Kwanza lazima nikukumbushe kitu..! Unapoongea pekeyako uwe makini kwakuwa unasikiliza....halafu unajikosokoa halafu unajiuliza na kujijibu ni wazi unaongea na wewe mwenyewe au na wengine kupitia wewe mwenyewe
wewe huko pekeyako uko wanne kwenye jumba moja
1.wewe jina
2.wewe mwili
2.wewe nafsi
4.wewe wewe
Kivipi
1.utambulisho wa jina/Muhuri kiapo cha kutambulika (ID)
2.wewe mwonekano haiba yako sura yako nk nk (AVATAR)
3.wewe nafsi. Uhai na ufahamu(SOUL)
4.Wewe utatu katika moja (me myself and I)
Utambulisho ndio mzizi kisha unakuja umiliki wa vitu na mali na mwili nk, kisha anakuja coordinator wako (ufahamu)halafu unakuja wewe mwenyewe
Kwahiyo unapoongea pekeyako unaongea na wewe mwenyeweunaunda maumbo unaunda roho za visasi unafanya mambo machafu au mema unapanga hili na kupangua lile. ..ni wewe mwenyewe huyo uko pekeyako
Matokeo ya dunia tuliyonayo leo hii kwa uzuri ama kwa ubaya kwa huzuni ama kwa furaha kwa kushindwa ama kwa kushinda ni matokeo ya mazungumzo yetu wenyewe kishapo kwenda kwa wengine yakitoka na kupitia kwetu wenyewe
Kumbuka kitu kimoja bila muunganiko wa vitu vitatu hakuna wewe yaani bila utambulisho mwili na roho wewe haupo na hujulikani...tunapozungumzia u mimi hapa ndio penye asili yake
Mwili unapoachana na roho wewe unatoweka na kubaki
1.mwili wako
2.roho yako
3.vitu vyako
4.familia yako
Nk nk
Upo kama wewe wakati mapigo ya moyo yanafanya kazi tofauti na hapo ni habari nyingine
Ni wazi hapo ulipo muda huu umezama kwenye fikra nyingi kuhusu maisha unaongea na wewe mwenyewe unajiumbia hofu na mawazo ya kutisha na kushindwa...unautesa mwili na ufahamu wako bure kwakuwa wewe sio wewe hivyo vitu vikishatengana
Jiulize tena huwa ukiongea pekeyako unaongea na nani?utapata jibu la kushangaza mno
Cha kushangaza ni kwamba unapokuwa katika hali ya kawaida huna msongo wa mawazo ama jambo linalokusumbua mazungumzo yako mwenyewe huwa mazuri na hayatoki nje ya masikio yako yani ni kama unajinong'oneza LAKINI mambo yanapobadilika ukawa na vitu vigumu vinakukabili nafsi yako hukuacha na kujitenga nawe na ndio hapo huongea kwa sauti ili isikie
Ni kwa muktadha huo hujenga daraja kutoka kwako mpaka kwenye nafsi nayo na kupitia hapo mazungumzo yako huenda kuongea na wengine hasa wale waliokuumiza kihisia kwa namna yoyote ile au changamoto za maisha
Wanaoongea pekeyao barabarani hawapo tena ndani yao wako tayari kwenye dunia tatu ya nafsi ya binafsi na ya ulimwengu
Haya ni mawasiliano ya kiroho.. Una kitu kinaitwa foreseen.. Wengi tuna hiyo hali lakini kwa viwango tofauti tofautiMkuu Mshana Jr Asante kwa fundisho lako
Kuna jambo bado linanitatiza, kipindi niongeapo mwenyewe, kuna mawazo ya mtu fulani hunijia; hua nazungumza juu ya uhalisia wa maisha yetu tulivyo sasa na kipindi cha nyuma.
Baada ya muda fikra hasi kuhusu yeye hutawala na mdahalo kuisha, ila mara tu baada ya kuacha kuwaza, hua ananipigia simu au kunitumia sms na mazungumzo ya kawaida kuendelea.
Kwanini hicho kitu hutokea maana ni mwaka wa pili sasa hunitokea?
Mazungumzo yasiyosikikaNaunga mkono hoja,napiga story nyingi sana alone kichwani.vikizidi mikono huhusika na badae napiga story tu kwa sauti nipo alone hapo njiani mpk najistukia km ha naongea peke yangu.
Maisha tunapitia mengi sana
[emoji1545][emoji1545][emoji1545]Kwa mtazamo wa psychology wa sigmund Freud's tunatawaliwa na mambo haya 3, upande mmoja unaposhindwa kufanya maamuzi unaathiri UPANDE mwingine.View attachment 1530440View attachment 1530445
Kwa mtazamo wa psychology wa sigmund Freud's tunatawaliwa na mambo haya 3, upande mmoja unaposhindwa kufanya maamuzi unaathiri UPANDE mwingine.[emoji1545][emoji1545][emoji1545]Kwa mtazamo wa psychology wa sigmund Freud's tunatawaliwa na mambo haya 3, upande mmoja unaposhindwa kufanya maamuzi unaathiri UPANDE mwingine.View attachment 1530440View attachment 1530445
Mkuu Mshana samahani kuingilia Mada jana Usiku nimeota niko Uchi kabisa kuna jirani yangu ni mtu mzima tena tunaheshimiana na ana pesa sana kakaa kwenye kiti mimi nikaja pembeni yake nimeinama huku mbele yuko mke wake kasimama kama katupusha tuongee kiukweli nimeogopa sana nine Tafsiri yake? NitashukuruRoho zinazotangatanga zinahusika sana hapa na sometimes mambo ya kishirikina
Takurudia usijaliMkuu Mshana samahani kuingilia Mada jana Usiku nimeota niko Uchi kabisa kuna jirani yangu ni mtu mzima tena tunaheshimiana na ana pesa sana kakaa kwenye kiti mimi nikaja pembeni yake nimeinama huku mbele yuko mke wake kasimama kama katupusha tuongee kiukweli nimeogopa sana nine Tafsiri yake? Nitashukuru
hayawani maana yake ni nini,au limetokana na neno ganiHapa ni kwa vile binadamu ana utashi na mnyama ni hayawani
Tuna tabia tunapoudhiwa kuwaita wengine hayawani! Ni kwa vile tu hatujawaza vema lakini kumuita mtu hayawani ni kukosoa uumbaji kwakuwa hayawani ni mnyama