Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Tuna maoni tofauti lakini mimi hainiingii akilini upate Phd kwa kutumia Kingereza halafu kikupe shida kiasi kile.

Tupo tofauti, kuna watu wapo natural kwenye kujifunza lugha. Kuna mtu namfahamu yupo fluent kwenye lugha tano. At the same time, wengine tuna struggle na lugha moja.
Mimi nina imani tukianza kusikiliza Kiingereza cha PhDs wengi tu, hakitakuwa mbali cha mama. Hasa hasa waliopatia hizi PhD Tanzania.
 
Ndiyo maana PhDs nyingi za Tanzania hazina matokeo chanya kwenye utendaji kwasababu wana PhD jina.
 
Na umesahau vilevile kwamba tupo vizuri kwenye Kiswahili.



Tungekuwa pia wazuri kwenye English kama lugha hizo zingeenda sambamba, tungekuwa tumepiga ndege wawili kwa jiwe moja. (sio yule jiwe wa jf).

Leo imekuwa shida kubwa vya watoto mashuleni, primary wanafundishwa kwa kiswahili wafikapo Secondary hadi vyuoni ni Kiingereza, what a confusion !!!, wewe umeona wapi jambo kama hilo katika nchi kama uingereza, Marekani, japan, Germany Russia, China nk, kote huko wanatumia lugha zao za asili (mother tongue) kufundishia toka Nursery---- University, na wataalamu wa psychology wanasema mtu/mtoto/mwanafunzi anaelewa vyema masomo anapofundishwa kwa lugha mama.

Sasa tuamue tutumie kiswahili kutoka Nursery--- universty au tuendelee na mfumo huu huu wa kimafia wa kuwafanya watoto wakariri masomo kwa lugha isiyo mama na kuendelea kuua vipaji na kuwa tegemezi kwa kila kitu kutoka kwa hao Wazungu.
 
Kama tunaona broken hata wewe basi wewe ni tatizo zaidi kuliko Ndalichako. Rudi kasikilize tena clip
 
Tuna maoni tofauti lakini mimi hainiingii akilini upate Phd kwa kutumia Kingereza halafu kikupe shida kiasi kile.
Ingependeza kama angejikita kusimamia curriculum za mashule na vyuo ambayo ndiyo her defacto job as minister. Hii ya kukagua miradi ya madarasa na majengo angewaachia technical people.

No wonder naye English inampiga chenga kwa vile hakuna anayesimamia mitaala ya English language.
 
Hiki kiinglish nakifananisha na kile cha yule msanii wa kenya, anaitwa kansiime, copyright...
 
Kama tunaona broken hata wewe basi wewe ni tatizo zaidi kuliko Ndalichako. Rudi kasikilize tena clip

Mimi nimepoint makosa niliyoyaona, na wewe point makosa uliyoyaona.

Ngoja nirudie tena ku-list makosa niliyoyaona

1. Matumizi ya “on” badala ya “in”
2. Misamiati michache ( lakini sahihi)

Kosa la kwanza ni common sana, just google “ common mistakes in English” utapata majibu.

Changamoto ya pili( na sio kosa) inatokana na mazingira yetu, ili uwe fluent in English unatakiwa kuzungukwa na wazungumzaji wa hiyo lugha.

Na mwisho kabisa, hauwezi kuzungumza kama native kwa sisi tuliojifunzia Kiingereza ukubwani.

Na tena bora sisi, watu wa Asia ndio wana very strong accent, kuna baadhi ya maneno huwa wanashindwa hata kutamka.
 
Tena kasoma Canada with first class, Kuna shida mahala, ndo maana hazipendi English medium
Hivi kwa mfano angezungumza Kiswahili ili wanaofahamu.kutema yai wakawatemea wale Wachina kungekuwa na shida gani? Mimi TAML mwezi November akiniteua nitakuwa natumia kiswahili tu, shida ya nni?
 
Lugha ya Malkia yataka moyo, ova!
Sent using Jamii Forums mobile app
 


Hao maprofesa walikuwa Waingereza au sio waingereza??, I mean, is English their mother tongue language??
 
Wewe jamaa much know sana. Kweli a little knowledge is a dangerous thing.


Wewe ni miongoni mwa watu wa ajabu, mtu anakusahihisha kutokana na makosa yako badala ya kushukuru unajifanya jeuri maskini!!🤣, sasa unyosha kosa langu hapo katika masahihisho yangu na kama nitakuwa nimekosea nitakushukuru kwa kunifundisha.

Wewe umeandika broken English, eti; " but I am always facing the same problem"--- neno "always" ni neno linaloendana na kitendo cha "simple present tense" sasa utawekaje- I am , ambayo ni "verb to be" ya present continuous tense??.

Mfano, unaweza kusema; I am going to school, yaani ninakwenda shule. (sasa hivi), hiyo ni present continuos tense. . Sasa Ukitaka kutumia neno "always" hiyo sentensi itakuwa; I always go to school. yaani siku zote huwa naenda shule, (huwa naendaga shule 🤣), hiyo ni simple present tense.

Sasa kosa langu liko wapi??, Shida ya waafrika ni hiyo kwamba kukubali kukosolewa mtu anajiona dhalili, kwa mzungu hapo angetoa shukrani kwa kusahihishwa makosa kwasababu wazungu siku zote.ni curious kutaka kujifunza mambo mapya tofauti na waafrika siku zote tupo kupambana sisi kwa sisi ili tusizidiane katika elimu na maendeleo, and that is one of causative of our backwardness.

Much know 🤣🤣
 
Hao maprofesa walikuwa Waingereza au sio waingereza??, I mean, is English their mother tongue language??

English sio first language kwao, lakini wengi wao wameishi kwenye mazingira ya kiingereza for more than 6 years. Huyu mama yetu English ni lugha yake ya tatu baada ya Kiswahili na Kiha, kwangu mimi sio ishu sana.

Kwa sisi ambao English tumejifunzia ukubwani ni ngumu kuwa perfect
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…