Shalom wapendwa,
Niwajulishe tu mimi ni mhanga wa zile kampuni zinazojitangaza zinauza viwanja redioni.
Unasikia matangazo: “Njoo Jumamosi saa kumi ukaangalie kiwanja chako…”
Mimi nililipa, na baada ya muda nikafika. Nilipokuta, ndugu wengine nao walikuwa wakisema mali zile ni zao. Hawa wanaoletwa hawajawalipa mpaka sasa—wanawaonyesha tu viwanja hewani.
Aisee! Baada ya kuhangaika sana, ile kampuni tulikutana nayo sehemu ya mbele.
Baadaye wakaomba radhi, wakasema watanipa kiwanja Mlandizi.
Nikampa dogo mmoja, sijui hata kama aliwahi kufika au kujenga.
Leo nafunguaga redio kwenye gari, nasikia tena kama yote. Sio kampuni moja tu—na hawa wahuni redioni wanavyowapamba unaweza kudhani unanunua kiwanja Marangu!
Aisee…
Watalaaniwa sana.