Hivi hii Tume ya Rasimu ya Katiba Itaisha Lini?

Hivi hii Tume ya Rasimu ya Katiba Itaisha Lini?

Muungano wa Tz Ndio muungano Ghari kuliko Miungano yote Duniani ebu Fikiria Zanzibar kuna Rais makamu wa kwanza na makumu wa pili na Tanganyika kuna Rais makamu wa Rais na waziri Mkuu viongozi wakuu 6 yaani Nchi Masikini yenye Watu million 1.5 visiwani na watu million 44 Tanganyika lakini Nchi kubwa inagawana nusu kwa nusu Utawala na Nchi ndogo ni Ruksa kwa mbunge wa ZNZ Kuwa waziri Tanganyika lakini mbunge wa Tanganyika hawezi Kuwa waziri ZNZ hata wabunge wa ZNZ Dodoma wanavuna posho lakini wabunge wa Tanganyika ni Marufuku kunusa baraza la wakilishi bila Ubishi Muungano huu unawanufaisha Zanzibar Ndio Maana wao wanaamua Yao kivyao lakini maamuzi ya Tanganyika ni ya Wote pesa iliyotumika kubembeleza muungano laiti ingelikuwa imejenga hospital pengine tungelikuwa na Hosptal kila kijiji .
 
Tambua Nyerere na Karume waliasisi Muungano wakiwa na Malengo ya muungano kujirekebisha kulingana na wakati hawakusema muungano usirekebishwe ujue Nyerere alijua ipo siku Wananchi watachoka na Muungano Analogia wenye Gharama kubwa Kama huu watataka Kuwa na Muungano Digtal Kama wa U.S.A Nchi 52 Hakuna Wizara ya muungano wala kero za muungano Pia hakuna bajeti za kubembeleza muungano . Nyerere alitambua iwepo wa mabaliko Ndio Maana hata mfumo wa vyama vyingi aliubariki Sasa inatupasa Tanganyika tuzinduke tuje na mfumo bora wa muungano usiokuwa wa Gharama Kama huu .

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu.Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalimbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. uk 18

Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa nikuunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungurnzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo, lingetokea,nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni Shirikisho; au la Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, na Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano.Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. uk 11

Link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 
Naunga mkono hoja yako 100%.
Waende wakafie mbali wayaishi matunda ya aibu Yao yaliyoyataka kuyapandikiza kwa wananchi Watanzania.

Tumezoea kuitwa Watanzania sasa huo utanganyika wapi na wapi?
Kuna mjumbe wa hiyo Tume anaitwa Humphrey Polepole namchukia kwa uongo na umbea wa serikali 3.
Poor them.

Hakuna nchi inayoitwa Tanzania duniani. Tanzania,Utanzania, watanzania,mtanzania ni usanii wa "kihindi" tu. Tafuta historia ya Jina "Tan Zan IA".
 
Muungano wa Tz Ndio muungano Ghari kuliko Miungano yote Duniani ebu Fikiria Zanzibar kuna Rais makamu wa kwanza na makumu wa pili na Tanganyika kuna Rais makamu wa Rais na waziri Mkuu viongozi wakuu 6 yaani Nchi Masikini yenye Watu million 1.5 visiwani na watu million 44 Tanganyika lakini Nchi kubwa inagawana nusu kwa nusu Utawala na Nchi ndogo ni Ruksa kwa mbunge wa ZNZ Kuwa waziri Tanganyika lakini mbunge wa Tanganyika hawezi Kuwa waziri ZNZ hata wabunge wa ZNZ Dodoma wanavuna posho lakini wabunge wa Tanganyika ni Marufuku kunusa baraza la wakilishi bila Ubishi Muungano huu unawanufaisha Zanzibar Ndio Maana wao wanaamua Yao kivyao lakini maamuzi ya Tanganyika ni ya Wote pesa iliyotumika kubembeleza muungano laiti ingelikuwa imejenga hospital pengine tungelikuwa na Hosptal kila kijiji .

Link Warioba: Ikulu kugawanywa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Link Warioba:Serikali tatu sio mzigo

Link Jaji Mark Bomani aitaka Serikali ya Tanganyika - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Link Warioba: Serikali ya Muungano haitakopa fedha - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Naunga mkono hoja yako 100%.
Waende wakafie mbali wayaishi matunda ya aibu Yao yaliyoyataka kuyapandikiza kwa wananchi Watanzania.

Tumezoea kuitwa Watanzania sasa huo utanganyika wapi na wapi?
Kuna mjumbe wa hiyo Tume anaitwa Humphrey Polepole namchukia kwa uongo na umbea wa serikali 3.
Poor them.
Usanii wenyewe ni huu. "Bollywood" act.

"Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya," anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.

Sasa wewe//sisi ni TaganyikaZanzibar-Igbal.Ahamadiya?

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-historia/9543-asili-ya-jina-tanzania-na-mwasisi-wake-4.html

Tamka. Tanganyika, mtanganyika, mdaganyika.....ladha bin ladha, dugu chuki.

Bado unatamani kuitwa mtanzania?
 
Serikali tatu sio kuvunja Muungano. Ni kuvunja Muungano dhaifu sana wa serikali mbili na kuunda Muungano imara kabisa wa serikali tatu ambao kila upande unaridhika! Alafu si kweli kuwa kuna kiongozi yeyote aliyeapa kulinda Muungano wa serkali mbili. Waliapa kulinda Muungano uwe wa serikali moja au mbili au tatu. Wanaotaka serikali tatu wanataka Muungano imara dhidi ya Muungano dhaifu wa serikali mbili. Muungano ni wa muhimu hasa ule wa serikali 3.

- Wale wote wanaotaka Serikali 3 nia na madhumuni yao ni kuvunja Muungano, wafike pahali wasimame kwenye majukwaa tuwasikie wakisema hivyo kwamba wanataka kuvunja Muungano, sasa kwa hawa waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere wakautetea na kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote leo wanapotuambia hawautaki inaleta maswali mengi sana kuliko majibu,

- Wote ni watu wa hatari sana, Jumbe alipokuwa hataki Muungano mboina hawakusimama na kumtetea kwamba yupo sawa? Maalim Seifu alipookuwa CCM hataki Muungano mbona hawakusimama na kumtetea ? leo Mwalimu hayupo hawataki Muungano, ukweli ni kwamba hawafai hata kuwasikiliza, watatuambia nini sasa eti wamebadilika baada ya Mwalimu kuondoka? Shame on all of them ni wasaliti wakubwa wa Taifa na dhambi hii itawatesaa mpaka mwisho wa maisha yao, ndio maana hili Taifa tumeshindwa kwenda mbele sana ni kwa sababu siku zote tulikuwa na maviongozi kama hawa with no msimamo,

- Hawa walishindwa nini kusimama mbele ya MWalimu na kusema hawataki Muungano tuone ubavu wao, wote ni wanafiki wakubwa tena hatari sana kwa Taifa, ninasema hivi hawa wanachotaka ni kuvunja Muungano na huku wamekula kiapo cha kulinda na kutetea Muungano, waondolewe haraka sana, na ni aibu sana kumpa Mwenyekiti wa tume hiyo mufilisi kuongea bungeni mbele ya Taifa ni aibu kwa sababu pale anaenda kumtukana baba wa Taifa Mwalimu, halafu Masikini Mwalimu kuna wakati alikuwa akihangaika sana kutaka kumfanya Warioba Rais, Mwinyi ndiye aliyeua hizo ndoto kumbe aliona mbali sana,

- KITENDO CHA KUMPA RUHUSA MWENYEKITI WA TUME YA KATIBA KUSIMAMA MBELE YA BUNGE NI KUMDHIHAKI BABA WA TAIFA MWALIMU AMBAYE VIONGOZI WENGI WANAFIKI WANADAI WANAMUENZI KUMBE NI NYOKA WA HATARI SANA, MWENYEKITI WA TUME AKABIDHI TU RIPOTI AONDOKE BILA KUSEMA ITAKUWA NDIO KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE!!

Le Mutuz
 
- Nimeshitushwa sana na habari kwamba kesho Mwenyekiti wa Tume ya Rasimu ya Katiba, atapewa Dakika 60 kuzungumza bungeni kuhusiana na Rasimu ya Katiba, so I am like daamn hivi tume itaisha lini it seems like it will never end kila siku tume tume, enough!! Hii tume inataka kuvunja Muungano kwa sababu ndio hasa siri ya wale wote wanaotaka kuvunja Muungano wanalilia Serikali 3 na kura za siri, wanataka tuwe na

1. MARAIS 3, 2. MASPIKA 3, 3. MABUNGE 3, 4. MAWAZIRI WAKUU 3, 5. MAKAMU WA RAIS 3, 6. WAKUU WA MAJESHI 3,

- I mean I can go on and on, nia yao ni moja tu nayo ni kuvunja Muungano ambao wao wenyewe kwa hiari yao waliapa kuulinda kwa nguvu zao zote na akili zao zote, leo wamegeuka na kukana viapo walivyoviapa wenyewe bila kulazimishwa na mtu, halafu bado tunataka kuendelea kuwapa nafasi ya kuongea mbele ya Taifa WHY? Ni muhimu sana kukawepo na mbunge atakayeruhusiwa kumjibu as soon as akimaliza maneno yake ya kuvunja Muungano, Demokrasia inataka maneno na kujibiwa, ameongea sana bila kujibiwa sasa ni wakati muafaka kaanza kujibiwa hapo hapo na hoja zake za Serikali 3.

- I mean kama ni muhimu Mwenyekiti huyo wa Tume ambaye hataki Muungano wa Serikali 2, ampe Mwenyekiti wa Bunge ripoti yake basi aondoke zake, bunge liendelee na mambo mengine, hakuna jipya atakalolisema zaidi ya kulilia kuvunja Mjuungano, shame on tume nzima mlikuwa karibu na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere kwa unafiki unafiki na tabia za mafisi, mlishindwa nini kumwambia Mwalimu akiwa hai kwamba hamtaki Muungano, mmesubiri ametangulia kwenye haki ndio sasa eti mnampinga na Serikali zake 2 mlizozipigania na kuzilinda maisha yenu yote ya kufanya kazi naye tena kwa karibu sana, leo hayupo mmebadilika na maneno mengi ya kilaghai ya kutaka kuvunja Muungano shame on you all!!

Le Mutuz

Umri wako (50+) tofauti kabisa na utoto unaouzungumzia.
 
Umri wako (50+) tofauti kabisa na utoto unaouzungumzia.

Mkuu utaumia kichwa bure kubishana na tikiti maji, you had better keep quite ili wanaharamu wapitishe uanaharamu wao ila huko miaka ya baadaye tutakuja tifuana tu we subiri
 
Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu.Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalimbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. uk 18

Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa nikuunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungurnzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo, lingetokea,nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni Shirikisho; au la Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, na Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano.Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. uk 11

Link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)

umenikonvice kweli ila wakubwa awataki hivyo wao wanataka hivihivi ili wapige kama walivyozoea.
 
Mwalimu Nyerere alichomkatalia mzee Malecela siyoujio wa serikali 3 bali tabia ya sura mbili ktk maamuzi ilihali yeye akiwa Kiongozi mkubwa tena wa Kariba ya Rais.....

Hapa tukubaliane tu kuwa kama Chama CCM hatukuwa tayari kwa move hii sasa .....mengine yote porojooo tu.

Tushawishi UMMA kuwa wakati si muafaka basi...
 
Serikali tatu sio kuvunja Muungano. Ni kuvunja Muungano dhaifu sana wa serikali mbili na kuunda Muungano imara kabisa wa serikali tatu ambao kila upande unaridhika! Alafu si kweli kuwa kuna kiongozi yeyote aliyeapa kulinda Muungano wa serkali mbili. Waliapa kulinda Muungano uwe wa serikali moja au mbili au tatu. Wanaotaka serikali tatu wanataka Muungano imara dhidi ya Muungano dhaifu wa serikali mbili. Muungano ni wa muhimu hasa ule wa serikali 3.

Ni kweli mkuu, kiapo ni kulinda Jamhuri ya Muungano
 
Le Mutuz, tatizo lako ni kungangania Muungano wa serikali mbili. Kumbuka kuwa kuna Muungano wa serikali moja na Muungano wa serikali tatu pia. Kwa mzalendo wa nchi hii kitu cha muhimu ni Muungano. Muungano ni lazima kwa kuwa waliopo kule Zenj ni ndugu zetu wa damu. Ila tukubali kuwa Muungano wa serikali 2 ambao umekuwepo kwa miaka 50 umekuwa na kero na nyufa ambazo wala hazizibiki. Serikali tatu ndio option. Binafsi sikubaliani na mtu atakaye kuuvunja Muungano, bali anayetaka kuwe na Muungano wa usawa wa pande mbili. Na serikali moja ingekuwa ndiyo ideal, lakini kwa kuwa tayari Zanzbar ni nchi kwa vigezo vyote na kwa kuwa hawatakuwa tayari ku-surrender nchi yao kwa muungano wa serikali moja, na kwa kuwa kero zile za serili 2 hazizibiki, suluhisho ni serkali 3. Huu ni Muungano imara kabisa!
 
Back
Top Bottom