Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Hivi hiki ndicho Kiingereza cha Profesa Ndalichako?

Shida ni kwamba huo uprofesa kaupata kwa kutumia Kingereza kama lugha ya kufundishia na siyo kichina wala kiswahili...
Kuna uwezekano mkubwa wa mtu kujua lugha kuiandika na usiwe mzuri katika kuizungumza lugha hiyo.... Kwaiyo kusoma hadi uprofesa haina maana ndio unajua kiingereza zaidi kuliko aliyeishia sekondari tu!!
 
nawewe ndio kopo kabisa, SGR wanajenga waturuki, lakini ujue kiingereza sio dili kiivyo, 34% tu ya watu duniani ndio huongea kiingereza. ureno spain ukienda unaongea kiingereza wala hawakuelewi
kwaiyo umekubaliana na mimi kuwa hata wewe ni kopo mwenzangu!! Lugha sio ujuzi
 
huyu mheshimiwa degree ya pili na tatu kasoma Canada, nadhani alighafirika tu
Canada imegawanyika mara 2, kuna wanakozungumza kifaransa na kuna wanakozungumza kingereza. Obviously kasoma wanakozungumza Kingereza lakini bado anashindwa master lugha aliyotumia kupata hiyo elimu mimi kwangu ni ajabu
 
Tunaotumia free basics jamani tunaomba mwongozo wa maandishi professor ndalichako alikuwa anatema ngeli inayozungumzia nini?
 
Muanzisha thread kajikita kwenye lugha siyo maamuzi aliyo chukua ndalichako dhidi ya mchina... hapa tunajadiri lugha na wasiwasi wa usomi wake
ha ha haaaa kwaiyo kujua kiingereza kunajustify mtu kuwa msomi?
 
Kuna uwezekano mkubwa wa mtu kujua lugha kuiandika na usiwe mzuri katika kuizungumza lugha hiyo.... Kwaiyo kusoma hadi uprofesa haina maana ndio unajua kiingereza zaidi kuliko aliyeishia sekondari tu!!
Mkuu hatusemi azungumze kingereza ka mwingereza, lakini kwa jinsi anavyo zungumza hapo nina mashaka hata kama akisoma kitabu anaelewa
 
Shida ni kwamba huo uprofesa kaupata kwa kutumia Kingereza kama lugha ya kufundishia na siyo kichina wala kiswahili...
Hivi china na russia hamna maprofesa vitabu vya science vimeandikwa kwa lugha za kwao?
 
ha ha haaaa kwaiyo kujua kiingereza kunajustify mtu kuwa msomi?
Kwa mtu aliyepata hiyo elimu kwa kutumia kingereza kama medium of instruction ni "Yes" kama hakijui basihiyo elimu aliipataje ina maana hakuwa anaelewa.
 
Hivi china na russia hamna maprofesa vitabu vya science vimeandikwa kwa lugha za kwao?
Logic hapa ni simple kwani yeye kasoma china au Russia? Kasoma Tanzania na Canada kwa lugha ya Kingereza hivyo hainabudi kuijua kama haijui elimu yake kaipataje na ndiyolugha ya ufundishaji?
Angekuwa kasoma China kwenye vyuo vinafundisha kichina hiyo isingekuwa deal hapa
 
Wacha kumlaumu Nyerere kwa umburula wako na Ndalichako. Mbona kuna Watanzania wengi tu wamesoma mpaka Bachelors tu enzi za Nyerere lakini wanapiga English vizuri tu. Usimtetee huyu Ndalichako ni kilaza



Shida mmekuwa brain washed na the positive side ya nyerere, mkiambiwa the negative yake macho, povu na mishipa ya shingo inawatoka.

Mimi sizungumzii watanzania waliosoma enzi za nyerere, mimi nazungumzia umma wa Watanzania in general---ukiangalia kenya au Uganda sisi tuko poor in English comparatively.

Hao ni jirani zetu Anglophone wenzetu. Sasa kwanini ipo hivyo??-- ni siasa za nyerere kuua kiingereza na kuinua kiswahili.

Ilitakiwa lugha zote ziende sambamba.
 
Write your reply...mmmhhh !! sema za kweli yai la profesa lipo chinii mnoooo , kwa kweli ajitahidi kulibrush japo kidogo . yani kiingereza anaongea yeye lakini aibu naona mimi mweee .
 
Awamu ya Tano inapiga kazi balaa, mama Prop yuko site anatimiza kauli mbiu ya Hapa kazi tu, soon Tanzania itaanza kutoa misaada kwa mataifa masikini, Mama Profesa Mtaalamu anapiga ung'eng'e balaa mpaka huyo mchina anashangaa shangaa hiyo English ya ndani kabisa pale London na kama hujakaa UK huwezi kuelewa kabisa, HIVI HUYU MAMA NI PROFESA NA NI WAZIRI WA ELIMU..?? haya twendeni tu..

Uchumi unakua kwa 7% watanzania wanafurahia maisha mitaan. machinga, mamantilie hawasumbuliwi tena.. Pato la Mtanzania limekua na linazidi kukua kwa kasi..
Kwahiyo kingereza ndo kipimo cha uelewa wa mtanzania

Acheni ulimbukeni , English ni lugha kama zingine

Waafrika tunapenda sana kujidharau na kujenga inferiority complex ndani yetu

Acheni utumwa wa mawazo IQ haipimwi kwa lugha. Huyo mama ni msomi mzuri lakini kusoma kwake usilinganishe na uwezo wake ktk kuongea kingereza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"I believe one day people will understand that English is language and not measure of intelligence" Martin Luther king Jr.
 
Hujaona shida ya alivyoongea Ndalichako kwa vile na wewe ni hujui kama Ndalichako. Hatumlaumu kwa lafidhi bali kwa direct translation na broken grammar.
wewe unajua aya imenisaidia nini kwenye mihangaiko yangu

mchina anaye ambiw hajui pia ila wewe unashadadia kama vile ulikuwa unaambiwa wewe
 
Back
Top Bottom