Hivi hatuwezi kufanya kama Nigeria, Rais kuweza kujiteua nafasi ya Uwaziri?

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
2,789
Reaction score
4,951
Rais Buhari alipoingia madarakani alifanya baadhi ya maboresho kwenye uongozi na moja ya mabadiliko aliyofanya ni kujiteua kama waziri wa nishati wa Taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika. Lengo kubwa ni kuhakikisha usimamizi unakuwa mkubwa katika sekta hiyo kubwa kwenye uchumi wa Nigeria.

Nawaza kwa sauti baada ya kutafakari, kuwaza na kuwazua nimeona ni Jambo zuri kufanywa hata hapa nyumbani lakini kwa Tanzania badala ya Rais kujiteua basi amteue Makamu wa Rais kwenye Uwazir na chini yake ateuliwe Naibu waziri ambaye atakuwa mtendaji.

Kwanini Makamu wa Rais? Nafasi ya Umakamu wa Rais inasemwa sana Kama ni 'Ceremonial' hivyo itafaa akiteuliwa Waziri wa Wizara nyeti yenye kuhusisha mipango na mikakati ya muda mrefu.

Nimemuangalia Dkt. Mpango katika mpango huu, angetusaidia sana kwenye wizara ya Fedha na Mipango.
 
Ukweli hatuna waziri wa fedha bali tuna mtu kopakopa nje tu. Kila akikopa mabasi ya familia yake yanaongezeka.
 
mkuu makamu wa raisi ni waziri wa muungano na mazingira kama ulikua hujui.......

pia raisi ni waziri wa wizara kadhaa, kwa sasa kuna tamisemi, utumishi, (na zingine zinazoitwa wizara ya nchi ofisi ya Raisi),

PM pia ni waziri wa wizara zilizo chini yake

sema katika kupunguza matumizi wangeweza kuteua mawaziri tu kwenye hizo wizara bila manaibu,.....…..
 
Rais Buhari alipoingia madarakani alifanya baadhi ya maboresho kwenye uongozi na moja ya mabadiliko aliyofanya ni kujiteua kama waziri wa nishati wa Taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika. Lengo kubwa ni kuhakikisha usimamizi unakuwa mkubwa katika sekta hiyo kubwa kwenye uchumi wa Nigeria.

Nawaza kwa sauti baada ya kutafakari, kuwaza na kuwazua nimeona ni Jambo zuri kufanywa hata hapa nyumbani lakini kwa Tanzania badala ya Rais kujiteua basi amteue Makamu wa Rais kwenye Uwazir na chini yake ateuliwe Naibu waziri ambaye atakuwa mtendaji.

Kwanini Makamu wa Rais? Nafasi ya Umakamu wa Rais inasemwa sana Kama ni 'Ceremonial' hivyo itafaa akiteuliwa Waziri wa Wizara nyeti yenye kuhusisha mipango na mikakati ya muda mrefu.

Nimemuangalia Dkt. Mpango katika mpango huu, angetusaidia sana kwenye wizara ya Fedha na Mipango.
Si alikwahi kuwa waziri wa Fedha na Mipango au wewe ulikuwa mwezini?
 
Kwamba kwenye nafasi ya urais anashindwa kufanya vizuri, ila akiwa na madaraka ya uwaziri ndio atakuwa na meno zaidi? Hii formula imekataa.
 
Ni nzur sna hyo hata Zimbabwe nao wananmfumo huo nadhani makamu rais naweza pia kuwa waziri wa afya au wizara yoyote kuliko kukah ofcn tu na kula kiyoyosi
 
Wito: jambo hili lisiishie Kwa Naibu Waziri mkuu tu Kwa kuteuliwa kuwa waziri wa nishati bali liende mbele zangu hata Kwa Makamu wa Rais na viongozi wengine waandamizi.

Kwa zile nafasi nyeti kwenye Taifa, nikimaanisha wizara ya ulinzi, wizara ya fedha, wizara ya nishati na wizara wizara ya mambo ya nje zingekuwa chini ya Rais, Makamu wa Rais, Waziri mkuu na Naibu Waziri mkuu. Na ziitwe the THE BIG FOUR
 
Rais Buhari alipoingia madarakani alifanya baadhi ya maboresho kwenye uongozi na moja ya mabadiliko aliyofanya ni kujiteua kama waziri wa nishati wa Taifa hilo lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika. Lengo kubwa ni kuhakikisha usimamizi unakuwa mkubwa katika sekta hiyo kubwa kwenye uchumi wa Nigeria.

Nawaza kwa sauti baada ya kutafakari, kuwaza na kuwazua nimeona ni Jambo zuri kufanywa hata hapa nyumbani lakini kwa Tanzania badala ya Rais kujiteua basi amteue Makamu wa Rais kwenye Uwazir na chini yake ateuliwe Naibu waziri ambaye atakuwa mtendaji.

Kwanini Makamu wa Rais? Nafasi ya Umakamu wa Rais inasemwa sana Kama ni 'Ceremonial' hivyo itafaa akiteuliwa Waziri wa Wizara nyeti yenye kuhusisha mipango na mikakati ya muda mrefu.

Nimemuangalia Dkt. Mpango katika mpango huu, angetusaidia sana kwenye wizara ya Fedha na Mipango.
Huku ukisikia waziri wa nchi ofisi ya ........ Maana yake mwenye ofisi ndo waziri mf rais ni waziri wa Tamisemi, makamu wa rais ni waziri wa muingano waziri mkuu ni waziri wa bunge maana wizara husika inakuwa moja kwa moja chini ya rais au pm
 
Wizara ya ulinzi, fedha, nishati na mambo ya nje ziko chini ya ofisi ya Rais ,Makamu wa Rais au waziri mkuu?
 
Hizo haziko moja kwa moja chini ya ofisi mojawapo kati ya hizo ulizozitaja.Zilizo moja kwa moja kwenye ofisi husika ni tamisemi na utumishi kwa rais, muungano na mazingira kwa makamu, bunge nadhani na uwekezaji kwa waziri mkuu. Sasa sijui tutaongeza na waziri wa nchi ofisi ya naibu waziri mkuu au tutafanyaje sijui😂😂
 
Back
Top Bottom