Mwanamayu
JF-Expert Member
- May 7, 2010
- 11,662
- 6,888
Inaonekana neno 'wanyonge' limeshika kasi katika matumizi yake hapa Tanzania, na kutumiwa sana na baadhi ya wakuu kabisa wa nchi. Kwa mujibu wa baadhi ya machapisho, 'wanyonge' maana yake ni 'masikini sana', au 'watu wadhaifu katika jamii'. Kwa Kiingereza ni 'disadvantaged', 'abject poor', au 'weaker people.'
Sasa tangu tupate uhuru CCM wapo madarakani, iweje mpaka leo baadhi ya viongozi wao wakuu waliopewa dhamana bado wanalalamika juu ya uwepo wa wanyonge mpaka kufikia kusema wao ni viongozi wa wanyonge?
Kwa nini wanyonge hawajaisha?
Nani anasababisha uwepo wa wanyonge?
Na kusema kuwa mimi kama kiongozi mkuu nitatetea haki za wanyonge, je nani atatetea haki za wasiokuwa wanyonge? Nani anayetoa haki kwa wananchi? Au wasiokuwa wanyonge upata haki ndani ya sekunde?