Hivi hii ni hali ya kawaida au nina tatizo?

Perry

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
10,058
Reaction score
2,195
Hello JF MMU members?

Jamani nahisi nina tatizo la kisaikolojia linanisumbua na ninaomba kushauriwa nini cha kufanya wakuu siku za hivi karibuni nimejikuta kwanza napenda kukaa mwenyewe mwenyewe tu, hata ndugu zangu wa karibu siwezi kukaa nao tukaongea zaidi ya dakika 5, nitajikuta nimeingia zangu chumbani au nitajikuta naendelea na shughuli zangu tu, alafu sipendi kuulizwa ulizwa maswali na watu naona kama wananikera tu na maswali yao.

Nilikua muongeaji sana na very charming but siku hizi story na watu wala mzaha mzaha sina tena naonekana kama niko serious sana au sijui wengine wanasema nimekua mkali sana.yani kwa kifupi i dont care bout people anymore tukija kwenye mahusiano ya kimapenzi ndo balaa sasa, sina hisia zozote zile za kimapenzi kabisa na mtu yeyote.

Siku mbili tatu nyuma nilikua na mtu wangu but nimemwambia tu anipe relief kwanza maana nilikua sihisi chochote kwake, nikaona nisimpotezee muda bora nimwambie ili kila mtu ashike hamsini zake.

Wakuu hiyo ndio hali halisi inayonikumba kwa sasa, tatizo langu sielewi ni nini maana i have peace of mind maana kama ni familia yetu haina mgogoro wowote wa kifamilia, kazi ninayofanya ni ya kawaida tu ingawa sio permanent but inanilipa vizuri tu.Naomba mnishauri wakuu namna ya kuondokana na hii hali maana nimepoteza idadi kubwa ya marafiki so far.
 
Una umri gani? Hebu kapime homoni zako. Nahisi una tatizo la kukosekana kwa uwiano wa vichocheo vya mwili wako.
 
Kuna kitu kinakusumbua, jaribu kujifikiria utaona
 
Umehisi sawa. Sasa tafuta mwanasaikolojia tu. Kwa tone yako, utakuwa jinsia ya kike, no?
 
Utakuwa na jambo kubwa linakukabili na limechukua sehem kubwa ya MAWAZO yako. Washirikishe jamaa na ndugu upate ufumbuzi mapema
 
Kugundua tatizo ni tiba tosha. Kumbuka ulipoanguka ukatubu, uyaache matendo mabaya uanze matendo mema. Kuna wakati unahitaji kujilazimisha kufanya Yale mazuri unayoona huyawezi
 
24 years.
hata mi nina tatizo kama lako na nina 24yrs sasa sijui ni umri huu hii hali ndio inatokea sipendi kuongea sana nipo busy for nothing hakuna mtu aliyenikera wala nn
 
Tumia muda wako wa ziada kufanya maombi, inawezekana ni pepo, na watu wa aina hiyo huishia kujiua.
 
Waswahili wanasema ukiona hivo ujue malaika izrail kakutumia friend request
 
Hata mie nilishawahi kupatwa na tatizo kama hilo ila niliwahi kujinasua haraka baada ya kujigundua kuwa si hali ya kawaida,nilianza kumpotezea rafiki yangu wa shule ambaye karibu shule nzima wanajua kuwa ni rafiki yangu na nyumbani nikataka kuanza kumpotezea dada yangu kabisa. Kwahiyo mkuu vizuri ushajigundua basi cha kufanya acha kuitumikia hiyo hali na kujilazimisha kurudi katika hali ya kawaida, hali ambayo watu wamekuzoea nayo hata kama hali hiyo itakuwa inakuchukiza.
 
Kama uko kati ya 20-30 ni kipindi kitapita kuna michakato inayoendelea mwilini mwako na mwili hautaki disturbance ya aina yoyote
Usijaribu kuzuia hiyo hali iache itapita yenyewe
Sasa mkuu mpaka hiyo hali ije kupita yenyewe mahusiano kati yake na ndugu au jamaa zake yatakuwa katika halo gani?
 
hata mi nina tatizo kama lako na nina 24yrs sasa sijui ni umri huu hii hali ndio inatokea sipendi kuongea sana nipo busy for nothing hakuna mtu aliyenikera wala nn
Acha kuitumikia hiyo hali mkuu.
 
Achana na punyeto wewe hahahaha
 
Chezea unemployment wewe, endelea kufanya ile biashara yako ya kufuga njiwa mpk watage Bata mzinga. Unyama unyamani tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…