Hivi hii hali mtu huzaliwa nayo au anaikuta?

Hivi uwezo wa mtu kufanya "argument" na kutoa "facts" anazaliwa nao au anaupata katika mazingira yanayomzunguka?

Mkuu upo sawa uwezo wa mtu kufanya 'argument' na kutoa 'facts' mtu uzaliwa nao na pia uupata kutokana na mazingira husika sababu zifuatazo ni baadhi tu zinazothibitisha hilo..
1.uwezo huo upo kwenye DNA za mtu alizorithi kutoka kwa wazazi wake yaani mtu uchukua dna nusu kutoka kwa mama na nusu kutoka upande wa baba hivyo uwezo wa mtu kutoa argument unasababisha na asili ya wazazi wao..
2.pia uwezo wa mtu kutoa argument unatokana na mazingira aliyolelewa toka umri wa miaka 0-12 mfano kam ulikuwa ukiambiwa ww unaakili sana bac hata ukiwa mtu mzima akili yako itakuambia hivyo hivyo kwa unaakili sana..
3.Pia mazingira uliyopitia na unayopitia tangu miaka 13 hadi sasa hapa inajumuisha matatizo,changamoto,elimu yaani mambo yote unayopitia ndio yanayokuwezesha kutoa argument na facts...
Mkuu nimejibu kwa ufupi coz natumia simu but naic utakuwa umepata mwanga kidogo..!!
 
Mkuu hii mada inauwanja mpana sana!

Ni kweli kunahoja zimeshatolewa toka kitambo! Inategemea na issue on table! Ikiwa nature ya issue haizingatii/haiathiriwi na wakati, bila shaka hoja za zamani zitaaply mutatis mutandis!!! But ni lazima kutakua na maelezo na mifano mipya ktk kuitetea hoja hiyo!

Na pia ukumbuke mtu anaweza kuvumbua hoja or kitu ambacho kimeshavumbuliwa bila ya yeye kujua! Na hapo ndio unashangaa kwa kuambiwa "mbona hicho kimeshanyika kitambo tu! Wewe ndio unajua leo?"

Na hapo kwenye mkinzano wa hoja, maamuzi hutegemea na issue husika! Si kila hoja iliyoshinda or iliyokosa upinzani ndio ifatwe! Chek mifano:
  • Religious issue:
    Kuna wenye hoja zisizopingika juu ya upotevu wa imani fulani!
    Hata hivyo watu bado tu wanaendelea kuamini imani yao hiyo!

    Angalia hoja za uwepo na kutokuwepo kwa Mungu!
    Ni wachache sana wanaopinga imani zao kwa hoja za wengine!
    Bora hata mapenzi (romantic love) inafanya watu wabadili dini zao kuliko uzito wa hoja!
  • Issue za mahakamani:
    Kule set of rules tu ndio zinatoa suluhisho! Mwenye hoja zinazokubalika kisheria tu ndio anashinda!

    Hata hivyo uzito wa hoja na burden ya kuproof inatofautiana kutokana na nature ya kesi! mfn: Crmnl case (ili mtu awe hatiani) ni kuproof beyond reasonable doubt =% 90 or 95! Wakati Civil case ni kunzia % 51 tu!
Kama ulivyosema kujenga hoja sometime ni siasa tu!

Hapa #Kiranga angepita, ungemwelewa kitu kimoja anacho alipata kueleza kuwa amezaliwa kwenye familia ya waamini wa Mungu na baadae amekuja kubadilika huyu unamuweka kwenye Dynamism Character? Et . . .
Kiranga siwezi kukusemea, njoo ujibu mwenyewe!
Wewe binafsi hivi una argument yoyote ile ambayo unajua uliiweza kutolea facts pasi kuwa na visababishi vya kukuwezesha zaidi ya lugha inayotamkwa na kuandikwa?
Ndio! Sometimes najenga hoja kwa kuonganisha picha/matukio! Hoja nitakazozitoa hapo zinakuwa za kwangu hata kama kuna mtu alishatumia!

And sometimes naabstract mifano ktk matukio or nilichosomeshwa kwa mtindo tofauti na nilivyosoma!

Mfn: Post ya juu nimekwambia Kinyengetile aliweza kuargue na kuwaaminisha watu kuwa ukijipaka maji ya mto ngarambe, risasi itageuka maji!

Hatukusomeshwa kinyengetile alipotosha watu! Hapo nimetafsiri mwenyewe ili kukazia hoja yangu niliyoitoa! Na sijawahi kumsikia mtu akitolea mfano wa kinjengetile kama ni mtu wa kupotosha watu!

Vile vile natumia sana hoja za mascholars however hoja zao nyenginge nazipinga!
 
Last edited by a moderator:

Baadaye nadhani utarudi na JF ipo mpaka usiku . . . Utani huu,
 

Narudi, kuja kujibu . . . Umeandika mazito sana yanahitaji utulivu.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hii mada inauwanja mpana sana!
kweli ina uwanja mpana sana lakini, ni kupunguza mkanganyiko ni kuelezwa pande zote kwa ufasaha kama wewe unaeleza vizuri sana lakini bado unaacha uwanja mpana wa maswali, hata wachangiaji wengine tatizo wanaacha maswali.


sawa umezungumzia hoja za zamani kwa utumikaji wake yaani kama reference, harafu sasa utetezi wake unazingatia nini hasa? Wewe binafsi haujawahi kuona hoja fulani ipo sawa lakini baada ya kipindi fulani hoja ile ile ukaiona imepotoka kwa mfano nikuulize wewe unaamini uwepo wa laana?

Na pia ukumbuke mtu anaweza kuvumbua hoja or kitu ambacho kimeshavumbuliwa bila ya yeye kujua! Na hapo ndio unashangaa kwa kuambiwa "mbona hicho kimeshanyika kitambo tu! Wewe ndio unajua leo?"
Kwenye uvumbuzi wa hoja mpya sidhani kama Dunia yetu upo zaidi ya zilizopo kuzisema wakati umesahau ulisikia wapi na kujifanya umevumbua lakini si haba nikasema ipo kwa kiasi kidogo sana.

Hapo ndio umeyatetea mazingira kwa ufasaha wa hali ya juu kwamba mazingira fulani yapo hivi ndio yanaelekeana na maamuzi haya na hoja kubwa ilikuwa hii 2+2=4 hoja ndo zinataka mtu uwe yaani bila kukinzana kimawazo, Mfano wapinzani walifika hawakuwa nyuma nao 1+1=4 utaniuliza inakuwaje hapa? Iko hivi waliita Probability maana yake walitengeneza mazingira ya hoja zao kukubalika hiyo imekaa hivi 0.5+0.5+0.5+0.5+0.5=4 kwa kuwa kila nusu inauwezekano wa kukamilika. Nayo hiyo ni hoja?


Kiranga siwezi kukusemea, njoo ujibu mwenyewe!
Atakuja kujibu . . .


Mimi hiyo hoja yako niliisikia CloudsFM kuhusu kuaminisha watu kwa Kinjekitile huenda hata wewe ulipata kusikia huko sema umesahau tu. Kwa kuwa akili ya binadamu unaweza ukaniona leo harafu tukaishi miaka kumi tusionane kwa kuwa umeniona mara moja basi unahisi kwa mara nyingine tumeonana unadhani ndio mara ya kwanza akili ya binadamu sio kubwa sana kuna baadhi ya wanyama wanatuzidi sie tunachojidaia ni Utashi tu.
 
Last edited by a moderator:
Utetezi wake utazingatia nature ya hiko kinakojadiliwa!
Ivi unadhani hoja zote za zamani zina utetezi mmoja?
Wewe binafsi haujawahi kuona hoja fulani ipo sawa lakini baada ya kipindi fulani hoja ile ile ukaiona imepotoka
Hilo linawezekana!
kwa mfano nikuulize wewe unaamini uwepo wa laana?
Ndio naamini!
Kwenye uvumbuzi wa hoja mpya sidhani kama Dunia yetu upo zaidi ya zilizopo kuzisema wakati umesahau ulisikia wapi na kujifanya umevumbua lakini si haba nikasema ipo kwa kiasi kidogo sana.
Jee unafikiria maisha ni marudio ya mambo yaliyopita?
Yap! Ni hoja but haina mashiko!
Hapana mimi sijaisikia popote hiyo hoja!
...
Kwa mujibu wa maelezo yako, ni wazi unaamini hakuna hoja mpya zinazovumbuliwa! Arent you?

Hivi hiyo hoja ya kuwa mimi nimesikia Clouds wakiongea kuhusu kupotosha kwa kinjengetile umeicopy wapi?

Embu nijibu, Nini maana ya hoja?
Kwanini tunatoa hoja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…