Hivi hawa watu wanatokaga wapi?

Hivi hawa watu wanatokaga wapi?

normally

Senior Member
Joined
Aug 1, 2018
Posts
194
Reaction score
167
1. Mtu anapiga simu usiku unapokea alafu anauliza umelala? Huyu huwa anataka nini hasa mimi nitakuja ni mjibu mtu ovyo alikuaanataka nimjibu vp?

2. Mtu huna stress zako alafu wapumbavu Fulani wanakutumia sms hongera umechaguliwa kushinda jackpot ya milioni 40 alafu wanakwambia unachotakiwa kufanya shiriki Sasa. nishiriki VP na nimechaguliwa kushinda si mnipe hizo pesa zangu nikafie mbele.

Huwa nataga nivunje lain sema Kuna watu wa muhimu nawasiliana nao.
 
Bibi yangu alikua ana mtindo asubuhi anakuja chumbani ukiwa umelala kabisa "si unajua usingizi wa asubuhi"

Anakutingisha kabisa CONTROLA wee CONTROLA then unaamka kiuchovu na hasira halafu anakuuliza

"umeamkaje mjukuu wangu" siku moja mi nilimjibu "bado sijaamka subiri nilale nkiamka ntakujibu"
 
Mchizi na madevu yake anakupigia simu:-

Wewe: Hallo
Mchizi: Hallo habari bwana?
Wewe: Salama aisee
Mchizi: Niambie ...

Hapo ukiangalia ni mida mibovu, uko busy kabisa halafu jinga linakupigia linakuambia niambie...
 
Back
Top Bottom