Hivi hawa waimba Singeli huko nyuma walikuwa wanaimba nini?

Hivi hawa waimba Singeli huko nyuma walikuwa wanaimba nini?

Kwani waimbaji wa bongo fleva huko nyuma walikuwa wanaimba nini?
 
Mshenzi ni tusi zito sana lakini kwavile User ID yako inaakisi huku kwetu, nitaacha yapite!! Huaga hatufanyiani hinda wenyewe kwa wenyewe. Ukisikia masela wananong'onezana "...ng'ombe hilo, ng'ombe hilo..!" Jua washajua kwamba huyu ni baki tu na kwahiyo ni halali; lakini sio wenyewe kwa wenyewe kwa sababu wanajua ukimfanyia mwana mtiti wake si mdogo!!!

Hinda= inda...umeanza kuishi lini uswahilini wewe??..hiyo lugha tuachie wenyewe waswahili we ungeendelea na lugha yako ya asili iliyokukuza...sawa Ndugu Masanja?
 
Kwani hawa wanaoimba bongo fleva nao walikuwa wanaimba nini huko nyuma enzi za masantula?
 
Hinda= inda...umeanza kuishi lini uswahilini wewe??..hiyo lugha tuachie wenyewe waswahili we ungeendelea na lugha yako ya asili iliyokukuza...sawa Ndugu Masanja?
WHY Masanja na isiwe Masawe, Mwakalindile, Rugemalila n.k?! Btw, niwaachie wenyewe "Waswahili" au "wa Uswahilini?" Nikukumbushe tu kwamba sio kila Mswahili anaishi Uswahilini na sio kila anayeishi Uswahilini ni Mswahili!!!!
 
Hahahahaaa mshenz sio tus moja kwa moja n mtu alikua sio mstaarabu kwa hiyo washenz ni kinyume cha kitokua starabu
Ni kweli kuna watu hawana stara wala aibu waache wajiite washenz ndio walivyo
Marhaba!! Sio tusi moja kwa moja lakini unafahamu mtu asiye mstaarabu ni mtu wa aina gani!! Kwetu, Mshenzi ni mtu asiye na staha, kuanzia ya lugha hadi matendo! Ni hayawani, fedhuli, mtu wa hovyo hovyo na maruhuni!! Huyu tunaishi nae tu... si wetu; sasa tumpeleke wapi!!!

Ni kweli tunaishi Ushenzini na tunayafurahia maisha ya Ushenzini kwa sababu hatuna uzoefu nayo wala kuyafahamu hayo ya Uzunguni!!! Lakini ukinasibisha ushenzi na mtu mmoja mmoja inakuwa mushkeli!! Ni kama Las Vegas wanavyoita Sin City lakini huwezi kumchomoa mtu mmoja ukasema "ewe ni mdhambi mkubwa!"
 
Hahahaaa mkuu nakuona wewe n mjuz Wa lugha nimefurah ila hata mjinga ni tusi kubwa endapo mjinga ataitwa mjinga na mwenye elim au mwenye slim akimuita mwenye elim mwenzake mjinga lakini kama mjinga akimuita mjinga mjinga hakuna tatizo au mshenz akimuita mshenz mwenzie mshenzi si tusi ni sifa
 
WHY Masanja na isiwe Masawe, Mwakalindile, Rugemalila n.k?! Btw, niwaachie wenyewe "Waswahili" au "wa Uswahilini?" Nikukumbushe tu kwamba sio kila Mswahili anaishi Uswahilini na sio kila anayeishi Uswahilini ni Mswahili!!!!

Hinda= inda...umeanza kuishi lini uswahilini wewe??..hiyo lugha tuachie wenyewe waswahili we ungeendelea na lugha yako ya asili iliyokukuza...sawa Ndugu Masanja?
Nikiangalia majina na majibizano yenu naona wote kama wa-ukae, kwa nini mgombane?
 
Nikiangalia majina na majibizano yenu naona wote kama wa-ukae, kwa nini mgombane?
Sidhani kama kuna ugomvi....
Huyu mjuaji juaji sana hawezi kuwa wa ukae.wa ukae hatupo hivyo..
Maajabu haya... hivi ni nani kati yetu ambae ni "mjuaji juaji"?! Si ni wewe ndie umejitia ujuaji kwa kuniambia Kiswahili sikijui na kwahiyo niongee lugha ya kikwetu wakati wala hunifahamu!!!
 
Ee Mungu, muweza wa yote, asante kwa kuifanya singeli ibakie Dar es salaam japo upepo wa fiesta ulitaka kuieneza hata huku bara, Bwana tunakushukuru kuwalinda watoto wetu na aina hii ya muziki ambao wavulana wanabinua tu-makalio kama ngedere usifike huku mikoani. Ameen!
 
Hahahaaa mkuu nakuona wewe n mjuz Wa lugha nimefurah ila hata mjinga ni tusi kubwa endapo mjinga ataitwa mjinga na mwenye elim au mwenye slim akimuita mwenye elim mwenzake mjinga lakini kama mjinga akimuita mjinga mjinga hakuna tatizo au mshenz akimuita mshenz mwenzie mshenzi si tusi ni sifa
Swadakta... nakubaliana nawe mia kwa mia pasi na japo ya punje ya shaka. Ni kama Marekani... weusi kwa weusi kuitana nigger, rukhsa... ni rafiki ati!! Lakini atokeapo mzungu kumuita mweusi nigger ni kuzua tafurani! Na si tafurani ndogo!! Ni juzi tu hapa kuna mwalimu mmoja mzungu amemwita mwanafunzi wake ambae ni African American kwa kutumia Nigger!

Haidhuru mwalimu huyu anaona tatizo lipo wapi ili hali wenyewe kwa wenyewe waitana vivyo hivyo; lakini hana namna... atalazimika kufanya kul'hali kujinasua na tuhuma za ubaguzi!!

Anyway, hata nami kwenye lile la ushenzi na mshenzi halikuwa na taabu yoyote zaidi tu ya kutaka kunogesha genge! Si unajua watu wa huku kwetu kwa kupenda kupindua pindua maneno na kauli ili mradi tu kunogesha hadhara?!
 
Ee Mungu, muweza wa yote, asante kwa kuifanya singeli ibakie Dar es salaam japo upepo wa fiesta ulitaka kuieneza hata huku bara, Bwana tunakushukuru kuwalinda watoto wetu na aina hii ya muziki ambao wavulana wanabinua tu-makalio kama ngedere usifike huku mikoani. Ameen!
Singeli mbona muziki mzuri tu, sema hujatulia na kuusikiliza kwa makini!!! Lakini iacheni ije manake na nyie watu wa bara hamtaki au mnashindwa kupenyeza miziki yenu na kuileta anga za kisasa!!

Kuna siku nilisikiliza ngoma moja ya asili... niliiependa kweli kweli kiasi cha kutamani lau kama ningekuwa producer basi ningeifanyia kazi ile rhythm na melody yake na kuileta kisasa zaidi! Nilipouliza ni ngoma za wapi zile; nikajibiwa ni ngoma ya Wagogo... cjui inaitwaje!
 
Nauliza tu, maana kuanzia mwakajana kumeibuka utitiri wa vijana wanaoimba muziki huu, je kabla haujaaanza kutambulika mtaani walikuwa wanaimba nini, au walikuwa hawaimbi?

wengi wao walikuwa wapiga kuladaku (daku kula) na vibaka kama walivyo wasanii wa bongo fleva.
 
Nauliza tu, maana kuanzia mwakajana kumeibuka utitiri wa vijana wanaoimba muziki huu, je kabla haujaaanza kutambulika mtaani walikuwa wanaimba nini, au walikuwa hawaimbi?
Wewe...labda ndio ulikuwa hujui ila wengi tunehamia dar tumekuta vijana wanaimba Mnanda ndio singeli tena ilikuwa maaarufu kuliko.Hiphop.
Vijana mitaaa..ya uswahilini Msasani.,manzese ,kigogo,buguruni,vingunguti.,temeke etc walikuwa wanajua wenyewe ratiba na enzi hizo hakuna simu .....
Walikuwa wana uwezo wa kutoka kwa miguu usiku msasani hadi temeke kufuata...mnanda ...it was very stong pengine kuliko..leo.

Utamaduni unaokufa...kwa kasi...ni wa...mdundiko..zamani ilikuwa...kawaida kuwaona wanapita
.Mnanda ulianza kufa kwa kasi miaka...ya mwisho ya 90 baada ya kutumiwa na...vijana wahalifu komando yosso au siku hizi panya rd kama..maficho...na..kupelekea waimbaji wengi kukamatwa na kuishia...keko
" kamucha mume wake kafuata mdundikoooo
Leleee leeee kafuata mdundikooo"
 
Mhh sijui kwakweli labda tumuulize Sugu (II Proud)
Bongo fleva ni muziki ulioletwa na upepo wa Hiphop na R AND B ,waimbaji wa kwanza hawa kina KWANZA UNIT,DIPLOMATZ ,MABAGA,GWM,SUGU etc wengi walikuwa wanakariri flows au copy za makundi...na rappers kama Easy E ,wutang Clan etc na R AND B KINA MR PAUL,FOUR CREWS FLAVOR etc wakiimba za.nje
Kwenye mashindano ya kufoka foka...yaliokuwa.yakiandaliwa na KIM AND THE BOYS kina black moses walikuwa wanawaiga Michel jackson na watu kama SALEH JABIR akawa wa mwanzo kubadili wimbo wa HEAVY D AND THE BOYS kwa ghani za kiswahili
Baadaye miaka ya kati kati ya 90 ndio wengi wakaanza kutunga
 
Swadakta... nakubaliana nawe mia kwa mia pasi na japo ya punje ya shaka. Ni kama Marekani... weusi kwa weusi kuitana nigger, rukhsa... ni rafiki ati!! Lakini atokeapo mzungu kumuita mweusi nigger ni kuzua tafurani! Na si tafurani ndogo!! Ni juzi tu hapa kuna mwalimu mmoja mzungu amemwita mwanafunzi wake ambae ni African American kwa kutumia Nigger!

Haidhuru mwalimu huyu anaona tatizo lipo wapi ili hali wenyewe kwa wenyewe waitana vivyo hivyo; lakini hana namna... atalazimika kufanya kul'hali kujinasua na tuhuma za ubaguzi!!

Anyway, hata nami kwenye lile la ushenzi na mshenzi halikuwa na taabu yoyote zaidi tu ya kutaka kunogesha genge! Si unajua watu wa huku kwetu kwa kupenda kupindua pindua maneno na kauli ili mradi tu kunogesha genge?!
Huu hapa ushahidi wa usemayo!!

Mozee Iyobo akimuita Harmorapa nyani ni tatizo, lakini rafiki wa harmorapa au yeye mwenyewe akijiita Kubwa la manyani ni bonge la Title...
 
Back
Top Bottom