Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wasiojulikanaKwanza lazima nikukumbushe kitu..! Unapoongea pekeyako uwe makini kwakuwa unasikiliza....halafu unajikosokoa halafu unajiuliza na kujijibu ni wazi unaongea na wewe mwenyewe au na wengine kupitia wewe mwenyewe
wewe huko pekeyako uko wanne kwenye jumba moja![]()
1.wewe jina
2.wewe mwili
2.wewe nafsi
4.wewe wewe
Kivipi
1.utambulisho wa jina/Muhuri kiapo cha kutambulika (ID)
2.wewe mwonekano haiba yako sura yako nk nk (AVATAR)
3.wewe nafsi. Uhai na ufahamu(SOUL)
4.Wewe utatu katika moja (me myself and I)
Utambulisho ndio mzizi kisha unakuja umiliki wa vitu na mali na mwili nk, kisha anakuja coordinator wako (ufahamu)halafu unakuja wewe mwenyewe
Kwahiyo unapoongea pekeyako unaongea na wewe mwenyeweunaunda maumbo unaunda roho za visasi unafanya mambo machafu au mema unapanga hili na kupangua lile. ..ni wewe mwenyewe huyo uko pekeyako![]()
Matokeo ya dunia tuliyonayo leo hii kwa uzuri ama kwa ubaya kwa huzuni ama kwa furaha kwa kushindwa ama kwa kushinda ni matokeo ya mazungumzo yetu wenyewe kishapo kwenda kwa wengine yakitoka na kupitia kwetu wenyewe
Kumbuka kitu kimoja bila muunganiko wa vitu vitatu hakuna wewe yaani bila utambulisho mwili na roho wewe haupo na hujulikani...tunapozungumzia u mimi hapa ndio penye asili yake
Mwili unapoachana na roho wewe unatoweka na kubaki
1.mwili wako
2.roho yako
3.vitu vyako
4.familia yako
Nk nk
Upo kama wewe wakati mapigo ya moyo yanafanya kazi tofauti na hapo ni habari nyingine
Ni wazi hapo ulipo muda huu umezama kwenye fikra nyingi kuhusu maisha unaongea na wewe mwenyewe unajiumbia hofu na mawazo ya kutisha na kushindwa...unautesa mwili na ufahamu wako bure kwakuwa wewe sio wewe hivyo vitu vikishatengana
Jiulize tena huwa ukiongea pekeyako unaongea na nani?utapata jibu la kushangaza mno![]()
Jamani nashukuru kwa michango yenu.Lakini hili ni tatizo limenisumbua muda mrefu na msichukulie kiwepesi.Nitaridhika roho yangu iwapo nitajibiwa kwa dalili aitha za biblia au quran.Mimi sijisemeshi mwenyewe bali sauti hii huniteka nyara na kuongea.Yaani ina ni override.Ndio ulimwengu wa ndani ni roho ni nafsi ni ufahamu
Roho ni kama betri
Nafsi ni kama nguvu itokayo kwenye betri
Ufahamu ni kama ile nguvu ya nafsi kusambaa na kufanya kazi husika
Hii package ndio inaunda ulimwengu wa ndani
Je ungependa kufahamu na ulimwengu wa nje?
Ufahamu unapofanya kazi husika mara nyingi huanzia hapo kwenda ulimwengu wa nje
Kama ni simu utampigia mtu au kutuma msg
Kama ni gari litatoka hapo lilipo na kwenda pengine
Kama ni mashine itafanya kazi husika
Na kama ni mawazo utawaambia wengine au utafanya kitendo
Je ni kama hallucinations? I mean mauzauza ndani ya Kichwa? Sauti isiyokoma kama mwangwi?J
Jamani nashukuru kwa michango yenu.Lakini hili ni tatizo limenisumbua muda mrefu na msichukulie kiwepesi.Nitaridhika roho yangu iwapo nitajibiwa kwa dalili aitha za biblia au quran.Mimi sijisemeshi mwenyewe bali sauti hii huniteka nyara na kuongea.Yaani ina ni override.
POA MKUU WA KAZINina mada yake subiri niisake
Ukiipata ni tag pmNina mada yake subiri niisake