Hivi hawa marefari kwenye NBC league Huwa wanatolewa wapi?

Hivi hawa marefari kwenye NBC league Huwa wanatolewa wapi?

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
4,035
Reaction score
11,462
Ni mambo ya ajabu kweli. Hawa waamuzi ni wa kiwango Cha chini sana, tena hawana ushawishi kabisa. Carrier ya waamuzi Kwa hapa nchini ni kizungumkuti.

.............
Mwamuzi wa mechi ya leo kati ya Simba SC na Yanga ameboronga sana kimaamuzi. Katoa kadi bila kushirikisha kichwa halafu sehemu za kutoa maamuzi ya kadi akafumba macho. Huyu ndiye tuliambiwa ni mwamuzi mwenye ueledi. Khaaaa! Tanzania inaweza kuwa nchi ya ajabu sana, endapo wapuuzi Kama hawa wataendelea kuangaliwa tu wakiharibu mchezo wa soka hapa nchini
 
Marefa wa Tanzania ni kichefuchefu. Yaani mchezaji akiguswa kidogo tu akaanguka chini, refa anapiga filimbi ya faulo! Utachezaje mpira bila kuguswa na mchezaji mwenzako? Labda kama mtu unakimbia riadha. Ndio maana wachezaji wetu hawawezi kucheza ligi Ulaya kwa kuwa hawajazoea matumizi ya nguvu kwenye mpira.

Mkuu The lost nakuunga mkono hawa marefa wetu ni vituko vya karne! Hakuna namna mpira wetu unaweza kukuwa kwa kuendelea kuwakumbatia marefa wa ovyo kama hawa tulio nao hapa Tanzania. Natamani ligi ya NBC iwe inaazima marefa kutoka Ulaya au mataifa mengine ya Afrika yaliyokomaa kisoka. Marefa wetu wanaudhi sana.
 
Kama ubinadamu Ungekuwa excuse basi magereza yasingekuwepo.. Refa ni binadamu ndiyo but anapaswa kutimiza majukumu yake Kwa ueledi na akizingua Sheria imuonye.
kwani refa ww unaona kazingua nn leo
 
Chief! Refarii kashindwa kabisa kuumudu mchezo. Kwa mfano Ile rough ya Faisal kumvuta mchezaji akiwa kwenye movement plan ilitakiwa ale umeme.
Umeanza vizuri lakini bila kuisema foul ya Chama dhidi ya Aucho ambayo ni advantage ya kutokuwa na VAR nakuona kama umeingia na upande kwenye ligi. Ni sahihi Feisal alitakiwa kutolewa Kwa Kadi ya pili ya njano lakini kabla ya hapo Hakuna neno lingine linaloweza kuwa mbadala wa Red card Kwa kitendo alichofanya Chama Kwa Aucho wakati amelala chini.
 
Hamtamuelewa refa ila, kaokoa sana wachezaji wengi(wasivunjane miguu), zile kadi ziliwapelekea wachezaji wa pande zote mbili kucheza kwa umakini wasile umeme. Na refa alifanya sahihi kutokutoa umeme kwa pande zote mbili. Leo hakukuwa na upendeleo wala mpira wa fujo.
 
Ndo maana yanga kimataifa ngumu kutoboa.

Mbeleko zinawaponza wanajipa kichwa

Leo wamecheza hovyo kweli. Simba hawakuwa na utulivu huko mbele otherwise tungeongea mengine
Kutokuwa na utulivu tu tayari inaashiria ni ubovu, kwann ukose utulivu kwenye mechi?
 
Umeanza vizuri lakini bila kuisema foul ya Chama dhidi ya Aucho ambayo ni advantage ya kutokuwa na VAR nakuona kama umeingia na upande kwenye ligi. Ni sahihi Feisal alitakiwa kutolewa Kwa Kadi ya pili ya njano lakini kabla ya hapo Hakuna neno lingine linaloweza kuwa mbadala wa Red card Kwa kitendo alichofanya Chama Kwa Aucho wakati amelala chini.
.
 
Back
Top Bottom