Hivi huku Mitaani huwa tunadanganyana tu au huwa kuna ukweli kuhusu Nyumba ya Rais wa SADEKI

Hivi huku Mitaani huwa tunadanganyana tu au huwa kuna ukweli kuhusu Nyumba ya Rais wa SADEKI

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwa tuliobobea Kukaa sana Vijiweni hadi sasa tumeshakomaa na hivi Vijiwe vyetu mbalimbali Jijini mnapokaa utasikia Watu wanaanza kusema kuwa kumbe Nyumba anayoishi Rais wa SADEKI ina Vyumba vingi sana na kwamba huwa halali katika Chumba Kimoja kila siku badala yake huwa anahamishwa hamishwa tu kama sehemu yake ya Kumlinda na Maadui zake.

Na kama haitoshi bado hapo hapo huwa humu humu Vijiweni Kwetu utawasikia tena Watu wakisema kuwa sijui katika Nyumba ya Rais wa SADEKI kuna Handaki moja la chini kwa chini linalotokea hadi katika Maji ya Kihindi yaliyoko jirani nae ili kama pakitokea hatari basi utamsikia yuko kwa Majirani anakunywa zake Kahawa tu.

Haya wana SADEKI Wenzangu karibuni nanyi mtoe hapa uzoefu wenu juu ya haya kwani Vijiweni kuna ‘ Stori ‘ sana tu.
 
Ni porojo tu IQ za vijiweni hizo

Sasa kama ni Porojo tu za Vijiweni inakuwaje wale Jamaa wa DG DAM mara nyingi huko ndiko hupenda Kukita Kambi ili kuweza Kuandika vyema Ripoti zao za Siku na ambazo pia huwa zinaaminika na hata Kufanyiwa Kazi? Kuna Mtu Mmoja nakumbuka aliwahi Kuniambia kuwa kamwe nisije Kuwadharau Watu wa Vijweni au hata Mawazo yao kwani Fikra nyingi za Ustawi wa nchi huanzia hapo / huko na ndiyo maana hata Hayati Baba wa Taifa mara nyingi alikuwa akipenda sana Kujichanganya kama siyo Kujumuika nao na sidhangai pia kuwa ilimsaidia Kuongoza vyema na Kimaadili kabisa nchi yake wakati huo.
 
Back
Top Bottom