Kuna wanaosema mbona Adele wimbo wake umerudiwa sana...ni kweli ila kwa mazingira na nafasi ya Adelle sio rahisi kuona tishio kwa wimbo wake kurudiwa na Wanamuziki wasio na majina, kwani hata huyo Mrudiaji naye hana cha kupoteza....ila mtu kama Joe hawezi kufanya hivyo bila kuwasiliana na Adele kwanza.
Manu Dibango angeweza kupotezea tu pale vionjo kutoka wimbo wake vilipotumiwa na Michael Jackson kwenye mziki wake...lakini kwa kuwa Dibango aliiona fursa akampeleka MJ mahakamani na kulipwa fidia....kumbuka ni kionjo tu sembuse wimbo mzima..ubunifu wa mtu/watu lazima uheshimiwe.
Tatizo tulilonalo huku kwetu kubwa ni la kutozingatia sheria mwanzo mpaka pale unapojitokeza mzozo ndio watu wanatafuta sheria ziko wapi.
Hiyo kazi uliyoirudia bila mazungumzo ikitokea kuanza kukupa dili usitarajie mwenye kazi yake atakaa pembeni na kukuangalia tuu, lazima mtashikana mashati...ni bora mmalizane mapema na labda hata unaweza kupata ruhusa bila malipo yoyote.
Kuheshimu sanaa ya ubunifu ni pamoja na kuwa na taratibu na sio kuacha kila mtu afanye anavyotaka...kila cover ya bongo ipate baraka ya mwenye haki miliki (kwa maandishi)....hizo za kina Adele zifanyeni tu mnavyotaka, coz ukishakuwa Mnyonge una kibali automatic cha kuhurumiwa na jamii kutoka mbinguni...na Adele hawezi hata kukutafuta akuulize.