Hivi huu msamiati mpya "Kushenyeta" au "Kushenyetwa" unamaanisha nini?

Hivi huu msamiati mpya "Kushenyeta" au "Kushenyetwa" unamaanisha nini?

Hili neno "kushenyeta" naliona kwenye muktadha tofauti tofauti sana na inanipa ugumu kujua maana yake halisi ni nini.

Wataalam wa lugha hebu tuambieni maana halisi ya hili neno
IMG_2089.jpeg


Case closed
 
Kushenyenta kiujumla ni kufanya

Sasa inategemea neno limetumika kwenye muktadha gani

Mfano kushenyenta msosi ni kula
Kushenyenta pesa za ada (kula)

Mwizi ameshenyentwa kofi (zaba)

Gari limeshenyenta ukuta (gonga, paramia)

Ameshenyenta biashara (piga kazi ya maana)

Mwanafunzi ameshenyenta mtihani (faulu kwa alama za juu)

Dogo ameshenyentwa na mtihani (ameshindwa vibaya)

Ameshenyenta usingizi tangu jana (lala fofofo)

Mvua imeshenyenta mwaka huu (nyesha kwa kiwango kikubwa)

Paskali ameshenyenta pamba (valia pigo la maana)

Kibaka ameshenyentwa na wananchi (amepewa kichapo kikali)

Kangi Lugola alishenyenta muziki hadharani (katika au densi kwa ufundi wa aina yake)
 
Back
Top Bottom