Ndio maana ikaitwa ndondo cup wee wa wapi mkuluNiseme tu ukweli na bila kuficha au kuwa ' Mnafiki ' ninachokiona katika haya ' Mashindano ' ya Ndondo Cup si vitendo vya ' Kimaadili ' kabisa hasa katika ' Jamii ' yetu ambayo ilianza ' Kustaarabika ' miaka mingi huko nyuma wakati wa enzi za akina Babu na Bibi zetu.
Ama hakika ukisema uende kutizama ' mechi ' huko ukiwa na ama Mkeo au Mwanao tegemea kupata aibu kubwa na ' Kustaajabu ' kwani Vitendo vingi ambavyo nimekuwa nikiviona huko ( katika Viwanja mbalimbali ambapo mashindano haya yanafanyika ) nimekuwa nikiviona sana katika ' Vijiwe ' vya ' bangi / bange ' na kule ambako ' Njemba ' zingine huenda Kunywa Gongo, Wanzuki na Mataputapu.
Kinachonishangaza ' Upuuzi / Upupu ' huu unaendelea na naona sasa unazidi kujizolea ' Sifa ' na tayari umeshaanza kuharibu Kizazi / Jamii lakini Wahusika wakuu wa ufuatiliaji wa ' mienendo ' ya Maadili nchini ' wameunyuti / wamenyamaza ' tu wakidhani kwamba pengine ' Kizazi ' hiki kikiharibika huko mbele ya safari labda ' Vizazi ' vyao havitaguswa au kuathirika kwa namna moja au nyingine.
Napenda sana Mpira na achilia mbali tu kuwa nimeshakuwa ' Mchezaji ' mpira tena mzuri tu kwa Viwango vya Shule, Vyuoni na Kitaani na nawaheshimu mno ' Waandaji ' wa haya ' Mashindano ' hasa ' Makamarada ' wangu akina Shaffih Kajuna Dauda, Alex Luambano na wengineo wote ila nadhani hili la ' Nidhamu ' na ' Maadili ' inabidi waliangalie sana ikiwezekana waanze sasa au kwa misimu ijayo ili iweze kutuvutia Watu wengine kuhudhuria pamoja na Wanafamilia wetu.
Yafuatayo tu ni baadhi ya ' matukio ' ya kusikitisha na kushangaza ambayo kama ukibahatika umeenda kushuhudia ' mashindano ' haya ya Ndondo Cup huwezi kuyakosa:
Uvunjifu mkubwa sana wa ' Maadili ' unaendelea katika hii michuano ya Ndondo Cup hivyo udhibiti wa haraka unahitajika kuweza ' Kuokoa ' hiki ' Kizazi ' na tukumbuke kuwa ' Wahenga ' walisema " Kinga ni bora kuliko tiba ".
- Mashabiki ' Masela ' Kunya ( kutoa haja Kubwa ) hadharani.
- Mashabiki ' Masela ' Kuoga mbele ya Wageni rasmi.
- Mashabiki ' Masela ' Kunyoa ' mavuzi ' yao hadharani.
- Mashabiki ' Masela ' Kushindanishana ' Mikuyenge / Mibolo ' yao mechi ikiendelea.
- Mashabiki ' Masela ' Kuvuta ' Sigara Bwege / Bangi / Puje / Jani ' hadharani.
- Mashabiki ' Masela ' Kushindana ' Kujamba ' hadharani huku mechi ikiendelea.
- Mashabiki ' Masela ' kuwaringishia ' Mikuyenge / Mibolo ' yao wale akina Dada wanaopita Kuuza vitu mule ambapo ' Mashabiki ' wameketi.
Nawasilisha.