesi mzee. isipokuwa kama ikitokea pale kitaa ndugu wa marehemu au marafiki wakawa wanakumind kutaka kulipiza kisasi kwa kukumaliza na wewe, polisi wanaweza kukuchukua wakakuweke mahali pa usalama tu kule lock up, wakijifanya unasaidia upelelezi au pengine hata kukufungulia shitaka la kuua, wakiona hali imetulia tu wanapeleka jalada kwa mwanasheria mkuu wa serikali haraka na kuondoa kesi kwa nolle.
binti amejiua yeye, wewe una kosa gani? hata kama ulikuwa na mahusiano naye, na mko 18 years, kwani mapenzi si hiari? sio lazima, unaweza kumpenda mtu ikafika kipindi unaamua kumuacha labda umependa mwingine, ni hiari ya mtu kama uyo binti atajiua amejiua yeye wewe huna malice aforethouth yeyote kichwani wakati ule unamuacha kwamba laba "namuacha ili afe" etc, kitendo chako hakijaungana na nia yako hadi kutengeneza kosa hivyo hapo hauna kosa na polisi hawatakukamata kabisa, na ikiwezekana nenda kajisalimishe utoe maelezo hayo ili kesi ife mapemaaa (kama kweli wanakutafuta).