screpa
JF-Expert Member
- Sep 10, 2015
- 10,857
- 15,866
Kiukweli kabisa mimi nimekuja mjini mwaka jana tu, yaani sikuzote nilikuwa nakaa kwetu Tandahimba ndanindani, Redio niliyokuwa nasikiliza ni RTD sasahivi inaitwa TBC Taifa. Na hata kiswahili nimejifunza baada ya kuja mjini. Nilivyokuja mjini ndio nikaanza kuwajua na wasanii sahivi nimekuwa mjanja hadi najiogopa. Swali langu ni je hawa wadada wamezaliwa Tanzania au wamekuja huku ukubwani kwa bahati mbaya? Maana tabia na swaga zao naona kabisa hawastahili kukaa kwenye hii nchi ya waswahili akina Msagasumu na ManFongo, sio type yao kabisa. Hawa walifaa sahivi wawe mitaa ya NewYork City wanakula maisha na wakina Mayweather na Justin Bieber. Ukipiga nao stori huwezi fikiri kama hata msalani wanaenda, yaani kumbe kukaa Tandahimba nilikuwa napitwa na mengi.