Hivi hawa mbwa aina ya Pitbull ni mbwa halisi?

Hivi hawa mbwa aina ya Pitbull ni mbwa halisi?

mimiamadiwenani

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
5,718
Reaction score
7,784
Ijumaa Kareem!

Matukio ya mauaji ya wamiliki na watoto kutoka kwa mbwa hawa yamekuwa mengi sana. Malalamiko nayo yamekuwa mengi sana kila kona ya dunia hii.

Swali langu ni je, vinasaba vya mbwa hawa ni vya asili kabisa na havijafanyiwa 'cross breeding'?

Kwa sababu kimuonekano wanatisha isivyo kawaida, hasa sura, na miili yao haina manyoya kama ya mbwa tulioawazoea!

Pia vifua vyao ni vipana sana na wanatembea kwa kujitanua mno(kibabe) hali inatozidi kunipa mashaka sana.

Nakumbuka tuliwahi kuwa na mbwa wa aina hii zaidi ya mara mbili nikiwa mdogo kiasi, ila sikujua kama ni pitbull.

Mpaka nilivyoona picha zao na kuoanisha na mbwa tuliowahi kufuga ndipo nimepata picha kuwa wale mbwa tuliokuwa tukifuga ndiyo PitBull wenyewe(niliogopa).

FB_IMG_16754127045286207.jpg
View attachment 2504646
 
View attachment 2504647View attachment 2504646
Hawa walitengenezwa Mahabara kwa lengo la Kupiganishwa kwenye Kamari. Sio God made Breed!
Huko South Africa ni Vilio kila kukicha

Attachments

  • IMG_8323.MOV
    2.5 MB
  • IMG_8322.MOV
    1.6 MB
  • IMG_8320.MOV
    2 MB
Yani kwa hizo crossbreeding zote, rottweiler na hao pitbull ndio vichaa. Hawafai kabisa kufugwa, kwanza wanamtindo wa kupoteza kumbukumbu.

Kuna clip niliona hao pitbull wamemshambulia mbwa wa aina nyingine na kumla
Kwamba hao pitbulls hata mbwa wenzao wao wanawaona mbwa tu[emoji38][emoji38]
 
Pitbull Terrier na Japanese Tosa ni marufuku kuwa nao [emoji636]
Hawa mbwa ni hatari sana na waanweza kushambulia mda wowote

Nakumbuka zamani walikuwa wanaachiwa na wenyewe kwenye parks ila wanashambulia halafu cha ajabu kama ni mwanaume anakurukia kwenye kende

Nawaogopa kama koboko
Waliuwawa wengi sana Uingereza ingawa ndio chimbuko lao na wakapelekwa USA
Wametengenezwa kwa ajili ya kupigana tu
 
Maumbwa ya maabara hayo wameyatengeneza kwa kuunda vinasaba. Hakunaga mbwa wa asili kama huyu.

Halafu sio salama kuyafuga maana wanamatukio ya kushambulia sana watu. Ukitaka kuyatumia haya maumbwa labda katika kuwinda wanyama hatari kama nyoka, au wanyama pori hatari kama simba chui au tiger wakiingia katika makazi ya watu. Ila sio kwaajiri ya kukaa nao nyumbani.
 
Yani kwa hizo crossbreeding zote, rottweiler na hao pitbull ndio vichaa. Hawafai kabisa kufugwa, kwanza wanamtindo wa kupoteza kumbukumbu.

Kuna clip niliona hao pitbull wamemshambulia mbwa wa aina nyingine na kumla
Ah ah eti wanapoteza kumbukumbu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Ah ah eti wanapoteza kumbukumbu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Hii ni kweli kabisa. Hawa mbwa wanatabia ya kusahau m'miliki na wanaweza kukushambulia maana memory zao huwa zinashake wanapandwa na mashetani wanaanza kushambulia hata watu wasiohusika.
 
Back
Top Bottom