Mnyamwezi wa Urambo
JF-Expert Member
- Dec 7, 2011
- 928
- 275
Bongo elimu yetu kwa ujumla ni zengwe tu hilo halina ubishi.Lakini jamani katika vyuo vya umma ambavyo vina matatizo usipokitaja Mzumbe utakuwa hutendi haki,miaka michache iliyopita bodi ya TCU iligundua PHD hewa za wahadhiri pale,mpaka sasa idadi ya wahadhiri waandamizi(Hasa Professors) pale Mzumbe hairidhishi hata kidogo,kinachonitisha zaidi vyuo vingine vya serikali wanafunzi wanaodisco kila mwaka ni wengi lakini ni tofauti kabisa na wao,Graduates wa-Mzumbe pia huwa wanakuwa na GPA kubwa sana tofauti na vyuo vingine vya umma.Yaani GPA ya 5 siyo ishu kabisa pale.Halafu wanakatabia kakupokea wanafunzi ambao hawajafanya vizuri form six wanasoma mwaka mmoja then wanajoin undergraduate hii sijaiona vyuo vingine vya umma. Mimi naona mzumbe wamekaa kimaslahi zaidi kama vyuo vya Private lakini umakini hakuna kabisa.Halafu jamani hivi hii inakuwaje mpaka leo kwenye ENCYCLOPAEDIA Tanzania inasomeka inavyuo vikuu viwili tu yaani UDSM na SUA?