Hivi hii Tume ya Rasimu ya Katiba Itaisha Lini?

Muungano wa Tz Ndio muungano Ghari kuliko Miungano yote Duniani ebu Fikiria Zanzibar kuna Rais makamu wa kwanza na makumu wa pili na Tanganyika kuna Rais makamu wa Rais na waziri Mkuu viongozi wakuu 6 yaani Nchi Masikini yenye Watu million 1.5 visiwani na watu million 44 Tanganyika lakini Nchi kubwa inagawana nusu kwa nusu Utawala na Nchi ndogo ni Ruksa kwa mbunge wa ZNZ Kuwa waziri Tanganyika lakini mbunge wa Tanganyika hawezi Kuwa waziri ZNZ hata wabunge wa ZNZ Dodoma wanavuna posho lakini wabunge wa Tanganyika ni Marufuku kunusa baraza la wakilishi bila Ubishi Muungano huu unawanufaisha Zanzibar Ndio Maana wao wanaamua Yao kivyao lakini maamuzi ya Tanganyika ni ya Wote pesa iliyotumika kubembeleza muungano laiti ingelikuwa imejenga hospital pengine tungelikuwa na Hosptal kila kijiji .
 

Muundo wa Muungano, pamoja na kwamba hatutaki uwe ukitibuliwatibuliwa mara kwa mara, ni suala la sera, si amri ya Mungu.Vyama vya siasa mbalimbali vinaweza vikawa na maoni mbalimbali kuhusu muundo unaofaa kwa Katiba ya nchi yetu. Muundo utakaokubaliwa na wananchi walio wengi ndio utakaokuwa sehemu ya Katiba ya nchi yetu. uk 18

Labda ni vizuri kukumbusha kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa nikuunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja. Na wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya, Uganda na Tanganyika zilikuwa katikati ya mazungurnzo ya kutafuta uwezekano, wa kuungana. Kama jambo hilo, lingetokea,nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi mpya ambayo ingezaliwa ungelikuwa ni Shirikisho; au la Shirikisho la Nchi Tatu zenye Serikali Nne, na Shirikisho la Nchi Nne zenye Serikali Tano.Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. uk 11

Link Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)
 

Hakuna nchi inayoitwa Tanzania duniani. Tanzania,Utanzania, watanzania,mtanzania ni usanii wa "kihindi" tu. Tafuta historia ya Jina "Tan Zan IA".
 

Link Warioba: Ikulu kugawanywa - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Link Warioba:Serikali tatu sio mzigo

Link Jaji Mark Bomani aitaka Serikali ya Tanganyika - Kitaifa - mwananchi.co.tz

Link Warioba: Serikali ya Muungano haitakopa fedha - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Usanii wenyewe ni huu. "Bollywood" act.

"Kwa hiyo kwenye ile karatasi nikaandika Tanganyika na Zanzibar kisha, nikaandika majina yangu mawili; Iqbal na Ahmadiya," anasema Dar na kufafanua kuwa Iqbal ni jina lake na jina la ubini na Ahmadiyya ndiyo dhehebu lake.

Sasa wewe//sisi ni TaganyikaZanzibar-Igbal.Ahamadiya?

Link https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-historia/9543-asili-ya-jina-tanzania-na-mwasisi-wake-4.html

Tamka. Tanganyika, mtanganyika, mdaganyika.....ladha bin ladha, dugu chuki.

Bado unatamani kuitwa mtanzania?
 

- Wale wote wanaotaka Serikali 3 nia na madhumuni yao ni kuvunja Muungano, wafike pahali wasimame kwenye majukwaa tuwasikie wakisema hivyo kwamba wanataka kuvunja Muungano, sasa kwa hawa waliofanya kazi na Mwalimu Nyerere wakautetea na kuulinda Muungano kwa nguvu zao zote leo wanapotuambia hawautaki inaleta maswali mengi sana kuliko majibu,

- Wote ni watu wa hatari sana, Jumbe alipokuwa hataki Muungano mboina hawakusimama na kumtetea kwamba yupo sawa? Maalim Seifu alipookuwa CCM hataki Muungano mbona hawakusimama na kumtetea ? leo Mwalimu hayupo hawataki Muungano, ukweli ni kwamba hawafai hata kuwasikiliza, watatuambia nini sasa eti wamebadilika baada ya Mwalimu kuondoka? Shame on all of them ni wasaliti wakubwa wa Taifa na dhambi hii itawatesaa mpaka mwisho wa maisha yao, ndio maana hili Taifa tumeshindwa kwenda mbele sana ni kwa sababu siku zote tulikuwa na maviongozi kama hawa with no msimamo,

- Hawa walishindwa nini kusimama mbele ya MWalimu na kusema hawataki Muungano tuone ubavu wao, wote ni wanafiki wakubwa tena hatari sana kwa Taifa, ninasema hivi hawa wanachotaka ni kuvunja Muungano na huku wamekula kiapo cha kulinda na kutetea Muungano, waondolewe haraka sana, na ni aibu sana kumpa Mwenyekiti wa tume hiyo mufilisi kuongea bungeni mbele ya Taifa ni aibu kwa sababu pale anaenda kumtukana baba wa Taifa Mwalimu, halafu Masikini Mwalimu kuna wakati alikuwa akihangaika sana kutaka kumfanya Warioba Rais, Mwinyi ndiye aliyeua hizo ndoto kumbe aliona mbali sana,

- KITENDO CHA KUMPA RUHUSA MWENYEKITI WA TUME YA KATIBA KUSIMAMA MBELE YA BUNGE NI KUMDHIHAKI BABA WA TAIFA MWALIMU AMBAYE VIONGOZI WENGI WANAFIKI WANADAI WANAMUENZI KUMBE NI NYOKA WA HATARI SANA, MWENYEKITI WA TUME AKABIDHI TU RIPOTI AONDOKE BILA KUSEMA ITAKUWA NDIO KUMUENZI BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE!!

Le Mutuz
 

Umri wako (50+) tofauti kabisa na utoto unaouzungumzia.
 
Umri wako (50+) tofauti kabisa na utoto unaouzungumzia.

Mkuu utaumia kichwa bure kubishana na tikiti maji, you had better keep quite ili wanaharamu wapitishe uanaharamu wao ila huko miaka ya baadaye tutakuja tifuana tu we subiri
 

umenikonvice kweli ila wakubwa awataki hivyo wao wanataka hivihivi ili wapige kama walivyozoea.
 
Mwalimu Nyerere alichomkatalia mzee Malecela siyoujio wa serikali 3 bali tabia ya sura mbili ktk maamuzi ilihali yeye akiwa Kiongozi mkubwa tena wa Kariba ya Rais.....

Hapa tukubaliane tu kuwa kama Chama CCM hatukuwa tayari kwa move hii sasa .....mengine yote porojooo tu.

Tushawishi UMMA kuwa wakati si muafaka basi...
 

Ni kweli mkuu, kiapo ni kulinda Jamhuri ya Muungano
 
Le Mutuz, tatizo lako ni kungangania Muungano wa serikali mbili. Kumbuka kuwa kuna Muungano wa serikali moja na Muungano wa serikali tatu pia. Kwa mzalendo wa nchi hii kitu cha muhimu ni Muungano. Muungano ni lazima kwa kuwa waliopo kule Zenj ni ndugu zetu wa damu. Ila tukubali kuwa Muungano wa serikali 2 ambao umekuwepo kwa miaka 50 umekuwa na kero na nyufa ambazo wala hazizibiki. Serikali tatu ndio option. Binafsi sikubaliani na mtu atakaye kuuvunja Muungano, bali anayetaka kuwe na Muungano wa usawa wa pande mbili. Na serikali moja ingekuwa ndiyo ideal, lakini kwa kuwa tayari Zanzbar ni nchi kwa vigezo vyote na kwa kuwa hawatakuwa tayari ku-surrender nchi yao kwa muungano wa serikali moja, na kwa kuwa kero zile za serili 2 hazizibiki, suluhisho ni serkali 3. Huu ni Muungano imara kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…