Hivi hawa makocha wa ligi yetu ya NBC mnawaelewa kweli. Kwanini wanaendekeza njaa zao na kudhalilisha taaluma zao za ukocha?

Hivi hawa makocha wa ligi yetu ya NBC mnawaelewa kweli. Kwanini wanaendekeza njaa zao na kudhalilisha taaluma zao za ukocha?

Morning Glory1

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2019
Posts
237
Reaction score
381
Wewe ni kocha umesomea taaluma yako ya ukocha na ukapewa leseni ya ukocha unawezaje kupangiwa kikosi na kiongozi wa timu ambae hana uelewa wowote na taaluma ya coaching?!...

Ifikie hatua haya malalamiko ya makocha kupangiwa timu na viongozi yafike mwisho

Wewe ni kocha ukiona kiongozi anakupangia kikosi ni bora ujiuzulu muachie yeye timu afundishe halafu njoo kwa wadau wa soka tuambie nimejiuzulu ukocha wa timu A au B kwasababu kiongozi wa timu alitaka kunipangia kikosi na mimi kwa kuheshimu taaluma yangu ya ukocha nimekataa hapo ndipo wadau wa mpira tutakuelewa.

lakini sio unakubali kupangiwa kikosi kama popoma na unakubali kusimama kabisa kwenye touchline na unatoa maeleko kwa dk90 halafu timu yako inapokula bao tano ndio unatoka mbele za wadau wa soka na malalamiko kua timu yangu imepoteza mechi kwasababu nimepangiwa kikosi na kiongozi flani...wewe unakua ni kocha mburura wa mwisho na wala haukustahili kua kocha...wewe ni sawa na kilaza na hata hiyo leseni ya ukocha ulipaswa unyanganywe

Kuendekeza njaa nje ya taaluma yako kwa kuogopa kufutwa kazi ni udhaifu mkubwa sana..makocha wa nbc badirikeni tumechoka na hizi drama next time tutawapiga mawe
Note:

Kuna tetesi zinaenezwa na mbumbumbu wasiojua mpira kua kocha wa singida David Ouma na kocha wa Mashujaa Mohamed Abdallah "Baress"(Alievunjiwa mkataba) walipangiwa vikosi vyao dhidi ya "mabingwa wa nchi" yanga na ndomana walipokea kipigo cha mbwa koko kwahy kuna dalili za upangaji wa matokeo.
 
Watajijua wenyewe...hawaoni mwenzao Patrike alikataa kupangiwa akafurushwa na wao wamekubali kupangiwa wakafurushwa...yani ndani ntinti nje ntiti...
 
Azam kapangiwa kikosi ndio maana akafungwa na pamba
Simba kocha kazuiwa kufanya sub na uongozi ndio maana Azam akasawazisha!!!
 
Ngao ya jamii na ligi round ya kwanza ambapo zote mlishenyentwa na Yanga Fadlu alipangiwa kikosi?
 
Tarehe 8 mbona siyo mbali. Tunasubiri watakuja na kisingizio gani baada ya dakika 90 za mchezo.
 
Back
Top Bottom