Unajua wakati mwingine na sisi watz sijui tukoje? Ingekuwa nchi zingine pasingekalika
Tz tumejaa uoga,unafiki,hofu,mashaka,wasiwasi ndio maana viongozi wetu wanatuona wajinga saana wanatugeuza mazumbukuku
Hakuna ujinga kama kuona mtu anakufa au kuumizwa halafu watu tunakaa kimya, tusipotafakari kwakina hakika tutaendelea kuwa sehemu ya damu zinazomwagika kila siku
Hili ni suala ambalo halipaswi kuingizwa ushabiki wa vyama hata kidogo we are the human being, sote tunahaki ya kuishi bila kujali itikadi zetu
Tuache ushabiki wa kufurahia na kushangilia mabaya
#Leo kwa kwake hatujui kesho ni nani
#Tunapaswa kuupinga ukatili bila kujali tofauti zetu