Hivi haya ni ya kweli wahanga wa ajira?

Hivi haya ni ya kweli wahanga wa ajira?

Chato tena

Member
Joined
Jan 17, 2021
Posts
24
Reaction score
50
“Katika kipindi cha kuanzia July, 2020 hadi January, 2021 jumla ya ajira 450,416 zimezalishwa katika sekta mbalimbali, kati ya ajira hizo, ajira 169,475 zimetokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Serikali na ajira 280,941 zimezalishwa katika sekta binafsi”-Waziri Mpango leo Dodoma

“Katika kipindi cha kuanzia July, 2020 hadi January, 2021 jumla ya ajira 16,067 zimezalishwa katika sekta ya umma, ikijumuisha ajira 13,529 za Walimu, 1,000 za Madaktari na 1,538 katika Taasisi mbalimbali za Serikali”- MPANGO

Mimi kwa kumbukumbu zangu walioajiriwa ni 8000 waliobaki 5000 walisema wataajiri baadae. Kumbe wameshaajiri. Tuendeleee kuwaombea waendelee kuwa hai ili wafaidi maendeleo ya nchi yetu.

Pia ikumbukwe hao walioajiriwa hawajalipwa mshahara kuanzia mwezi wa 12, 1,2 na haijulikani kama mwezi huu mshahara utakuwepo uhakiki umeanza leo waaalimu wapya.Tuendelee kuombeana
 
Kennedy Wengine waliandaa vyombooo walibook ili visije kuisha, mara paa ni mzima😆
 
Kama serikali ingetoa ajira hizo 450k+ basi usingeona mtaani watu na bahasha za kakhi.
 
Inafikia mahala unasema tu
"Mungu tuepushe na huu utawala".
Watu wanaumia sana mtaani huku wakiwa wanadaiwa na HESLB bila ajira.
 
Kwani kipindi hiki Kuna corona na corona inaleta madhara kwenye ubongo , mapafu na sehemu zingine kwa hiyo sio kila habari au takwimu inatakiwa uzikubali zingine tunasema itakuwa sababu ya corona,

Asilimia kubwa tumeathiriwa na corona katika ubongo,
 
Back
Top Bottom