Sina uhakika kamili ila najibu kama ambavyo nimekuwa nikiambiwa na watu wamewahi kupekeka filamu.
DSTV - Hawa nasikia ndiyo wanaolipa zaidi kulivyo ving'amuzi vingine. Niliambiwa ni kati ya 1M to 2M kwa movie ila ubora ni kitu kinachozingatiwa sana kwao. Huwa wanachukua movie na kuipitia kisha wanakupa majibu kama itaonyeshwa au lah.Muda wa filamu kukaguliwa huweza kufika hata miezi miwili.
Azam - Nasikia wanalipa kati ya 500k to 700k, lakini pia ukitaka mkataba wa kulipwa kulingana na inavyoonyeshwa basi utalipwa 200k kwa kila itakapooneshwa.
Startimes - Sina hata tetesi kuwa wanalipa sh. Ngapi, kitu pekee ninachokifahamu ni kuwa wao startimes wanazipa kipaumbeleo filamu zilizochezwa kuonyesha mazingira ya asili.
ZUKU - Sina taarifa zozote.
Hizi ni taarifa za kusikia, nakushauri uzidi kukusanya taarifa ili kupata majibu sahihi zaidi.