Hivi haya mambo yana faida gani kwa Walimu zaidi ya kutapeliwa hela? Nani aliyeturoga?

Hivi haya mambo yana faida gani kwa Walimu zaidi ya kutapeliwa hela? Nani aliyeturoga?

informer1

Member
Joined
Jul 23, 2024
Posts
34
Reaction score
28
Habari za saa hizi Makada wa CCM.

Ndugu zangu wanaSongwe mliambiwa kuwa kutakuwa na Mafunzo ya Walimu Makada wa CCM yatakayofanyika tarehe 02.11.2024 hadi 03.11.2024 , Wilaya ya Mbozi eneo la Mpakani na Mbeya kata ya Nanyala katika ukumbi wa sekondari ya SONGWE SUNRISE Mafunzo haya yataendeshwa na Viongozi ngazi ya Taifa baada ya Mafunzo Washiriki watapatiwa vyeti vya Ukada kama Utambulisho maalumu wa ukada wa Mwalimu atakaye hudhuria

Aidha, baada ya kupewa vyeti vya Mafunzo hayo kila Mwalimu wa CCM aliyepata Mafunzo nakala ya Vyeti vitawekwa kwenye Faili na kupelekwa Ofisi ya KATIBU CCM MKOA WA SONGWE na KATIBU WA CCM WILAYA SONGWE kwa utambulisho maalumu ya Ukada.

Majukwaa yote ya Walimu Makada wa Chama Cha Mapinduzi yana Mipango mizuri na kabambe juu ya Maadalizi ya Mafunzo hayo asante sana JUKWAA LA WALIMU MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA SONGWE kwa mwitikio unaoendelea wa uhamasishaji juu ys suala Michango itakayo tumika kutengeneza Vyeti vyetu jitihada zenu zinaonekana.

Niwaombe ndugu wanaSongwe Makada watiifu na Wazalendo tuhanasishane juu ya hili tusikose fursa hii adhimu ya Chama ukiwa kama mwanaCCM lazma kuwa mstari wa mbele kupata Madini yatokanayo na CCM

Niwaombe tuhamasishane ili wanaSongwe tukawe wengi kwenye Mafunzo hayo

Uongozi wa JUKWAA LA WALIMU MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI NGAZI YA MKOA unashughulikia eneo la kulala, Chakula, Vinywaji na Ukumbi kwa kuwaomba wadau mbalimbali ili kuwezesha Mafunzo haya Muhimu

Narudia tena tuhamasishane juu ya Mafunzo haya ili kila aliye Mwalimu na Kada wa Chama cha Mapinduzi akahudhurie Mafunzo.

Asanteni.

Mwl. SAID MWALIS NGONDO
KATIBU WA JUKWAA LA WALIMU MAKADA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA SONGWE.

Simu namba: 0765053050
My take

Kwanini haya mambo wakati wa uchaguzi, Hebu oneni aibu basi kama njaaa zificheni, halafu mnaenda kusambaziana ukimwi walimu kuweni makini
 
Nchi ina vimbwanga hii🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Habari za sahizi Makada wa CCM.
Ndugu zangu wanaSongwe muliambiwa kuwa kutakuwa na Mafunzo ya Walimu Makada wa CCM yatakayofanyika tarehe chaguzi,Hebu oneni aibu basi kama njaaa zificheni, halafu mnaenda kusambaziana ukimwi waalimu kuweni makini
Walimu wanatumika sana aisee
 
Walimu Tanzania ni mbumbumbu na vilaza waliopatiwa nafasi na mfumo kutengeneza mbumbumbu wengi ili nchi iendelee kuwa chini ya mambumbumbu walioungana na kuwa chama cha siasa kiitwacho Xixiem.
Zao la mbumbu huwa ni mbumbumbu sasa wewe unakosaje kuwa mbumbumbu ikiwa ni zao la mambumbumbu
 
Back
Top Bottom