Hivi hizi dini za Kikristo ni za kweli?

Dini ni ya ukweli sema wanadamu wamebadilisha au kuongeza vitu kwa maslahi yao.simple

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna dini hata moja iliyokuwa salama, zote zilimezwa na mfumo wa dunia na ulimwengu.

Muumba angeamua kuhukumu asingepona hata mmoja.

Na kweli iliyokuwa imefichwa ni Muumba hana dini wala dhehebu au kabila bali yeye ni UPENDO ULIOPITILIZA unaofuta mauti.

Alisema mwenyewe Wakati ukifika ataishi ndani yetu wote,vyote na wote(isaya 57:15).

Ufunuo 21:3
Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao.
 
Hakuna mistari yoyote kwenye biblia iliyosema ukristo ni dini
 
Aisee
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya dini za kikristo na Yesu Kristo mwenyewe. Na kwahiyo wapo wafuasi wa dini za kikristo wanazoanzisha watu na kupata hao wafuasi.

Yupo Yesu Kristo ambaye siyo dini bali ni mkombozi wa walimwengu na Njia pekee ya kuurithi ufalme wa Mungu Baba. Wafuasi wa Yesu Kristo ni tofauti kabisa na wafuasi wa dini za kikristo! Mfuate Yesu Kristo na si dini ya kikristo!
 
Muumba hana dini yeyote wala dhehebu au kabila, Yeye ni upendo uliopitiliza zaidi ya imani maana wote ni wake.
 

Umekusudia ukristo wa kanisa lipi na biblia ipi ??




Your browser is not able to display this video.
 
Mbona unawaandama wakristo tu, Waislamu wenyewe wako sahihi?


Waabudu wa kweli watamwabudu baba....

“…. waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli, kwa maana hao ndio aina ya waabuduo Baba anawatafuta. Mungu ni roho, na wamwabuduo imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
( Yohana 4:23,24 )- Bible Gateway

Yesu alionyesha waziwazi kwamba Waabudu “WA KWELI” wangekuwa wale waliomwabudu Baba yake aliye mbinguni.

Ni nini kitatokea kwa wale wanaomwabudu Yesu kama mungu ???

Mathayo 7

21 “Si kila mtu anayeniambia, ‘Bwana, Bwana,’ atakayeingia katika Ufalme wa mbinguni, bali ni yule tu anayefanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

22 Wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako na kwa jina lako kutoa pepo na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?’

23 Ndipo nitawaambia waziwazi, ‘Sikuwajua ninyi kamwe. Ondokeni kwangu, enyi watenda maovu!’

kwa hivyo Ndugu na dada Wakristo, Mwabudu Baba sio Yesu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…