Hivi hawa FINE MODERN HOMES ni kweli au ni Utapeli? (Uzoefu na Uhalisia wa Off-Plan Yao

Hivi hawa FINE MODERN HOMES ni kweli au ni Utapeli? (Uzoefu na Uhalisia wa Off-Plan Yao

C.T.U

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2011
Posts
5,080
Reaction score
3,771
Habari za muda huu wakuu,

Naomba kuwasilisha mada hii kwenu ili kupata uzoefu au taarifa za kina kama kuna mtu yeyote humu ndani alishawahi kufanya kazi na kampuni inayoitwa Fine Modern Homes.

Wana mpango wao wanaoutangaza sana unaosema unalipia 40% ya gharama ya nyumba, kisha wanakujengea, na hiyo 60% iliyobaki unaimalizia kuisimamia kidogo kidogo ndani ya miaka 5.

Kwa muonekano wa nje hii ofa inaonekana ni nzuri na ya kuokoa wengi, lakini kuna vitu viwili vikubwa ambavyo vinanipa wasiwasi na kunifanya nizione kama Red Flags:

  1. Picha na Video za Miradi Yao: Mara nyingi kwenye kurasa zao wanapost nyumba ambazo ukiangalia vizuri muundo na mazingira ni kutoka nchi za Magharibi mwa Afrika kama Ghana, Nigeria n.k., badala ya kuonyesha miradi yao halisi waliyojenga hapa nchini na wateja wao wa zamani.
  2. Kufunga Comment Kwenye Instagram: Biashara inayotoa huduma kubwa kama hii ya ujenzi na mikopo inatarajiwa kuacha sehemu ya maoni wazi ili wateja kutoa reviews (ziwe nzuri ama mbaya). Kufunga comments kunazua maswali mengi kama kuna kitu wanaficha au wanakimbia malalamiko ya watu waliotapeliwa au kuahidiwa vitu visivyotekelezeka.
Kwa yeyote mwenye uzoefu au taarifa za uhakika, naomba anisaidie kwenye maswali haya:

  • Uhalali (Legitimacy): Je, ni kampuni iliyosajiliwa rasmi na kufanya kazi kisheria hapa nchini, na wana ofisi zinazoeleweka?
  • Ubora wa Kazi: Kuna mtu yeyote alishawahi kujengewa nao nyumba ikakamilika chini ya utaratibu huu au mwingine wowote?
  • Masharti na Mikataba: Hiyo program yao ya miaka 5 imekaaje kisheria? Je, kuna gharama zilizojificha (hidden costs), riba kubwa, au masharti magumu ya umiliki wa kiwanja/nyumba wakati wa ujenzi?
Lengo la uzi huu ni kujiridhisha kabla ya kuingia kwenye mkataba au kutoa fedha zozote, na pia kuwasaidia wengine wanaoweza kuwa kwenye mpango wa kufanya nao kazi.

Nawasilisha.
 
Kuhusu uhalali (legitimacy) matapeli wameendelea sana siku hizi, kumbuka deci? Kalynda? Mr kuku? Sijui mradi wa vanilla, no miradi ilisajiliwa kabisa kama kalynda ilikua inatangazwa na itv Kila siku ila walitukunyuga vizuri tu!

We mtu kama Lowasa alikua kwenye skendo kubwa kabisa escrow na kina tibaijuka Kisha somehow akaja kua mgombea rais na watu wakamsapoti kweli kweli we huogopi? hiyo ndo bongoland.
 
Sahihi ndio maana nataka kuona kama kuna watu wowote wamefanya kazi na kampuni hii watupe veiw zao pia kwa upande wao
 
Back
Top Bottom