Nashangaa mtu anamcheka mtoa mada au kumshangaa halafu hamsaidii chochote..
Mkuu Unapoona Vitu hatalishi kama hivyo vimekubalika katika maeneo hatalishi basi ujue pale ukomo wako ulipoishia ndio wenzako wakaanzia kwenda juu...
Kuta za vioo Ni Salama kwa kiwango ambacho huwezi zania,
Kile kioo unachokiona pale kina upana wa mm12, vinakua viwili ndani 6mm iliyokua subject to Tension katikati 1mm kwa ajili ya hewa halafu nje 6mm nyingine iliyokua subject to compression(Ulisoma Effects of forces 4m2?)
Kitaalam wanaita Tempered glass,
Ni kioo cha kawaida kinachopitishwa kwenye joto la 600°c-1400°c baada ya hapo kinapitishwa kwenye very high pressure cooling air system kinapozwa haraka sana ndani ya sekunde kadhaa..
Kitendo hiki kinafanya upande wa nje kusinyaa(ref kutanuka na kusinyaa kwa mada) hii inaleta compression halafu upande wa pili unajivuta kutoka nje na kutengeneza tension, kazi inakua imeisha na hapa ndipo sifa ya ugumu wa hivyo vioo unapopatikana, na vinakua na ugumu ×5 ya kioo cha kawaida..
Sasa Vingine vinakua laminated, yaani pale kati baada ya kuacha space ya hewa wanaweka plastic ambayo nayo ni transparent kama kioo halafu process kama hio inafanyika, hiki cha namna hii sasa ndio usiombee.
Kutokana na hizo mechanical process hapo unafanya pia hicho kioo hata kikipasuka, badala ya kutoa vipande vikubwa kubwa vinavyoweza kumkata mtu, inatoa chenga chenga ndogo(ushawahiona kioo cha gari kimepasuka?)
Hawatumii kioo kwenye ujenzi eti ili kufanya jengo livutie.. kuna advantage nyingi sanaaa...
1. Kupata mwanga wa Asili hii hupelekea kupunguza gharama za umeme kuwasha taa mda wote kwa ajili ya mwanga
2. Kupunguza uzito hatimaye gharama ndogo za msingi..
3. Haviungui,(Tumeona kilichompata mwenzetu kule kimara)
4. Kioo hakiathiliwi na hali ya hewa(nahisi unaelewa ukuta wa nyumba uliopigwa rangi ukipigwa sana na jua)
5. Ni water na dustproop( kii hakipitishi maji na hakipokei vumbi kirahisi na ikiw hivyo kinafutika kirahisi).
6. Ujenzi wa haraka..
Nimejitahidi kutumia terminology nyepesi kadiri niwezavyo japo ni ngumu kuelewesha baadhi ya mambo kwa kiswahili.
NOTE: usalama wa kitu chochote una ukomo wake, katika matumizi ya kawada na emergency, ukizidisha yatakukuta kama ya [emoji116]
View attachment 1859335
Na ukienda ukajaribu menginenyo mimi simo.