Hivi hawa viongozi wa Marekani wanatumia mbinu gani kumwaga madini kwa muda mrefu hivi?

NIMEONA

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2019
Posts
3,862
Reaction score
5,693
Namwangalia huyu Gavana Cuomo wa New York kupitia Fox News akimwaga maneno yalipangilika vizuri kuhusu corona kwa muda mrefu sasa, zaidi ya saa moja na zaidi. Ukimwangalia haonekani akisoma popote pale (labda kama sielewi). hakuna blah blah blah, ni madini tupu.

Nawakumbuka kina Obama na viongozi wengine wengi wa Marekani wako hivyo. nikilinganisha na huku kwetu naona kama kuna utofauti mkubwa sana. wajuzi, hawa jamaa wanawezaje? Ni uwezo tu wa akili zao au kuna namna wanafanya?
 
Wanapoongelea jambo wanakuwa wana data zote na wanafuatilia kila kitu kwa ukaribu zaidi
Wanasoma na kuwasiliana na wahusiki wa jambo lililopo kwa ukaribu
Wanajua mambo kama wewe unavyojua mambo yako ya nyumbani kwako
Huo ni mfano tu

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Kwa viongozi wote wa dunia waliopita hakuna mtu namshangaa kama George Marshall, Secretary of State wa Marekani kipindi na baada ya vita ya pili ya dunia. Sijui aliwezaje kushawishi serikali nzima itoe misaada kwa Ulaya baada ya vita ( Marshall Plan). Yule mtu alikuwa na uwezo mkubwa mno wa kuwasilisha jambo.
 
inaonekana kuna vichwa sana kule......mzee xi jinping huwa namuona na makaratasi yake akisema kitu
 
Kwa viongozi wote wa dunia waliopita hakuna mtu namshangaa kama George Marshall, Secretary of State wa Marekani kipindi na baada ya vita ya pili ya dunia. Sijui aliwezaje kushawishi serikali nzima itoe misaada kwa Ulaya baada ya vita ( Marshall Plan). Yule mtu alikuwa na uwezo mkubwa mno wa kuwasilisha jambo.
Subiri uone baada ya corona kupita kutakuwa na Makonda Plan.
Plan ya kuwasaidia watanzania kupambana na madhara ya corona virus
 
Back
Top Bottom