Hivi hawa Watanzania 'wanyonge' wana sifa zipi? Na wanapataje hizo sifa?

Wanakubali kuswagwa kama kondoo. Hawawezi kusimama kudai haki zao hata wakiibiwa, wakidhulumiwa, wakitukanwa, wakidharaulika, wakitumiwa, wakidanganywa, wakiumizwa na kuuliwa.

Wao huwa na tabia ya kulalamika chini chini na kumwachia Mungu mateso yao. Watawala hufurahia hali hiyo kwakuwa hutawala bila hofu kwa kisingizio kuwa wanawatetea wanyonge kumbe wanawamaliza.

Msemakweli ni mpenzi wa Mungu. Au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Binafsi mimi sio mnyonge! Hata kama nalala njaa au sina fwedhaaaaa ila mambo ya kuitana "MNYONGE" yaishue Lumumba tu hukohuko... [emoji847][emoji847]
 
Sifa:-
1) UWE MTOTO WA MKULIMA, MWALIMU, MCHUNGAJI au MFUGAJI->wale wa zamani.

2) UWE ULISOMA SHULE ZA KAWAIDA SIYO MIDIAM

3)KATIKA MAISHA YAKO UWE UMEWAHI KUCHUNGA MBUZI, KULIMA KWA JEMBE LA MKONO, KUTEMBEA PEKU, KUTEMBEA MWENDO MREFU KWENDA SHULE, KUISHI KWENYE NYUMBA ISIYO NA BATI

->Hii haijalishi hali ya maisha uliyo nayo sasa.
->Kwa vigezi hivyo wewe ni MNYONGE au MTOTO WA MASKINI
 
Dharau ya Viongozi Nchi hii Umasikini umeletwa na CCM na Majina yanatolewa na Hao Hao VIONGOZI
 
Sifa yakuwa Mnyonge ni kuwa MJINGA

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo tumebatizwa jina la WANYONGE na kwa kiasi kikubwa tumelikubali, kwa kuwa tumewaachia watu wachache ndiyo wawe wenye kufikiri kwa ajili yetu. Tanzania ni ya watanzania wote si ya CCM wala Chadema wala ACT wala chama chochote si ya waislamu wala wakristo wala imani yoyote, wala si ya kabila lolote. Hili neno tulikatae kwani kuna kiongozi alishawaita watu wapumbavu, haya ni maneno ya dharau na kejeli kutoka kwa viongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…