Hivi haya mashindano ya Ndondo Cup ni ya kuibua Vipaji au yanaibua Wahuni wa muda mrefu waliotukuka?

Hivi haya mashindano ya Ndondo Cup ni ya kuibua Vipaji au yanaibua Wahuni wa muda mrefu waliotukuka?

Niseme tu ukweli na bila kuficha au kuwa ' Mnafiki ' ninachokiona katika haya ' Mashindano ' ya Ndondo Cup si vitendo vya ' Kimaadili ' kabisa hasa katika ' Jamii ' yetu ambayo ilianza ' Kustaarabika ' miaka mingi huko nyuma wakati wa enzi za akina Babu na Bibi zetu.

Ama hakika ukisema uende kutizama ' mechi ' huko ukiwa na ama Mkeo au Mwanao tegemea kupata aibu kubwa na ' Kustaajabu ' kwani Vitendo vingi ambavyo nimekuwa nikiviona huko ( katika Viwanja mbalimbali ambapo mashindano haya yanafanyika ) nimekuwa nikiviona sana katika ' Vijiwe ' vya ' bangi / bange ' na kule ambako ' Njemba ' zingine huenda Kunywa Gongo, Wanzuki na Mataputapu.

Kinachonishangaza ' Upuuzi / Upupu ' huu unaendelea na naona sasa unazidi kujizolea ' Sifa ' na tayari umeshaanza kuharibu Kizazi / Jamii lakini Wahusika wakuu wa ufuatiliaji wa ' mienendo ' ya Maadili nchini ' wameunyuti / wamenyamaza ' tu wakidhani kwamba pengine ' Kizazi ' hiki kikiharibika huko mbele ya safari labda ' Vizazi ' vyao havitaguswa au kuathirika kwa namna moja au nyingine.

Napenda sana Mpira na achilia mbali tu kuwa nimeshakuwa ' Mchezaji ' mpira tena mzuri tu kwa Viwango vya Shule, Vyuoni na Kitaani na nawaheshimu mno ' Waandaji ' wa haya ' Mashindano ' hasa ' Makamarada ' wangu akina Shaffih Kajuna Dauda, Alex Luambano na wengineo wote ila nadhani hili la ' Nidhamu ' na ' Maadili ' inabidi waliangalie sana ikiwezekana waanze sasa au kwa misimu ijayo ili iweze kutuvutia Watu wengine kuhudhuria pamoja na Wanafamilia wetu.

Yafuatayo tu ni baadhi ya ' matukio ' ya kusikitisha na kushangaza ambayo kama ukibahatika umeenda kushuhudia ' mashindano ' haya ya Ndondo Cup huwezi kuyakosa:

  1. Mashabiki ' Masela ' Kunya ( kutoa haja Kubwa ) hadharani.
  2. Mashabiki ' Masela ' Kuoga mbele ya Wageni rasmi.
  3. Mashabiki ' Masela ' Kunyoa ' mavuzi ' yao hadharani.
  4. Mashabiki ' Masela ' Kushindanishana ' Mikuyenge / Mibolo ' yao mechi ikiendelea.
  5. Mashabiki ' Masela ' Kuvuta ' Sigara Bwege / Bangi / Puje / Jani ' hadharani.
  6. Mashabiki ' Masela ' Kushindana ' Kujamba ' hadharani huku mechi ikiendelea.
  7. Mashabiki ' Masela ' kuwaringishia ' Mikuyenge / Mibolo ' yao wale akina Dada wanaopita Kuuza vitu mule ambapo ' Mashabiki ' wameketi.
Uvunjifu mkubwa sana wa ' Maadili ' unaendelea katika hii michuano ya Ndondo Cup hivyo udhibiti wa haraka unahitajika kuweza ' Kuokoa ' hiki ' Kizazi ' na tukumbuke kuwa ' Wahenga ' walisema " Kinga ni bora kuliko tiba ".

Nawasilisha.
Ndio maana ikaitwa ndondo cup wee wa wapi mkulu
 
Macho yako yameona vitu sana kwa wakati mmoja.... Nimewahi kuhudhulia michuano hii na wala sijawahi kukutana na mambo uliyoyaorodhesha katika bandiko lako Mkuu....
 
Hivi hao sailor ni watu gn? Msiharibu fani za watu,, nyie ni wahuni mavi, mnajiita sailor,,
 
Back
Top Bottom